Na Martha Fataely, Moshi
SERIKALI imeombwa kwenda mbali zaidi katika vita dhidi ya ufisadi kwa kuhakikisha inawadhiti, kuwafilisi na kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wote wanaotajwa kwani ni
sawa na wahujumu uchumi.
Mjumbe wa umoja wa vijana wa CCM (UVCCM) mkoa wa Kilimanjaro, Bw. Paul Makonda aliyasema hayo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari mkoani hapa ambapo pia alitaka utajiri wa wanachama wa CCM wahojiwe jinsi ambavyo wamepata mali hizo.
Madai ya Bw. Makonda yamekuja siku chache baada ya viongozi wa CCM kutoa taarifa zinazotatanisha, baadhi wakidai kuwa kwenye vikao vyake watu watatu walitajwa kuhusishwa na ufisadi na kupewa siku 90 kupima wenyewe na kuachia nyadhifa zao, huku wengine wakisema hayakutajwa majina wala orodha ya watuhumiwa hao
Bw. Makonda katika taarifa yake aliomba serikali iwahoji aliyekuwa Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa, aliyekuwa Mwasheria Mkuu wa Serikali, Bw Andrew Chenge na Mbunge wa Igunga, Bw. Rostam Azaz ili kujua wamepata wapi utajiri walionao.
Bw. Makonda alisema watuhumiwa wote waliotajwa katika tuhuma mbalimbali za ufisadi ndani ya nchi,wafilisiwe ili kuhakikisha rasilimali walizopora watanzania zinarejshwa.
Alisema pamoja na Kamati Kuu ya CCM kutoa muda wa siku 90 kwa watuhumiwa wenyewe kujivua nyadhfa zao lakini, ni vyema kwa serikali ikawafilisi ili iwe fundisho kwa wengine wenye nia ovu ya kujilimbikizia mali.
“Hawa wote wamechafuka na wananchi wanawatuhumu wanapaswa kufukuzwa CCM ikiwa ni pamoja na hatua nyingine za kisheria kuchukuliwa dhidi yao kwani wao ni majeruhi,” alisema.
Alisema wapo baadhi ya vigogo ambao wana utajiri wa kutisha hapa nchini wakati waliwahi kushika nyazifa mbalimbali hapa nchini lakini pia wamekuwa wakihusishwa na tuhuma mbalimbali za ufisadi.
“Tunaomba watu hawa wafilisiwe, utajiri wao uhojiwe kwani wameweza kuliingiza taifa katika mikataba feki mbalimbali wakati wakiwa na nyazifa za uongozi serikalini,” alisema.
Aidha Bw. Makonda ameendelea kutoa madai mazito kwa viongozi
wa UVCCM, Mwenyekiti Beno Malisa, James Millya, Hussen Bashe na Martine
Shighela, ambao alidai ni vibaraka wa watuhumiwa hao.
Bw. Makonda aliongeza kuwa iwapo Bw. Lowassa aliwahi kujiuzulu katika kashfa ya Richmond, mapema wakati bunge likiendelea na mjadala, basi anatakiwa kufanya vivyo hivyo katika hatua hii, pamoja na watuhumiwa wengine wote.
Kwa upande wake, Makamu mwenyekiti wa UVCCM, Bw. Beno Malisa, alipohojiwa alisema masuala ambayo yanaigusa taasisi yatajibiwa na taasisi husika na mengine anayozungumzia vijana Bw Makonda atajibiwa na vijana wa saizi yake.
“Ah sasa tusipoteze muda, huyo kama amezungumza hivyo,subiri atajibiwa na taasisi anazozitaja….mengine pia atajibiwa na vijana wa saizi yake, we chukua hilo ndiyo jibu sasa, au unataka jibu unalotaka wewe?" alihoji.
BONGO BWANA DOWANS NDIO TATIZO NA NI LAZIMA LILIPWE KWA SABABU MKATABA UPO NA YOTE HAYO NI MATUNDA YA CCM,MHASIBU WAO MKUU ALITUMIA PESA YAKE KWA PILAU NA POSHO SASA NDIYO MATUNDA YAKE.
