03 May 2011

Jinsi Osama Bin Laden alivyouawa

*Maiti yake yazikwa haraka baharini
*Wamarekani walipuka kwa furaha

WASHNGTON, Marekani

MWANZILISHI na kiongozi wa kundi la kigaidi la Al Qaeda, Bw. Osama Bin Laden ameuawa na
majeshi ya Marekani nchini Pakistan, Rais wa Marekani,  Bw. Barack Obama amesema.

Kabla ya Rais Obama kuutangazia ulimwengu juu ya kifo hicho, maofisa wa Serikali walisema kuwa usiku wa giza, helkopta za Marekani zililivamia jengo la kifahali lililokuwa na ukuta mrefu nchini Pakistan ama kwa lengo la kumkamata kiongozi huyo wa ngazi ya juu wa ugaidi au kumuua.

Wamebainisha kuwa katika kipindi cha dakika zisizozidi 40, Bw. Bin Laden alikuwa ameshauawa sambamba na watu wengine wanne, na kufanikisha kile Marekani ilichokuwa inahangaika nacho kwa miaka 10 iliyopita bila mafanikio.

Jengo la Kifahari

Wakati iliaminika kuwa Bin Ladema anaishi mapangoni ama Afganistan au Pakstani, taarifa za kifo hicho zimebainisha kinyume chake, kwani alikutwa kwenye jengo la kifahari.

Maofisa hao waliothibitisha taarifa hizo walisema kuwa jengo hilo linasadikika kuwa lilijengwa miaka mitano iliyopita umbali wa kilometa 100 kutoka Kaskazini mwa mji mkuu wa Pakistani, Islamabad maalumu kwa ajili ya kumficha Bw. Bin Laden.

Hata hivyo, maofisa hao wa ngazi ya juu walikataa kutaja idadi ya wanajeshi waliotumika katika mpango huo lakini wakawaeleza waandishi wa habari jinsi hali operesheni ilivyofanyika.

Wakizungumza kuhusu muundo wa jengo alimokutwa kiongozi huyo, maofisa hao walisema kuwa lilikuwa la vyumba vitatu likiwa na madirisha kidogo yaliyojitokeza kwenye ukuta mrefu uliokuwa na urefu wa futi saba.

Walisema kuwa walilibaini jengo hilo kuwa huenda linahifadhi magaidi wa ngazi ya juu akiwemo Bw. Bin Laden baada ya kazi ya ujasusi iliyochukua miezi kadhaa.

Kwa mujibu wa maofisa hao jengo hilo ambalo linakadiliwa kuwa na thamani ya dola milioni moja hapakuwepo na huduma ya simu wala internet na wakasema kuwa wakati wa shughuli hiyo helkopta yao moja ilianguka kutokana na sababu za kiufundi.

Kauli ya Rais Obama

Katika taaifa yake Rais Obama alisema kuwa kwa mujibu wa taarifa za kijasusi, kiongozi huyo wa al-qaeda aliuawa katika operesheni ya ardhini nje ya mji wa Islamabad baada ya ufyatulianaji wa risasi, majeshi ya Marekani yalichukua mwili wake.

Bw. Bin Laden anashutumiwa kwa kuhusika katika baadhi ya vitendo vya ukatili ikiwemo mashambulizi mjini New York na Washington, mnamo Septemba 11, 2001.

Kifo chake ni pigo kubwa kwa kundi la Al-qaeda lakini kuelezea hofu kuwa huenda wakashambuliwa katika mashambulizi ya kulipiza kisasi.

Bw. Obama alisema alielezea Agosti mwaka jana kuhusu mahali  alipokuwa amejificha Bin Laden na kufuatia uchunguzi wa kijasusi waligundua kuwa amejificha nchini Pakistan.

Wiki iliyopita alitoa amri operesheni kufanyika kumsaka Bin Laden na akasema kuwa operesheni hiyo iliendeshwa na kundi ndogo la wanajeshi wa Marekani katika eneo la Abbottabad, Kaskazini mwa Islamabad.

"Baada ya ufyatulianaji wa risasi, Bin Laden aliuawa na mwili wale kuchukuliwa na majeshi ya Marekani," alisema Rais Obama.

Rais Obama na maofisa wa ngazi ya juu walisema kuwa hakuna mwanajeshi wao hata mmoja aliyejeruhiwa wakati wa oparesheni hiyo iliyofanyika juzi asubuhi kwa muda wa saa za Pakistan.

