FROLIDA, Marekani
MCHEZA mieleka, John Cena amewapongeza wanajeshi wa Marekani baada ya taarifa za kifo cha mtuhumiwa wa usukaji mipango ya ugaidi Osama Bin Laden.Rais wa
Marekani, Barack Obama ndiye alitangaza kuwa Bin Laden mwenye umri wa miaka 54 aliuawa katika operesheni iliyofanywa na kikosi maalumu cha Jeshi la Marekani Jumatatu, akiwa katika jumba lake la kifahari nchini Pakistan.
Cena alipata taarifa za kifo cha Osama, muda mfupi baada ya kushinda pambano lake la mieleka na kutwaa ubingwa wa WWE lililofahamika kama Extreme Rules, hakusita kuelezea tukio hilo lililofanikishwa na wanajeshi wa Marekani.
Alisema: "Ninaondoka hapa kila usiku nikiwa najidai, utii heshima moyoni.
"Huu ni uchotara niliourithi kutoka kwa mwanaume na mwanamke, ambaye anatetea uhuru wa nchi hii.
"Rais ametangaza kwamba tumemkamata na kummaliza kabisa Osama Bin Laden."
Akielezea ushindi wake, Cena aliongeza: "Hiki ni kitu fulani usiku, lakini ninajihisi kujivunia kuwa Mmarekani."
Cena mwenye umri 34, kisha aliondoka ulingoni katika Ukumbi wa Tampa, Florida na kwenda Stars and Stripes Forever.
No comments:
Post a Comment