25 May 2011

'Mtoto' ahukumiwa jela maisha kwa ubakaji

Na Suleiman Abeid, Shinyanga

MAHAKAMA ya wilaya ya Maswa mkoani Shinyanga imemuhukumu kwenda jela maisha sambamba na adhabu ya viboko 14 mtoto Dotto James (14) baada ya
kukutwa na hatia kwa kosa la ubakaji.

Akitoa hukumu hiyo juzi, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Maswa Bw. Thomson Mtani alisema ametoa hukumu hiyo baada ya kupata uthibitisho wa vipimo vya kitaalamu kutoka katika hospitali ya serikali wilayani Maswa ambavyo vimeonesha mshitakiwa ni mtu mzima kinyume na umri anaodaiwa kuwa nao hivi sasa wa miaka 14.
 
Mtoto James alifikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza mnamo Mei 15, kwa tuhuma za kumbaka mtoto mdogo wa kike mwenye umri wa miaka mitano (jina limehifadhiwa) na kumsababishia maumivu makali katika sehemu zake siri.

Awali Mwendesha Mashtaka wa mahakama hiyo Bw. Kidwadi Kalinga alidai kuwa siku ya tukio mshitakiwa alimkuta mtoto huyo akiwa na watoto wenzake wakicheza nje ya nyumba yao ambapo alimwita kwa madai ya kwenda kumnunulia pipi.

Bw. Kalinga aliieleza mahakama kwamba baada ya mtoto huyo kuitikia wito huo, mshitakiwa hakumpeleka kumnunulia pipi aliyokuwa ameahidi na badala yake alimkamata na kumpeleka katika nyumba aliyokuwa akiishi ambako alimfungia mlango na kuanza kumbaka sambamba na kumlawiti.

Alidai kuwa kutokana na kitendo hicho mtoto huyo alipata maumivu makali na kulia huku akipiga kelele hali ambayo iliwashitua wanakijiji waliokuwa jirani waliokimbilia nyumbani kwa mshitakiwa kwa lengo la kujua kilichosababisha mtoto huyo alie kwa nguvu.

Ilidaiwa kuwa mshtakiwa alikamatwa na wanakijiji akiwa katika harakati za kutoroka. 

Mshtakiwa huyo baada ya kusomewa shitaka lake alikiri kutenda kosa hilo ambapo al

2 comments:

  1. Ushauri wako ni wa kijinga mno. Inabidi uombewe!

    ReplyDelete
  2. We must introduce "jino kwa jino" punishment! Otherwise criminals won't learn any lesson

    ReplyDelete