Hata hivyo, viongozi hao hawakutoa taarifa zaidi lakini maofisa wa kikosi cha wanamaji walisema kuwa kikosi chao kilihusika huku maofisa wengine wakisema kuwa walitumia njia mbalimbali ili kutambua maiti hiyo kama ni ya Bin Laden.

Osama azikwa baharini

Taarifa mbalimbali zilizosambaa kwenye vyombo vya habari zilisema kuwa tayari mwili wa Bin Laden umeshazikwa baharini kwa kufuata taratibu za kiislamu zinazolazimisha mwili huo kuzikwa ndani ya saa 24, lakini hawakutoa taarifa zaidi ya hapo.

Maafisa wa Marekani ambao hawakutaka kutajwa majina walisema ingekuwa vigumu kupata nchi ambayo ingekubali kupokea mwili wa Bin Laden kutoka na vitendo vyake, hivyo wakalazimika kuuzika baharini.

Hata hivyo kitendo hicho kimeibua maswali mengi, huku watu wakijiuliza ni kwa vipi azikwe haraka na wasioneshe mwili wake, jambo ambalo lingeifanya dunia kuamini kuuawa kwake.

Bin Laden ni nani?

Histroa inaonesha kuwa kiongozi huyo ambaye jina lake kamili anaitwa Bw. Osama bin Muhammad bin Awad bin Laden, alizaliwa mjini Riyadh, Saudi Arabia mwaka 1957.

Kwa mujibu wa historia hiyo kinara huyo alikulia kwenye familia yenye utajili akiwa mtoto wa 17 kati ya watoto 50 wa mzee Mohammed bin Laden, ambaye alikuwa mataalamu wa ujenzi akiwa na mahusiano na familia ya ukoo wa kifalme.

Bin Laden, ambaye mama yake ni raia wa Syrian, alikulia katika madhebu ya Kiislamu ya Wahhabi na alipata elimu yake nchini Saudi Arabia na baba dyake alifariki kwenye ajali ya ndege mwaka 1967.

Alioa mke wa kwanza raia wa Syria akiwa na umri wa miaka 17 na inasadikika kuwa amezaa watoto zaidi ya 20 kutoka kwa wanawake watano.

Akiwa kijana mdogo alijiunga na mshirika wake, Bw. Abdullah Azzam nchini Afghanistan ili kupambana na majeshi ya uvamizi ya Kisovieti na kuanzisha kundi la Maktab al-Khadamat na kwa kutumia utajili wake aliwekeza fedha nyingi katika vita hiyo na kufanikisha ununuzi wa silaha.

Mwishoni mwa miaka ya 1980 alirejea nchini Saudi Arabia akiwa shujaa wa mujahideen baada ya kuyashinda majeshi ya Russia na kisha akaanzisha mtandao wake wa siri wa kundi la al-Qaeda, na wakati Irak ilipoivamia Kuwait mwaka 1990, na kisha Saudi Arabia ikakubali majeshi ya Marekani kutumia ardhi yake ndipo akaigeuka nchi alipozaliwa kwa kitendo cha kuruhusu majeshi ya  Marekani kutumia ardhi hiyo.

Baada ya kukwaruzana na serikali ya Saudia huku fedha zake zikiwa zimezuiwa, mwaka 1992 Bin Laden alikimbilia uhamishoni nchini Sudan akiwa na wapiganaji wake wa kundi la Mujahideen na hatimaye kuunganisha nguvu zake na kundi la Kiislamu la nchini Misri liitwalo Egyptian Islamic Jihad ambalo lilikuwa likiongozwa na Bw. Ayman al-Zawahiri.

Hata hivyo mwaka 1995 kundi hilo lilifukuzwa Sudan baada yakujaribu kumuua aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Bw. Hosni Mubarak.Baadaye Bin Laden alirejea nchini Afghanistan ambako alikuwa akilindwa na utawala wa Taliban uliokuwa chini Bw. Mullah Mohammed Omar na kuanzisha kambi ya kutoa mafunzo kwa kundi la al-Qaeda ambalo limekuwa likifanya mashambulizi maeneo mbalimbali duniani.

14 comments:

  1. Sijaujua utakatifu wake, lakini jamaa wanamsifia na kumtukuza sana kama Mungu mtu vile! na wengi wanadai kuwa ni uwongo hajafa! Ama duniani tumezongwa na unafiki wa hali ya juu!

