03 May 2011

Mukama; CCM haina orodha ya mafisadi

*Yakanusha kuwapa siku 90

Na Mwandishi Wetu

CHAMA  Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kwamba japokuwa kuna tuhuma za ufisadi dhidi ya baadhi ya makada na  viongozi  wake, bado hakina
majina rasmi ya watuhumiwa hao, kama inavyodaiwa na vyombo vya habari nchini huku kikikanusha  kwamba kilitoa siku  90 kuwatimua wanachama hao.

Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa CCM,  Bw. Wilson Mukama  alipokutana na wahariri wa vyombo  mbalimbali  vya habari  kwa  lengo la kufahamiana na  kutambulisha sekretarieti mpya ya chama hicho.

Hatua hii inazua  maswali mengi miongoni mwa umma  na wanachama wa CCM , ambao bado wamegubikwa na utata juu ya nani hasa analengwa  katika operesheni hiyo maalumu inayojulikana  kama ‘kujivua gamba’  ambayo wachambuzi wanasema  huenda ikawa ngumu kwa CCM katika utekelezaji wake.

Tayari  vyombo vya habari nchini vimekuwa vikiwataja makada  watatu wa CCM kuwaoanisha na hatua  ya kuvuliwa nydhifa zao ndani ya chama akiwemo Waziri Mkuu aliyejiuzulu Bw. Edward Lowassa, Mwanasheria mkuu mstaafu, Bw. Andrew Chenge na Mbunge wa Igunga, Bw. Rostam Aziz .

Hata hivyo, Bw. Mukama  aliyeonekana kukwepa kujibu moja kwa moja  maswali ya waandishi hao alibainisha kuwa orodha ya watu 11 wanaodaiwa kuwa mafisadi  iliyotolewa na Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt.  Wilbroad Slaa sio ya CCM .

“CCM haina orodha ya mafisadi. Kilichopo ni kwamba tunarajia utekelezaji wa hotuba ya mwenyekiti wetu pamoja na maazimio ya Halmashauri Kuu ya chama iliyokaa katika kikao chake mwezi uliopita,” alisema Mkama.

Pamoja na hayo Katibu Mkuu huyo alisistiza kuwa CCM imepania ‘kuwatema’ wanachama wote wanaohusishwa kwa namna yoyote katika tuhuma za ufisadi  kwani uamuzi huo ni moja ya maazimio ya NEC lililopitishwa kwa kauli moja katika kikao hicho.

Akisoma Azimio  namba 15 la  NEC, alisema  NEC ilisisitiza kuwa chama kitaendelea na mapendekezo yake dhidi ya ufisadi aidha viongozi wote waliotuhumiwa, watafakari, wapime na wachukue hatua.

Alisema mbali ya Azimio hilo, hotuba ya Mwenyekiti wa chama hicho Rais Kikwete ilisisitiza kuwataka wote wanaotuhumiwa kwa ufisadi  watafakari na kuchukua hatua.

“Wasipofanya hivyo, basi tunatarajia kwamba chama kitachukua hatua kupitia Tume yake ya Maadili ambayo imeongezewa nguvu na kwa kuongezewa  idadi ya wajumbe,”  alisema.

Hatua hii inakuja ikiwa imebaki mwaka mmoja kwa chama hicho kufanya uchaguzi wake mkuu na miaka minne kabla ya uchaguzi mkuu wa rais, na wabunge na madiwani.

Katika mkutano huo ambao ulitawaliwa na maswali mazito  ya waandishi, Bw. Mukama alikanusha pia hatua ya CCM kudaiwa kuwapa siku 90 watuhumiwa ufisadi na bila kufanya hivyo watatimuliwa.

“ Haya yakusema siku 90 sijui yametoka wapi, kwa utaratibu NEC inakutana mara tatu kwa mwaka hapo pana miezi minne, huenda mtu alidhani NEC inakutana baada ya miezi mitatu na kudai tumeweka muda huo,” alisema.

