Na Mohamed Hamad, Manyara
MKAZI wa Kijiji cha Njoro wilayani Kiteto mkoani Manyara, Bi. Mwajuma Selemani (70) amebakwa na watu wasiojilikana na kuchanwa chanwa sehemu za
siri na kitu chenye ncha kali.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kijiji cha Njoro, Bw. Selemani Farandi amesema tukio hilo lilitokea Mei 3, mwaka huu, wakati bibi huyo akitoka shambani kwake kwenda nyumbani hivyo kukutana na vijana wawili ambao waliamtaka bibi huyo kuwauzia alizeti.
“Hawa vijana walifika shambani na kumkuta mama akivuna alizeti walimtaka awauzie lakini mama lisema hauzi wakaondoka baada ya muda alirudi mmoja na kumtaka tena auze ndipo mama akapata wasiwasi na kulazimika kuanza safari kurudi njiani,” alisema Asha Iddi mtoto wa mama huyo.
Alisema akiwa njiani mama huyo alijitokeza kijana ambaye hakufahamika na kumpiga 'ngwara' akaanguka hatimaye kumchania nguo za ndani na kutimiza kumbaka na kumchana chana sehemu za siri na kiti kinachodaiwa kuwa cha ncha kali.
“Pamoja na mama kubakwa kwa mujibu wa Daktari aliyempima ametueleza kuwa aliingiziwa kitu kigumu sehemu za siri kilichomfanya apate maumivu makali amayo kwa sasa yanampa shida hata kujisaidia haja kubwa na ndogo inamwia vigumu,” alisema Bi. Asha.
Unyama wa namna hii haufanani hata kidogo na mienendo ya nchi yenye amani au dini. Nchi yetu haina amani, tunao utulivu tu. Ni wapi penye amani umekuta gari ikipata ajali vibaka wanawaibia majeruhi na hata maiti? Ni wapi ukimbaka mama kizee na kumchana sehemu za siri na ukikamatwa na kuhonga hela unaachiliwa na kikongwe cha watu kinateseka hadi kufa. Amani eh!
ReplyDeleteSHETANI YUKO KAZINI
ReplyDeleteKwa hatua tuliyofikia in bora ya mnyama,tunalaani kwa nguvu zote vitendo vya kinyama kama alivyofanyiwa bibi yetu huyu.Tunamumba mungu ampe afya mapema na waliofanya kitendo hicho mwenyezi mungu atajua namna ya kuwahukumu kwani ndiye hakimu wa mahakimu.Poleni sana ndg zangu na ugua pole bibi yetu kuwa na subra mungu atakujaaliya kheri inshaallah.
ReplyDeleteHawa vijana wakamatwe na wao wafanyiwe kama walivomfanyia huyo bibi asiye na kosa lolote lile. Wakamatwe na kushindiliwa vitu vigumu kama vile walivovitumia kumuangamizia huyo bibi wa watu. Haya yanaweza kutimizwa na wananchi. Mungu awaangamize kwa haki ya huyo bibi.
ReplyDeleteDu kweli dunia imekwisha ila mungu atamlipa kila mmoja kwa matendo yake,namuomba allah amjaalie bibi huyu afya na amponye mapema ila hawa vijana watalipwa stahiki yao.
ReplyDelete