    ReplyDelete
  2. Osama si lolote yule ni muuwaji tu ayejaa mapepo. Osama na kundi lake wali-underestimate nguvu ya marekani. Mungu ibariki marekani.

    Erick Michael Kitundu
    Dallas,Texas

    ReplyDelete
  3. hayo ni mambo ya kisiasa, baada ya obama kukumbwa na kashfa ya uraia wake wameona watumie mbinu hiyo kumpa umaarufu kwamba amefanya kazi kubwa ili kufuta tuhuma yake.
    kama kafa kwa nini wamzike haraka? kama kafa nadhani wamarekani na mataifa mengine yangefurahi na kumsifu obama na marekanai kwa ujumla kama angeonekana

    ReplyDelete
  4. Hakuna anaemtukuza na kumfanya kama Mungu mtu,hizo ni fikra zako potofu!! Yule ni mpiganaji wa kutokomeza dhulma na mauaji zinazofanywa na mataifa ya magharibi,hasa Marekani na washirika wake,yeye ni jasiri fikiria miaka 10 anatafutwa yeye mpk sasa wanadai kumuua Osama feki,hakuna picha zaidi zilizoonyeshwa zaidi ya hiyo moja inayoonyesha kapigwa risasi jichoni, angalia ya uhai wake na hiyo ni picha ileile haina mabadiliko ila hiyo ina nguo na kilemba hiyo nyingine haina nguo ina damu uchwara wakati sasa kakonda ile bado ni mnene,ndevu zilezile,mdomo uko kama ule angalia The Citizen la leo!! Ni mbinu chakavu kama kweli wamemuua arudishe askari wake walioko Afghanistani aone kimbembe!!

    ReplyDelete
  5. Ukitaka kujuwa kinachoendelea juu ya mbinu na vitimbi vya marekali kumbukeni 1) Unajua the first casualty in George W Bushu Iraq war was Truth? 2) unajua how Vetnaum war started? - find a book by Proffessor Mamdan. Kumbuka Mtanzania tusiwe kama vyombo vyetu vya habari Magharibu ikiseti agenda huibeba jujuu. Think whenever an event comes up Tusije sisi Watanzania tukaonekana tunaakili uchwara

    ReplyDelete
  6. Pole wewe kaka uchwara mimi naona umeingiwa
    na pepo mchafu unadhani sisi ni wa kuabudu sanamu au kiumbe kilichoumbwa na Mwenyeezi Mungu?Kaa ujuwe Uislamu ni DINI iliyoongoka na ina misingi yake thabit, na tegemezi na matumaini yetu Yapo kwa Subbhana wa Taghaala.Wewe kaa na matumaini yako na kutegemea misaada toka huko kwa wahisani wenu wasagaji na walawiti wakubwa
    waliokubuhu, kaa kimya wacha kuchezea Imani za Watu, huyo Osama ni mtu kama watu wengine na kila mtu anabeba dhimma yake mwenyewe, alikuwa kama walivyokuwa kina Hitler,Papa paul 11,na Hailesislasi,Iddi amini,Bush nk.

    ReplyDelete
  7. Anonymous tumechoka na msg zako hazina kichwa wala miguu..

    ReplyDelete
  8. MIMI NI MKRISTO,NASHANGAA WANAO FANANISHA MAOVU YA OSAMA NA UISLAMU?KWANI HAKUNA WAKRISTO WAOVU KAMA OSAMA?MUNGU WETU NI MMOJA, KILA MMOJA ANAWEZA KUKUBALI KUMTUMIKIA MUNGU AU SHETANI VITABU VYOTE VINASEMA HIVYO, FIKIRINI KABLA YA KUTOA MAONI YENU, MOTO HUAZA NA CHECHE.KLA MMOJA ATAJIBU YANAYO MHUSU MBELE YA MUNGU. MUNGU IBARIKI TANZANIA

    ReplyDelete
  9. nimeshasema sana kuhusu huyu mtu anayezungumzia udini, angalia usimdhihaki Mungu wako ndugu yangu, na usimbeep kwani yeye kukupigia ni mara moja tu