Alisema  mabadiliko yaliyofanyika kwenye Kamati Kuu ya chama na sekretarieti ni  hatua ya kawaida ya kitaasisi na kinachotafsiriwa na wananchi ni tofauti kabisa na makusudi ya chama hicho.

“Tunaamini kwamba mageuzi ya kisiasa yanakua kwa kasi sana hapa Tanzania. Sisi kama CCM tunajiweka sawa kukabiliana na mabadiliko haya, kwa kuanzia ngazi ya juu kuelekea chini,” alisema Bw. Mukama.

Bw. Mukama alisema kwamba ufumbuzi wa matatizo ya kiuongozi ya CCM ya umeanzia katika ngazi za juu na inatarajiwa kuendelea katika ngazi za chini ili kurudisha imani kwa wananchi.

16 comments:

  1. Kwa hiyo Nape na Chiligati walitunga?, au mafisadi wametishia kufichua madudu ya MWENYEKITI?, Haiwezekani NAPE na CHILIGATI WOTE WAONGOPE NA SASA MMEWAPIGA STOP, DUH KWELI NIMEAMINI CCM BILA MAFISADI HAIWEZEKANI, NGUVU YA EL, RA, WATZ TUMEIONA. MKUU WA KAYA TWO IN ONE, JUZI ALISEMA KAULI YA NAPE NDIO MSIMAMO WA CHAMA LEO MAKAMBA MPYA KAJA NA SINGO NYINGINE.TULIYAJUA MAPEMA, CCM NA MAFISADI DAMDAM, INGEKUWA AJABU,AU GAMBA ALILENGWA MAKAMBA?. NYINYI ZZM MPAKA MSHINIKIZWE NA DK SLAA NDIO MNALETA USANII, CHADEMA WAKIPOA HAMTEKELEZI. TUMEWASOMA.

    ReplyDelete
  2. Ama kweli ukishangaa ya Musa utaona ya Firauni. Siamini huyu ndiye Katibu Mkuu mpya aliyesifiwa saaana kulinganisha na Yusufu Makamba kwamba wataisaidia CCM kujisafisha. Kauli ya watuhumiwa wa ufisadi kupewa siku 90 tumemsikia Mwenyekiti Mh. Kikwete akitamka kwa kinywa chake. Halafu Kamati mpya iliyochaguliwa baada ya ile ya zamani kujiuzulu wanatamka kwenye majukwaa kusisitiza Mafisadi wasipotii tamko hilo walilopewa kujivua madaraka ndani ya chama siku 90 zikipita watapewa barua. Leo hii tena huyu Mukama anajikanyaga si ajabu huyu ataikoroga CCM hata baadaye tumkumbuke Makamba. Jamani hii CCM kila anayepewa madaraka kwa uzoefu wangu atanyamazishwa tu. Baada ya muda tunamshangaa naye ni fisadi. Hata hivyo hao mafisadi wanaotajwa ni marafiki wa Mwenyekiti hawafanywi lolote. Hotuba zinazotolewa kwenye majukwaa ni kiini macho.

    ReplyDelete
  3. Mukama alipo jidai bila aibu kule Zanzibar kwamba chama pekee chenye itikadi ni CCM na kwamba itikadi hiyo ni ujamaa na Kujitegemea nilimdharau. Lakini ni yeye Mukama na majuha wenzake wamekuwa wakipita wakitangaza kwamba watuhumiwa wa ufisadi watatakiwa wajiuzuri nafasi zao za uongozi. Iweje leo anashangaa!!?Nashauri ajiuzuru mara moja ktk nafasi hiyo kabla hajaleta maafa makubwa kwenye Chama chetu.

    ReplyDelete
  4. Nguvu ya pesa, binafsi siamini kwamba Mukama anazungumza upuuzi namna hii, ina maana mmetuona watanzania wote mazuzu sio, siku tisini mlitoa wenyewe leo unasema hamkutoa,endelezeni Movie yetu mbongo na macho.

