MADRID, Hispania
MSHAMBULIAJI hatari wa timu ya soka ya Barcelona, Lionel Messi ameanza kuwarusha roho Manchester United.Mshambuliaji huyo amesema anatrajia
kutoa maumivu tena kwa timu hiyo ya Alex Ferguson, Jumamosi katika fainali ya Ligi ya Mabingwa.
Mesi ambaye ni mchezaji bora wa Dunia wa mwaka wa Barcelona, ndiye alifunga goli la pili katika fainali ya mashandano kama hayo miaka miwili iliyopita mjini Rome, ambapo Barca ilishinda mabao 2-0.
Ilikuwa ni shambulio la kwanza la Messi kwa klabu hiyo ya Uingereza, kati ya mashambulizi 10.
Nyota huyo wa Argentina alisema: "Ilikuwa ni hisia nzuri kwa jinsi goli lilivyokuwa na maana kwangu, kwa timu na mashabiki ni kumbukumbu nzuri.
"Ninatumaini kufunga tena Wembley. Ninatumaini kufunga tena kama haikuwa hivyo ninachotaka ni kuifunga United na kutwaa kombe. Nitacheza mechi kwa kujituma kama ni ni mechi yangu ya mwisho kama vile fainali. Sitaki kuikosa."
Messi alisema kuwa Barcelona, itacheza mpira wake wa ushambuliaji na kuionya United kwamba watacheza pasi nyingi kama ilivykuwa Rome.
Aliongeza: "Sijui Machester United itachezaje. Kunakuwa na timu ambayo hukaa na mpira na kutengeneza nafasi. Lakini tutajaribu kucheza uchezaji wetu kwa kukaa na mpira na kutengeneza nafasi."
Lakini Messi alikiri kuwa, Wayne Rooney na wenzie hawatakuwa na kazi rahisi. Alisema: "Kumbukumbu nzuri za Rome tayari ziko nyuma yetu. Kwa ujumla itakuwa ni mchezo tofauti na ule wa miaka miwili iliyopita.
"Tutakutana na upinzani mkali kwa timu yenye wachezaji wazuri. Itakuwa ni mechi iliyo balansi vizuri."
Messi alimsifia mchezaji wa United kutoka Mexico Javier Hernandez 'Chicharito', ambaye amecheza Old Trafford kwa msimu wa kwanza.
Alisema: "Chicharito amekuwa ni mchezaji muhimu kwa United, ambapo amefunga magoli mengi muhimu.
"Nilicheza dhidi yake katika Kombe la Dunia na pia alifunga dhidi yetu.
"Ni mchezaji mwenye kasi, anatumia akili sana na amezoea vizuri uchezaji katika klabu kubwa kama United, katika msimu wa kwanza."
Messi alipingana na mawazo kuwa United ni dhaifu kuliko timu iliyocheza na Barca miaka miwili iliyopita na haitakuwa na Cristiano Ronaldo.
Alisema: "Wameshinda Ligi Kuu na wametinga fainali ya Ligi ya Mabingwa kwa hiyo hawawezi kuwa dhaifu na kupata mafaniko kama haya."
Lakini bado ninaona kuwa kuna mshindi mmoja.
Alisema: "Nilijua katika maandalizi ya msimu tulikuwa na timu nzuri na kuwa na nafasi ya kutwaa kila kitu kwa mara nyingine, "Kila wakati nimekuwa na hisia tunakwenda kushinda kwa timu tuliyonayo."
No comments:
Post a Comment