*Maswali kibao yaibuka, picha ya maiti yaghushiwa
*Wengi wahoji kuzikwa haraka haraka, baharini
*Wataka picha zake zioneshwe hadharani, ili waamini
Na William Shao
Siku moja baada ya kutangazwa kuuawa kwa aliyekuwa kiongozi wa mtandao wa kigaidi duniani wa
al-Qaeda, Osama bin Laden, watu mbalimbali nchini na duniani wameonesha wasiwasi wao kuhusu kifo hicho wakidai kuwa huo ni mchezo wa kutaka kuipumbaza dunia, Majira limegundua.
Kwa mujibu wa maoni mbalimbali kutoka kwa wasomaji wa Majira na mtandao wa intaneti, inawezekana Osama alifariki miaka kadhaa iliyopita jambo lililofanya Marekani kuona aibu kwa kuendesha operesheni ya mabilioni ya dola bila mafanikio hivyo kuamua kufanya usanii huo ili kuihadaa dunia.
Tangu dunia ilipotangaziwa rasmi kifo cha kiongozi huyo wa al-Qaeda na Rais Barack Obama wa Marekani mlolongo mzima wa tukio hilo umeacha maswali mengi kuliko majibu huku baadhi ya wasomaji wa gazeti hili wakihoji kwanini picha za maiti ya Osama hazikuoneshwa na sababu za kuzikwa haraka kiasi hicho pamoja na kwamba alikuwa mtuhumiwa aliyesakwa kwa udi na uvumba na Wamarekani.
“Najua kuwa hizi ni sheria za Kiislamu, kama watu wengi wanavyosema, lakini hapa tunamzungumzia mtu aliyekuwa akitafutwa zaidi duniani kuliko mwingine yeyote,” alisema msomaji mmoja na kuhoji, “Walimtafuta kwa zaidi ya miaka kumi, hatimaye walipomuua, ndipo ghafla wakaona kuwa ni bora waheshimu sheria za Kiislamu?”
HATA HIVYO, WASOMAJI WENGINE WAMEINGIWA NA WASIWASI JINSI JAMBO LENYEWE LILIVYOTENDEKA. WANAHOJI IKIWA OSAMA BIN LADEN AMEUAWA KWANINI PICHA ZA MAITI YAKE HAZIJAONESHWA POPOTE KATIKA VYOMBO VYA HABARI?
HABARI ZINADAI KUWA VIPIMO VYA VINASABA (DNA) VILITHIBITISHA KUWA ALIYEUAWA NI OSAMA KWA SABABU VILIWIANA NA VINASABA KUTOKA KATIKA UBONGO WA DADA YAKE AMBAYE ALIKUFA KUTOKANA NA KANSA MJINI BOSTON, MAREKANI.
TELEVISHENI YA CNN ILIRIPOTI KUWA UBONGO WA DADA YAKE HUYO ULIHIFADHIWA NA WAMAREKANI KWA KUSUDI LA KUGUNDUA VINASABA VYA BIN LADEN KAMA SIKU MOJA ANGEPATIKANA HAI AU AMEKUFA.
Taarifa zilizoenea katika mitandao zinaeleza kuwa picha inayodaiwa kuwa maiti ya Osama inadaiwa kutengenezwa nchini Pakistan ili ionekane ni kweli Osama amekufa. Picha hiyo ilioneshwa pia katika televisheni ya Pakistan.
Hata hivyo, taarifa za awali zilidai kuwa Osama bin Laden alipigwa risasi kichwani, lakini taarifa nyingine zinasema alipigwa risasi jichoni na nyingine zinadai kuwa alipigwa risasi kisogoni.
Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) ya Januari 9, 2010, Osama bin Laden alikufa miaka minane iliyopita wakati wa vita iliyokuwa ikiendelea Tora Bora, Afghanistan. Mwandishi wa BBC, Mike Rudin, alisema huenda Osama aliuawa ama na mabomu ya Marekani au ugonjwa wa figo ambao tayari ulikuwa umemdhoofisha.