    ReplyDelete
  5. ndio ujue waandishi wa habari huwa wanahuzuria tu baada ya wenzao kuwa wameketi kivyao pale wanapoalikwa wanapewa uongo tu mikakati wenzenu wameisha ipanga mbinu zote wenzenu wanazijua ndiomaana hata humsikii mtiu hata mmoja aliyrtajwa kwa kile amakipi hawajasema kitu hapo ndugu zangu waandishi pagumu msiende kuwahoji hao wanayao mengi ambayo hamtayapata ili mtudanganye

    ReplyDelete
  6. Watanzania tukubali kuwa CCM haina nia ya dhaati ya kulikomboa taifa hili. Mbali na kutuhadaa. Tuachane nao.

    ReplyDelete
  7. Watu wenye akili timamu kama watanzania waliowengi siku hizi walisema toka awali kuwa, Haakuna kitakachofanyika ndani ya CCM hii ya sasa ambayo tuliiamini sana huko nyuma. Ufisadi na madudu mengine yote ambayo tumekuwa tukiyashuhudia yakifanywa na viongozi wetu ni JADI na sio bahati mbaya. Dhuluma kwa wananchi wao ni kitu kilichohalalishwa kuanzia kwa Mwenyekiti. yeyote anayejaribu kuukana ukwweli na aabike sasa. Kwani hata waliokuwa waapanda majukwaaani kujisifu na kuuhakikishia umma juu ya dhamila yao ya kuwawajibisha mafissadi, nao sasa wanakana maneno yao kama bwana willison mukama. Je bado tunahitaji kuendelea kuwaamini CCM kuongoza nchi yetu? Kwa vyovyote vile, anayeendealea kutetea CCM basi anamasilahi yake binafsi na hana mapenzi na watanzania wenzake.

    ReplyDelete
  8. Hivi mliwachagua kwa kura chache na zingine wakachakachua mnafikiri wanaubavu wa kuwaacha wafadhili (mafisadi) waliojitoa mhanga kupata lawama lakini ukweli ni kwamba fisadi anaewatumia ni CCM. Jibu ni kuwamwaga tu kabisa tuachane na viwavi hawa wasioshiba.

    ReplyDelete
  9. CCM ni chama kubwa kaeni kubwabwaja na maneno yakitoka kwa huyu vuvuzela wenu ndio ya busara ambayo ni uongo dhahiri lakini huku ni uongo!!Acheni umbumbumbu huwoooo,YA NGOSWE MWACHIE NGOSWE, NA YA MAJUHA TUNAWAACHIENI,KALAGABAHO

    ReplyDelete
  10. ccm achen kupoteza muda kwenye majukwaa huku mkiendelea kula bure vya watanzania. tuvueni gamba la maisha magumub mliyotuvisha ndpo tuwaelewe.kikwete n zaid ya punguan.anzen kumwondoa yeye kwan n aibu ccm n a serkal

    ReplyDelete
  11. hakuna msafi aneyeweza kuteuliwa na mchafu. kwa vyovyote vile haiwezekani kwani huyu msafi aweza kumwaibisha siku moja aliye mteua. hivyo sikutarajia kuwa Kikwete angeweze kumteua katibu mkuu aliyetofauti naye sansa kimaadili. kauli ikitoka imetoka huwezi kuimeza tena si tunasubiri siku 90 siishe tuounekitakachofuata, tuthibitishe kwa maranyingine kuwa ccm imedhamiria kuwalinda mafisadi kwa gharama yoyote ile hata ikibidi kuendelea kuwaangamiza watanazia. kwahiyo Mkama anendeleza ya bosi wake

