Na Grace Michael
SERIKALI ya Tanzania imepinga uamuzi wa Kampuni ya Vifaa vya Kijeshi nchini Uingereza ya BAE Systems kuunda jopo litakalosimamia malipo ya fidia ambayo iliamuliwa na
mahakama kuilipa Tanzania kwa kuwa uamuzi huo unakwenda kinyume na msimamo wa serikali ambayo inataka fedha hizo ziingizwe serikalini.
Mbali na hilo, imesema kuwa lugha iliyotumiwa na BAE kwamba fedha hizo zikiingizwa serikali zinaweza kutumika vibaya ni matusi kwa Serikali ya Tanzania na hivyo kuitaka Serikali ya Uingereza kushinikiza fedha hizo kurejeshwa kwa serikali ya Tanzania badala ya kuingizwa kwenye mashirika ya hiyari.
Uamuzi ulioitaka BAE kuilipa Serikali ya Tanzania kiasi cha paundi milioni 29.5 ulitolewa na Jaji Bean wa Mahakama ya Southwark ya Uingereza Disemba 21, mwaka jana baada ya jaji huyo kutoridhika na maelezo pamoja na makubaliano ya SFO na BAE ambapo mahakama iliamuru fedha hizo zilipwe kwa wananchi wa Tanzania.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe aliwaeleza waandishi wa habari jana, “Uamuzi huu wa BAE una lengo la makusudi kuonesha sura ya kutokuamini dhamira ya Serikali ya Tanzania kutumia fedha hizo kwa kusudi lililokuwa limetolewa.. Unalenga kuonesha umma wa Uingereza kuwa Serikali ya Tanzania inatawaliwa na rushwa na haiaminiki kuwatendea haki wananchi wake,” alisema Bw. Membe.
Alisema kuwa uamuzi huo unakwenda mbali zaidi kwa kupuuza ahadi iliyokuwa
imetolewa na Serikali ya Tanzania na Uingereza kuwa fedha hizo zitasimamiwa vyema, hivyo akasema Tanzania haiko tayari kukubaliana na uamuzi huo na badala yake inataka fedha hizo zirejeshwe serikalini ambako ndo ziliibwa.
Alisema kuwa kampuni hiyo inataka kujaribu kujikosha mbele ya asasi mbalimbali zisozo za kiserikali za Uingereza baada ya kukosolewa sana kwa kashfa ya rushwa, hivyo kutaka kujionesha kuwajali zaidi Watanzania.
“Serikali yetu ina uhusiano mzuri sana na Serikali ya Uingereza na serikali hiyo imekuwa mfadhili wetu mkubwa wa miradi ya maendeleo kwa miaka yote, tunaiomba Uingereza ituunge mkono katika kushinikiza BAE kurejesha fedha zetu Tanzania,” alisema Waziri Membe.
Akielezea matumizi ya fedha hizo ambayo yaliwasilishwa na Tanzania pamoja na Uingereza kuonesha namna zitakavyotumika, Bw. Membe alisema zingenunua vitabu vya kiada vya sh. milioni 4.4 kwa ajili ya shule za msingi, vitabu vya miongozo ya mitaa vya masomo 12 kwa shule 16,000, madawati 200,000, kujenga nyumba 1,196 za walimu katika wilaya zote nchini vifaa vya kufundishia na kujenga vyoo 2,900.
Awali BAE ilishtakiwa kwa kuongeza gharama za mauzo ya rada kwa Serikali ya Tanzania ambapo waendesha mashtaka wa SFO na BAE walikubaliana kuimaliza kesi hiyo nje ya mahakama kwa BAE kukiri kosa la kutoweka sawa kumbukumbu za fedha na mahesabu katika mchakato wa mauzo ya rada kwa Tanzani.
Kutokana na hali hiyo, BAE ilikubali kulipa sehemu ya faini hiyo kwa Tanzania kama sehemu muhimu ya makubaliano hayo.
Baada ya miezi sita BAE imekuja na uamuzi wa kuunda jopo litakalosimamia fedha hizo ikiwa na maana ya kutotoa fedha hizo kwa Serikali ya Tanzania bali kwa asasi zisizokuwa ya kiserikali.