ReplyDeleteHIVI DUNIANI KUNA MTU ANAYETOA PESA BILA KUPATA FAIDA SASA CCM MJUE WALE WALIOWAPA PESA ZA UFADHILI NDIO WANAZIRUDISHA.
TUNASUBIRI TUONE MATOKEO YA KUWANYANG'ANYA MALI ZAO HAYA WEEE
Kweli hii ni bongo,Mkama alisema hawana orodha ya mafisadi, sasa wewe uvccm unajifanya kutoa tamko ili watu wakuone wamaana, huna lolote songi ni lilelile tulilolizoea, mafisadi wakubwa mnawajua na hamuwezi wafanya kitu chochote, unajing'atng'ata hapo, una meno ya kuwala mafisadi.
ReplyDeletejitokeze basi umtaje hata mmoja tuone ujasiri wako ukowapi!!!
tetetetetete, humndanganyi mtu, tetetete,
Matamko ya CCM na wanaCCM hayasadikiki, hayatoki moyoni, hayana dhamira ya kuleta mabadiliko. si ajabu huyo kijana Makonda kesho akakanusha katakata kuwa hajawahi kusema hayo aliyoyasema. inasikitisha kwakuwa inaoneshajinsi tunavyopoteza mwelekeo sahihi kilakukicha.Hatahivyo ikosiku wenye dhamira yakweli wahanga wa ufisadi huu tutasema tusikike na tutasimamia tunachokisema huo ndio utakuwamwisho wa waongo na hao wanajiona miungu watu. Ulemwisho wao wenyewe umekaribia. Mungu yu pamoja nasi hatutahofia wauwaji mafisadi.
ReplyDeleteHii ngonjera ya CCM kujivua gamba, na mafisadi kupewa siku 90 inafaa kupelekwa katika mashindano - "is a good fiction"!
ReplyDeleteMwadhani CCM inao ubavu wa kuwanyoshea kidole mafisadi? Wanalindana na hakuna chochote watakachotendewa; yote muyaonayo ni kiini macho tu. CCM inajifanya imeondoa gamba, lakini sumu ni ile ile, tena imezidi kuwa kali. Ona walivyoanza kusuasua na hizo barua walizokuwa wanatamba nazo akina Nape. Wangekuwa na ubavu mbona wasizisambaze? Ni usanii mtupu. Na mabaradhuli tu ndio watakaotazamia mafisadi kushughulikiwa. Ni nani katika viongozi waliopo atathubutu? Ni nani kati yao aliye msafi?
ReplyDeleteCCM haina orodha ya mafisadi! wewe unasemaje wafilisiwe? Huna akili?
ReplyDeleteMimi nashauri suala hili la ufisadi tumeshachoka kulisikia. Nina hakika hawatafanywa kitu chochote kwani wao ndio CCM yenyewe. Bila wao CCM haina uhai. Ninasema hivi kwa sababu watu hawa ni wafadhali wakubwa wa CCM. Pia wana siri kubwa wanayoijua juu ya serikali iliyoko madarakani kwa hiyo Mkuu wetu hayuko tayari kuwaudhi hawa kwani watamuumbua. Kwa hiyo sisi walalahoi tunateseka mioyo yetu bure mafisadi CCM hawataisha kwani wanaotajwa ni mapacha watatu tu je hao wengine vipi? Watalindana kama walivyozoea. Mwenyekiti wa taifa CCM alitamka jukwaani kuwa amewapa siku 90 wajiondoe lakini nina hakika siku 90 zitaisha bila hatua yoyote kuchukuliwa dhidi yao. Sababu ni hizi kauli zinazopingana za kina Nape na Mukama kuanza kusema hawajapewa siku 90. Wameona maji yako shingoni watanzania wako makini sana zikiisha siku 90 sijui watapita barabara gani.
ReplyDelete