MADRID, Hispania
TIMU ya Real Madrid, imeripotiwa kuwa inatarajia kupoteza wachezaji wake wanne muhimu katika
usajili wa majira haya ya joto.Gazeti la Marca liliripoti juzi kuwa
baada ya kipa wa zamani wa Liverpool, Jerzy Dudek kutangaza kustaafu soka, wachezaji
wengine watatu katika kikosi cha kwanza hawatakuwemo kwenye timu hiyo msimu ujao.
Wachezaji hao wanaotajwa kuwa watabwaga manyanga ni Sergio Canales,
ambaye anacheza kwa mkopo nje ya timu hiyo baada ya kushindwa kufanya vizuri,
wakati Pedro Leon na Lassana Diarra wanadaiwa kuwa wapo sokoni.
Kiungo wa
zamani wa timu za Chelsea na Arsenal, Diarra anahusishwa kutaka kurejea tena
Uingereza lakini hata hivyo bado hajaweka wazi maamuzi yake.
Timu za Manchester
United na Tottenham zinadaiwa ndizo zinafuatilia kwa karibu maendeleo ya
mchezaji huyo.
No comments:
Post a Comment