MIMI NAISHANGAA SERIKALI YETU, WAKATI WATU WALIPIGIA KILELE RUSHWA HII SERIKALI ILIKAA KIMYA NA KUWATETEA MAOFISA WALOHUSIKA. MBAYA ZAIDI WALIENDELEA KUWA MADARAKANI. HATA WAKATI WA HUKUMU SERIKALI HAIKUWAKILISHWA NA OFISA YEYOTE, SASA IMEFIKA KWENYE FIDIA NDIO MISULI INATUNISHWA! ETI WANAHURUMA NA WANANCHI. KUMBUKA WAZIRI WA UENGEREZA ALIJIUZULU KWA UCHUNGU WA WATANZANIA. TUACHE SIASA KWENYE UKWELI. KAMA VIONGOZI WALISHAKULA RUSHWA YAO HIVYO VYOO NA MADAWATI WATAACHA KULA?
ReplyDeleteBora zipitie NGO kuliko kupitia mikononi mwa mafisadi ya tazifisadi hadi nusu yake.Chenge anatesa tu hana wakumshitaki.serikali ya Tanzania ya ajabu sana
ReplyDeleteNi aibu kwa serekali kukosa uaminifu, hii inaonyesha picha gani? Kama kweli serekali wanataka pesa hii irudi serekalini na ilitoka kwa udanganyifu, je waliohusika WAKO WAPI????
ReplyDeleteWe Membe umeona unataka kunyang'anywa tonge ndo unakuja juu. Hebu mkamate Chenge aliyesababisha upotevu halafu ndo udai pesa
ReplyDeleteTumekwisha washtukia bora zipitie NGO's hata zikitafunwa huko ni bora kuliko mzitafune mafisadi
WATZ HAMNA AIBU. VIGOGO WALILIPA HIZO HELA KWA NJIA YA RUSHWA AMA TUSEME KWA NJIA YA AMBAY SI SAHIHI . SASA WANAPOSEMA WAKIWARUDISHIA MTAZITUMIA KWA NJIA ISIYO HALALI MNALALAMIKA... HAYA SI MATUSI MNAAMBIWA UKWELI. MJIREKEBISHE. KWANZA MAFISADI MNAWAKUMBATIA THEN MKISEMWA MWALALAMA
ReplyDeleteTAARIFA ALIYOITOA MH WAZIRI KWA VYOMBO VYA HABARI INAONESHA NI JINSI GANI TULIVYO NA VIONGOZI GOIGOI. UINGEREZA NDIO WALIOWEZESHA TAARIFA ZA UFISADI ULIOFANYWA NA BAE NA WAMETUMIA GHARAMA KUBWA HATA HUKUMU IKATOKA AMBAPO BAE WALITAKIWA KUREJESHA HICHO KIASI CHA FEDHA.SASA KWA KIFUA MBELE MEMBE ANAROPOKA OVYO KUZITAKA FEDHA HIYO HUKU AKIJIU WAHUSIKA WAKUU WA DILI HILI NI PAMOJA NA ALIYEKUWA WAZIRI WA MABO YA NJE WAKATI HUO,WAZIRI WA FEDHA,MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI NA WADAU HAO WENGINE. KAMA MEMBE NI MZALENDO BASI HAWA WOTE NDIO WANGETAKIWA WALIPE HIZO FEDHA PAMOJA NA KUFILISIWA KWA HASARA HIYO NA SIO WAINGEREZA WATUREHEMU.