    ReplyDelete
  12. Jamani ccm kwa mara ya kwanza nashuhudia ikiwa mikononi mwa mtu zaifu kuliko wenyeviti wake wote walopita. eee ndiyo ni kweli mbona wewe mwanamtandao unonekana kuukataa huu ukweli ulowazi! Ivi wewe Kikwete unataka ukiue chama kwa kukumbatia rafiki zako, kwanini usiwe strong km mwenzako Mkapa! Ndiyo hata kipindi cha mkapa mafisadi walikuwepo lakini hawakuchezea chama kiasi hiki unatia aibu kwa udhaifu wako. Yaani mnafanya madudu mpaka Chadema mnawapa fursa ya ku-win support kubwa ya UMMA-yaani mpaka wasukuma wa mwanza na Shinyanga, wakere etc ambao ni too royal kwa chama na serikali wamechoka chini ya uongozi wako!!No no, tusiwanyooshee vidole chenge, rostam na lowasa peke yao bt also our chairman for he is so sleepy to decide. Wananchi wanawasikiliza chadema si kwasababu chadema wanajua sana kukampeni no!, ila kwasababu chadema wanaongea ukweli na wananchi wanaona! Chadema wanapata supporters wengi kwasababu ya kusema ukeli wa madudu ambayo chama chetu na serikali yake vinafanya. Ivi kweli mwenyekiti, hata km hao rafiki zako walikupa hela za kupata urais waambie imetosha na muda ulobaki uwatumikie watanzania kwa maslahi ya nchi na wewe binafsi itakuwa faraja kwako baada ya kustafu watu wakukumbuke kwa jinsi ulivyoleta maendeleo ktk nchi na chama na siyo wakukumbuke for deepening makundi, grand corruption and disfunctional friendship! CCM imefikia kipindi mtu unaona aibu kutaja mbele za watu wenye akili timamau kuwa wewe ni mwanachama wa ccm si kwasababu watakupiga au kukuzomea no, ila nafsi inakusuta labda uwe kiongozi km kina mkama, nape, chiligate,wabunge etc ambao huwezi kuficha identity. Kiukweli inaboa saaana. Haya makundi yanaharibu si chama tu, walio kwenye makundi wana majimbo na kanda wanazotoka, so tuwe makini kwani yaweza kuwa ya kikanda na hivyo kuharibu kabisa misingi ya utaifa. Narudia tena mwenyekiti kwa kipindi chako hili jambo limezidi please help out the country social, political and economic stability. Mungu ibariki Tanzania!

    ReplyDelete
  13. Nyie pigeni domo tu, ila usiku mtaenda lala kwenye vigodoro vyenu. Kwani mmesahau kama nyie ni WADANGANYIKA? Na hawa wazee wa KUJIVUA MAGAMBA wanalijua hilo vizuri sana, that's why wanaendeleza usanii wao kwa sababu mmekuwa WADANGANYIKA watiifu. Nape, Chiligati walisema kuhusu kuwapa siku 90 watuhumiwa wajiondoe. Wilson Mukama akakumbuka sie sio WATANZANIA bali ni WADANGANYIKA na ametekeleza dhamira yake! Tatizo ni MUKAMA au sisi WADANGANYIKA? Jamani tuwapatie likizo hawa wazee wa MAGAMBA mwaka 2015 wakatafakari upya.

    ReplyDelete
  14. Niliposikia habari ya kujivua gamba nilijua ni usanii. Nawapa pole sana walioamini / wanaoamini katika porojo hii!!!!!

    ReplyDelete
  15. Masikini mzee mkama.....njaa kumbe inakuangaisha hivi1 unasema uwongo wazi wazi! Oh.... njaa mbaya!

    ReplyDelete
  16. Hata huyo kiongaozi wenu Slaa,angeshika madaraka ndio ingekua pumba zaidi na sera zake za alinacha. Inaingia akilini kuwa binadamu unaweza kuwafanyia binadamu kila wakihitajicho. Sasa bora waliopo sasa hivi lakini huyo "SILAHA" Ndio atakua "NYANGUMI" badala ya"MAPAPA" waliopo

    ReplyDelete