Kwa muda wa muongo mmoja, Osama bin Laden alifanikiwa kuyapiga chenga mataifa makubwa, hususan Marekani, waliokuwa wakimsaka kwa nguvu kubwa.
Picha kadhaa za video za Osama zimekuwa zikitolewa zinazomwonesha akitoa vitisho kuwa angeendelea kuishambulia Marekani na Wamarekani popote walipo. Video ya kwanza ya mfano huo ilitolewa na Wizara ya Ulinzi ya Marekani Desemba 2001.
Katika video hiyo, Osama alisema alishiriki tukio la kigaidi la Septemba 11, 2001 ingawa wengi wanadai kuwa Osama hajawahi kukiri kufanya tukio hilo.
Madai kwamba inawezekana Osama alifariki miaka mingi iliyopita yalitolewa pia na mwanasiasa wa Pakistan, Bi. Benazir Bhutto. Katika mahojiano na vyombo vya habari muda mfupi kabla yeye hajauawa, Bhuto alisema Osama alishakufa.
Pia, kituo cha televisheni cha Fox News Reported, Desemba 26, 2001, kilitangaza kuwa Osama bin Laden alikuwa amekufa. Lakini miaka 10 baadaye Rais Barrack Obama wa Marekani akatangaza kifo cha Osama bin Laden.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari mara baada ya taarifa ya kuuawa kwa bin Laden katika mashambulizi yaliyofanywa na askari wa Marekani, maofisa wa Serikali ya Pakistan walisema mwili wake ungezikwa kwa mujibu wa taratibu za Kiislamu.
Kwa mujibu wa taratibu za dini ya Kiislamu, mwili unatakiwa uzikwe ndani ya saa 24, walisema maofisa hao. Baada ya kuona ugumu wa kukubali kupokea mabaki ya gaidi aliyekuwa akitafutwa zaidi duniani, walisema maofisa hao, Marekani waliamua kuuzika mwili huo baharini.
Osama bin Laden alizaliwa Jumapili ya Machi 10, 1957, mjini Riyadh, Saudi Arabia. Inaaminika kuwa yeye ni mwanzilishi wa mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda ambao unaaminika kuwa ulihusika na mashambulizi ya Marekani ya Septemba 11, 2001 na yale ya Dar es Salaam na Nairobi mwaka 1998.
Alikuwa katika orodha ya watu kumi wanaotafutwa zaidi duniani na Shirika la Upelelezi la Marekani, FBI. Kuanzia 2001 hadi 2011, bin Laden na mtandao wake walikuwa ndio shabaha kubwa ya Vita Dhidi ya Ugaidi duniani.
Mei 1, 2011, Rais wa Marekani, Barack Obama, aliamuru mashambulizi dhidi ya eneo ambalo Marekani walihisi Osama alikuwa amejificha. Operesheni hiyo, kwa mujibu wa Rais Obama, ilifanikiwa kwa kusaidiwa na Shirika la Kijasusi la Marekani, CIA. Katika muda wa dakika 40, bin Laden akawa amepigwa risasi kichwani. Mwili wake ulichukuliwa na kupelekwa kusikojulikana hadi ilipotangazwa kuwa amezikwa baharini.
Remember the first casualty in many American operations is always TRUTH from from Vetnum war to Iraq war. It is not Uncommon to see discontention among people around the world
ReplyDeleteWaandishi wa habari wa kibongo nendeni shule hiyo elimu yenu ya VODAFASTER mnatia haibu. yaani ni upuuzi mtupu
ReplyDeleteWee anonymous, "haibu" ni nini tahira?
ReplyDeleteKwa kweli khidaa za Wamerekani kwa Ulimwengu wa leo zimebainika wazi wazi nani nivigumu sana kukhadai watu kwa wakati huu uliojaa vyombo vya habari mbalimbali vinatoa ukweli kwa watu wote Duniani. Hii ni njia ya kujitangaza au kujikosha uchafu walio jipaka Wamerekani katika Ulimwengu mzima. Njama yao inajulukana na nia yao kufuta Uislamu Duniani lakini hawataweza kamwe na mwishoe watajikuta wanajiuwa wenyewe kwa wenyewe.