    ReplyDelete
  10. Unajua Osama alikvyokuwa na akili, ni mjanja wamarekani walimfundisha ukomandoo, wakamgeuka ktk mambo waliyoahidiana, ndipo alipoingia msituni kuwalipiza kisasi, kwa ujanja wake akatafuta kuungwa mkono kwa kichaka cha dini, akaficha kiini cha ugomvi wao, akipiga mahali anatangaza waislamu wamuunge mkono kwamba wameshinda, na ndg zangu waislam bila wao kujua wanameunga mkono wakidhani ni uislamu umeshinda, kumbe ni mambo yake peke yake , kwa kuthibitisha mbona amekataza watoto wake wasijiunge na al-qaeda?.Msishabikie mambo bila kujua , elewa mmarekani ni kigegeu mkipatana jambo asipolifanya ukimdai atakuchapa, ukiwa king'ang'anizi tu atakuita adui namba moja,dicho kilichotokea kwa osama, hakuna udini hapo,ila osama aliteka umma wa waislam na wao bila kutafiti wanamwita shujaa, ni bora kukaa kimya/kutokuwa mshabiki wa upande wowote kama hujui kinachoendelea.Sadam alikuwa komandoo wao na mtu wa karibu alipowageuka wakatafuta mbinu, visingizio chungu mzima wakamnyonga.Libya kuna mafuta tele,wananchi wamemchoka Rais wao ,marekani amejifanya kuwasidia ili wamuue waingie kiulaini wajichotee mafuta, lakini watu wasioelewa wanaingiza udini wangetaka kuupiga uislamu mbona ziko ncni zenye serikali ya Kiislam si wangezipiga mojakwa moja , kwani wanashindwa nini, lakini wanamlenga mtu walie na hoja naye, kumbe kuna mambo humo tofauti na dini.Hata hapa Tz tukibweteka saaaana kutegemea marekani na kuwaachia vitu vya maana wao siku tukisema sasa tutafanya wenyewe utaona wanavyogeuka na kuwa adui,wale hawana cha udini bali wanataka mahali penye maslahi yao wanufaike.

    ReplyDelete
  11. HUYU MTU ALIKUA AKAMATWA AKIWA HAI HALAFU AWATAJE NA WENZIWE WOTE WAHUKUMIWE KWA WALIOYAFANYA NA WAO WAONJE MACUNGU VIZURI LAKINI NA HAO WENGINE WATATIWA MKONONI SOON

    ReplyDelete
  12. HA HA HA HA KWELI WAISLAMU HAMUNA HAYA ETI SASA HIVI TU MUMESAHAU MULIYOYAFANYA KULE SAURI TANGA SI MULIUWA? SASA BABA YENU KAFA SASA SIJUWI NINANI ATAWASAIDIA KUFANYA MAUWAJI HUKO TZ NAJUWA KUWA NYINYI NIWAUWAJI WAKUU KABISA DINI YENU NI YA UPANGA SASA BABA YENU AMEKUFA KWA BUDUKI SASA SIJUWI KAMA BADO MUNATAKA KUEDELEA KUENEZA DINI YENU YA UPANGA, HONGERENI SANA NA ROHO YA UNYAMA MULIYONAYO SASA MUSISAHAU KUWA UBALOZI WA MAREKANE ULIOKO TZ NA KENYA NI NYINYI MULIHUSIKA SASA MUNAKATAA SI DUNGU YENU ANAOZA HUKO GEREZANI MAREKANE SASA NI SIRI MBONA MUNAJULIKANA KOTE. DINI YA UPANGA JA JA JA JA JA JA JA POLE SASA NAIHOFIA TZ MAANA NYINYI MUNAIPELEKA KUMWANGA DAMU KAMA MULIVYOZOEA. CHAUUUUUUUUUUU A DIOS

    ReplyDelete
  13. Uislamu ni dini ya amani na wala si dini ya upanga kama usemavyo wewe. Na huyo unaemuita baba yetu alikua na wake wangapi mpaka akatuzaa waislam wote. Ok nafikiri umeamua kuutukana uislam sio. Basi muda si mrefu utajua ipi CHACHU na ipi CHUNGU

    ReplyDelete
  14. Kwani kwani yule wa uganda anayeua watu kwa jina la baba na mwana mtakatifu ni muislamu. Dhulma ya marekani haitaiacha dunia ikae kwa amani milele,kafa osma lakini kuna zaidi ya osama kwa mamilioni wa kuendeleza hiyo na ndiyo unaoiyona huko arabuni sasa lakini nchi za magharibi zinajitia zinasapoti demokrasia wakati wao ndio waliokuwa wanawapa sapoti hao watawala. kifo cha osama ndio mwanzo wa mapambano kaeni sawa.

    ReplyDelete