Na Gladness Mboma
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete ametakiwa kujivua gamba kwa kuivunja Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho kwa
madai kwamba wajumbe wengi ndani yake wanashirikiana na mafisadi.
Mbali na hilo sektretarieti mpya inayoongozwa na Bw. Wilson Mukama imetakiwa kuhakikisha kwamba wanawavua uanachama pamoja na ubunge wanachama wao wanne wanaotajwa kwa tuhuma mbalimbali ili chama hicho kiweze kuibuka kidedea mwaka 2015.
Hayo yalisemwa jana na Mwanaharakati Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na utawala bora na haki za binadamu, Bw. Renatus Mkinga wakati alipokuwa akizungumzia hali ya siasa nchini na mwelekeo wa CCM baada ya kuamua kujivua gamba.
Alisema kuwa gamba kubwa linalolitikisa CCM ni Bw. Edward Lowassa, Bw. Rostam Azizi, Nazir Karamagi na Bw. Andrew Chenge.
"Hawa watu ni hatari kwa nchi yetu kwani baada kufanya mbinu zote za kujivua hilo gamba na kushindikana wanachokifanya sasa ni mbinu chafu za kuwapaka viongozi wa chama hicho matope akiwemo Mwenyekiti Rais Kikwete na familia yake," alisema.
Kwa mujibu wa Bw. Mkinga, wanachama hao hujisafisha kwa kutumia viongozi mbalimbali wakiwemo wa dini, wasiasa na watu binafsi.
Alisema kuwa viongozi wapya CCM waliochaguliwa wote anawafahamu vizuri kwamba ni watu wazuri na kusisitiza kwamba kujivua gamba kwa viongozi wachache hakutoshi, bali Halmashauri Kuu nayo inatakiwa kuvunjwa haraka kwa sababu nako kumejaa mafisadi.
Alisema kuwa nchi hii watu hawaichukii serikali bali chuki yao ni pale viongozi wanapokuwa hawachui hatua.
Bw. Mkinga alisisitiza kwamba kuvuliwa gamba kwa baadhi ya mafisadi hao haitoshi na badala yake wawavue pia uanachama pamoja na ubunge kwa kuwa ikifanikiwa kufanya hivyo CCM haitapoteza chochote wala haitakuwa na athari yoyote.
"Ninasisitiza kwamba kama CCM inataka kuanguka mwaka 2015 iendelee kuwang'ang'ania hawa wanne wafukuzwe na kisha wafikishwe mahakamani," alisema.
Alisema CCM imegawanyika katika makundi matatu ambapo yeye yupo katika kundi la CCM-Asilia, lingine ni CCM-Mamboleo na la mwisho CCM-Chumia tumbo.
Bw. Mkinga alisema kuwa kamwe wanachama hao wanatakiwa kujiondoa wasidhani kama watapata urais kwa kumchafua rais, familia yake na viongozi wa nchi.
ww mkinga una uelewa finy sana kuhusu ccm yako. yaan hujui mpaka ssb kwamba ccm yenyewe n gamba. na kikwete n kiongoz wa gamba lenyewe
ReplyDeletehiyo ndiyo si hasa
ReplyDeleteKWAKO MKINGA,
ReplyDeleteBinafsi nakuheshimu sana lakini nakata tamaa unaposema m-kiti awavue gamba watu wengine wakati naye pia anazo kashfa chungu nzima kwani uwezi kuwa urafiki wa karibu na mafisadi halafu wewe mwenyewe ukawa safi haiwezekani.wahusika uliowataja wangeshakuwa mahakamani siku nyingi lakini ni M-KITI ndiye anayewalinda na akaenda mbali hadi kuwafanyia kampeni na kuwaita watu safi watu ambao serikali yake yeye mwenyewe imewafikisha mahakamani kwa kuwa wana ushahidi wa kutosha kuwa ni mafisadi.
mwenyekiti JAKAYA KIKWETE NDIYE INABIDI AWE WA KWANZA KUJIVUA GAMBA kabla ya kuwavua wengine.