Na Addolph Bruno
BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Benson Mwakyembe ametimiza ahadi yake ya kumnyuka mpinzani wake raia wa Uganda, Kakande Charles baada ya kupimga
kwa KO katika pambano lisilo la ubingwa, lililofanyika Ukumbi wa Travertine, Dar es Salaam juzi.
Mwakyembe alimchapa, Charles katika pambano hilo la raundi ya 10 lililokuwa na upinzani kwenye raundi ya sita.
Pambano hilo lilianza kwa Mwakyembe, kuanza vyema katika raundi ya kwanza hadi ya tatu ambazo alionesha uwezo mkubwa wa kumrushia makonde mazito mpinzani wake, lakini katika raundi ya nne walitoshana nguvu.
Raundi ya tano iliendelea kwa mabondia wote kwenda sawa, lakini ilipofika raundi ya sita Mwakyembe alimrushia makonde mazito mfululizo mpinzani wake na kusababisha kudondoka kwenye kamba, hali iliyosababisha mwamuzi wa mchezo huo Ali Bakari 'Champion' kusimamisha pambano.
Baada ya kusimamishwa kwa pambano hilo bondia, Charles alionesha ishara ya kuwa asingeweza kuendelea na kufanya majaji wa mchezo huo kumpa ushindi wa KO, Mwakyembe na mchezo kumalizika.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa pambano hilo, Mwakyembe alisema ushindi alioupata umetokana na maandalizi mazuri aliyoyafanya awali na sapoti ya mashabiki waliojitokeza kumshangilia.
"Lakini pamoja na hayo yote, naomba mjue huyu jamaa ni mzuri sana anacheza vizuri na anajua jinsi ya kumweka sawa mpanzani wake, mabondia tunaotegemea kupigana mapambano ya kimataifa, tunahitaji kufanya maandalizi kiukweli," alisema Mwakyembe.
No comments:
Post a Comment