ReplyDeleteVIONGOZI WETU WANAANGALIA PU TU NA WAVIVU MNO KUFIKIRI NA HATA KAULI WANAZOZITOA HAT MTU AMBAYE HAJAKANYAGA DADASA ANAWASHINDA. KUNA LOGIC GANI KWA MEMBE KUWA MKALI KUTAKA FEDHA HIZO AKIDAI HATAKI MSAADA BALI HALALI YA WATANZANIA AKIJUA MUIDHINISHAJI NI BOSI WAKE NA WATENDAJI WENGINE AMBAO NDIO WANAOPASWA WASHAMBULIWE NA WALIPE KWA UDANGANYIFU WALIOUFANYA?
kutplewa pesa hiyo kwa NGO ni sawa kabisa serikali mara nyingi imekuwa na matumizi mabaya ya ya fedha za serikali zinapotolewa na wafadhili. wizara inayoongoza kwa matumizi mabaya ya fedha zinazotoka nje ni ya waziri mkuu ambayo haina uwoga kabisa hela za AMSDP zilizotolewa kujenga magara, barabara, maghara na masoko hazijalipwa kwa walengwa ingawa ADB ilileta fedha hiyo ni aibu kubwa sana. kitu kinachowafanya waingereza wapeleke kewnye NGO ni mipango iliyokuwa tayari ya kutumia pesa hizo kuwalipa Viongozi wa CCM kwenda kuwajibu CHADEMA.
ReplyDeleteMembe anaona pesa zikipitia Kwa NGOs hawatafaidika kuzila. Ndio maana anakomaa macho yamemtoka ili zipitie serikalini ziliwe tena. BAE ndo waliolipwa pesa hizo kwa wizi hivyo wanajua jinsi serikali inavyowaibia wananchi ndio maana wametubu na kupendekeza hilo.
ReplyDeleteMEMBE ACHA zipitie NGOs tufaidike wananchi wa hali ya chini. Zikipitia kwenu hatutaziona, Chonde chonde Membeeeee...!!!
Pumbafu! pumbafu! pumbafu kabisa hivi tuna viongozi wa aina gani?? Laiti Mwalimu JK angefufuka kesho wote wangekula viboko. HII KWA MAANA NYINGINE, UK WANAIONA SEREKALI YOTE YA TZ NI MBOVU YA KIFISADI, MEMBE UNATAKA MUAMBIWE KWA LUGHA GANI????
ReplyDeleteHawa waingereza wanawafahamu viongozi wa serikali ya tanzania ni wezi na mafisadi, ni heri kwenye NGO hata wakila nao watakuwa awamepunguza umaskini wao.Sasa Membe anatumiwa na mafisadi wa serikali ya CCM kuzikomalia ili waje wazile.Wakiamua kujenga hayo majengo anayodai ni lazima yatakuwa chini ya kiwango ikiwa ni pamoja na kuzidisha mchanga kwenye matofali ya simenti ili wale cha juu.Wakitaka tuwaamini basi MKAPA (Aliyekuwa Rais), CHENGE (Aliyekuwa mwanasheria mkuu),MRAMBA (Aliyekuwa waziri wa fedha),KIKWETE (Aliyekuwa waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa), SUMAYE (Aliyekuwa waziri mkuu),wanatakiwa KUKAMATWA NA KUSHTAKIWA. Hawa wanafahamu kila kitu kuhusu dili hilo maana lisingewezekana kama mmoja wao hajui.
ReplyDeleteHAKA KASIRIKALI KANANUKA RUSHWA..MFUU, NA WAKUU WAKE WANANUKA RUSHWA, HAMUONI AIBU MNAPOENDA MAMTONI NA HIYO HARUFU, MNAZANI WAZUNGU WAJINGA MNAVYOJUA KUPOTEZEA KWA TABASAMU NA MATAKWIMU YASIYO NA KICHWA WALA MIGUU MNAPOKUTANA NA WAZUNGU MAMTONI,
ReplyDeleteNI NOMA..YANI HUYU WASIRI ANASEMA ATANUNUA DAWATI, VITABU, SHULE ZA WALIMU NA MAMBO CHUNGU MSIMA..HIYO DANGANYA TOTO ANATAKA KUNDI KUBWA LA WATANZANIA LIMSAPOTI KATIKA UTEKELEZAJI WA HIYO JANJA YAKE, YAANI NI BORA HATA ZISIJE KULIKO ZITUE MIKONONI MWA SIRIKALI.
MI NAONA ZIENDE ZIKALIPE MADENI TUNAYODAIWA, TUTAJUA TUMEFANYA JAMBO.