ReplyDeleteWhy Tanzania people are so dump? You have a lot in your plate, for starting power ratio, poverty, no clean running water and poor infrastructure and bad government. If I remember correctly few months ago, there were blasts in Gongolamboto which killed few local residents again and nothing has been done to ensure that doesn’t happen again. Don't worry about what Americans do, worry about your problems in your country...which I mention few of them above.
ReplyDeleteHizo kauli za kidini sioni kama zina maana, na hakuna mwenye nia ya kufuta dini ya mtu, bali ni kama walivyo mafisadi na magaidi ni hivyo hivyo wasiwepo sasa wewe mwenye ufinyu wa akili rudi shuleni ukaelemishwe kwani hujui kinachoendelea duniani. wao hawakumuuwa mwislam bali wamemuua Gaidi.wewe utaacha lini kuchanganya watu na udini kila kona upo kwa ajili ya kuvuruga watu, jirekebishe.
ReplyDeleteBlalshit,are you crazy, any time u talk about islamic, ongelea ugaidi acha kuingia choo cha wanawake ingia cha wanaume wenzio na kama wamekuone wewe ni wakike fuata kina mama, ili wakufundishe jinsi ya kuchuchumaa chooni. acha kuongea pumba
ReplyDeletehapo ndio ninapo wapa sifa wabongo kila kitu kujua nchi yenu bado masikini inawashinda jueni yenu ya osama na marekani ya nn?hata kama obama muongo inawasaidia nn du hiyo nchi kiboko
ReplyDeleteNyie waandishi wa gazeti hili ndo mnaipumbaza Tanzania!
ReplyDeleteSijui mnafaidika nn na huyu NDULI Osama
kunatofauti kibwa kati ya uislam na muislam.kwaiyo hanayo yafanya m2 hinawezekana hakawa hanatete uislam au kwa maslai yake binafsi.kwahiyo ww asiyejua achakujifanya unajua.4 now kila mwislam wanamuita gaidi.je? kama nyie wange kua wanatukana dini zenu mgejisikiaje? so kufatilia kitu usicho kijua.Dunia ya leo uislam unatukanwa sana kwanini nisitete dini yangu kwa kuzalilishwa,nasema komeni matusi yenu na pia kashifa zenu dhidi ya uislam.
ReplyDeletenote:uislam na mwislam ni vituviwili pea vinaweza fika leta mitazamo fotauti kwa wasio elewa.
Hongera Marekani kwa kumuua Osama, ndugu zetu wengi wamepotezamaisha bila ya hatia. Na kama angeendelea kustawi ina maana mtandao ungezidisha mauaji. Ni kwa nini Muslims wanakuwa na roho za kinyama hawana ubinadamu! Utakuta hata tanzania kuna watu wanamuunga mkono bin laden, wa nini mtu kama huyo? acha afe na akina alshababu labda watapunguza mauaji wanayoyafanya katika Africa.
ReplyDeleteChunga ulimi wako wewe,waislamu wanaroho mbaya! Wewe unamjua mwenye roho mbaya? Christians[makafiri] ndio wana roho mbaya na ndio maana machafuko mengi duniani yanasababishwa na Christians especially Roman Catholics.Forexample Burundi & Rwanda
ReplyDeleteHIZI NINJAMA ZA MATAIFA YA MAGHARIBI, UFREEMASSON, NA MAADUI WA UISLAM KTK KUUPIGA VITA UISLAM. OSAMA HAKUHUSIKA NA 09/11. WALA KULIPUA UBALOZI WA KENYA NA TZ. ZILIKUWA NI PROPAGANDA TU KWAAJILI YA KUJIIMARISHA NA SABABU ZA KUUHUJUMU UISLAM. MAKAFIRI NI WATU WABAYA SANA.
ReplyDelete