*Wasomi wamshangaa kushtaki wateule wake
Na Edmund Mihale
HOTUBA ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa kwa watendaji wa serikali katika semina elekezi juzi mjini Dodoma imeibua mjadala mkali baada viongozi wa
kisiasa na wanaharakati mbalimbali kumtaka ajiuzuru kwa kuwa ameonesha udhaifu katika uongozi wake.
Katika hotuba hiyo Rais Kikwete alisema ipo kasoro kubwa ya watendaji wakuu serikali kwa kuwa kumekuwa na uhusino mbaya kati ya makatibu wakuu, mawaziri na wafanyakazi wa chini jambo ambalo ni hatari kwa serikali.
Rais Kikwete aliwataka viongozi wasiowajibika kujiondoa katika Baraza la Mawaziri na bungeni ili watakaobaki wajenge umoja.
Akizungumza na Majira kwa njia ya simu Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mt. Augustine, Prof. Mwesiga Baregu alisema hali ilipofikia sasa kwa Rais Kikwete kuwasuta watendaji wake hadharani kinaonesha ni jinsi gani Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ilivyo dhaifu katika kuwatumikia wananchi.
"Alikaa akawaona wanafaa na sasa anawashtaki kwetu, sisi tunalalamika kutoka na ugumu wa maisha na yeye analalamikia sasa tumsaidieje.
"Aliwateua pekee yake hakuna mwanachi yeyote aliyemsaidia kujua kuwa wanafaa, sasa ni miezi mitano imepita, ameanza kulalamika anawashtaki kwetu wakati kuna cabinet meeting (Baraza la Mawaziri) sijui wanakaa mara ngapi, lakini alitakiwa kuwambia huko bila ya sisi kujua kama anaona serikali imemuelemea anatakiwa kujiuzuru na kutuachia tuunde serikali itakayowajali wananchi," alisema.
Profesa baregu alisema Rais Kikwete alipaswa kuwashtaki mawaziri hao kwa wananchi kana alivyofanya juzi iwapo wangekuwa wamechuguliwa na wananchi au kuwateua na kuidhinishwa na bunge lililochaguliwa na wanachi kama ilivyo Marekani ambapo ambako mawaziri hudhinishwa na bunge.
Alisema kuwa kimsingi haoni mantiki ya Hotuba ya Rais Kikwete katika kuwatumikia wananchi, hivyo kama naona kuwa serikali imemuelemea anatakiwa kujiuzuru kuliko kuunda serikali inayotumia muda mwingi kualalamika kuliko kutatua matatizo ya wananchi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi Wanawake Tanzania (TAMWA). Bi. Ananileya Nkya alisema kuwa anashindwa kuelewa ni kwa nini rais aliamua kuzungumza udhaifu wa watendaji wake katika hadhara ya Watanzania.
"Ni kwa nini alalamike, wananchi walalamike, yeye naye alalamike sasa tukimbile wapi kama serikali nayo inalalamika? Kama anaona mtu hafanyi kazi awafukuze sisi tunataka wachapakazi nchi iendelee," alisema Bi Nkya.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi Bara (CUF), Bw. Mtatiro alisema Rais Kikwete alikuwa anajaribu kupoteza muda kwa kuwa serikali imeshindwa kufanya kazi ya kuwatumikia wananchi.
Alisema kukiri kwa Rais Kikwete kuwa kuna baadhi ya watendaji ni mzigo ni ishara kuwa serikali yake ni dhaifu mbele ya wananchi na mabadiliko iko hayawezi kutokea hata kama akizungumza vipi.
"Serikali imeshindwa kuchukua hatua kwa watendaji wake, utasikia huyo ni mzigo, leo unamtoa katika wizara hii kesho unampeleka katika wizara ile akiharibu, sasa mabadiliko ya kifanisi yatapatikana wapi hapo," alisema Bw. Mtatiro.
Alisema Rais Kikwete ni dhaifu pamoja na serikali yake na kwamba mabadiliko hayaji kwa kuzungumza katika semina elekezi bali kutokana na utendaji.
"Sasa wamachinga wanalalamika, wafanyabishara nao wanalalamika, wananchi pia wanalalamika, serikali nayo inalalamikia. Bora wananchi wanahangaika na kujikwamua kiuchumi kwa kutafuta mitaji huku na kule baada ya kuona serikali yao imeelemewa, sijui tufanyeje ili kuisaidia," alisema Bw. Mtatiro.
Alisema sasa tunahitaji rais atakayekwenda kufanya kazi kuwasaidia wananchi ili wajikwamue na hali ya ugumu wa maisha lakini sasa tuna serikali iliyoshindwa kufanya kazi imekaa madarakani kwa sababu ya kulalamika kuhusu utendaji wake.
AMMA KWELI KILA MTU ANA UHURU WA KUSEMA ALITAKALO KWA KUDAI NI DEMOKRASIA!!HAKIKA ALICHOSEMA RAISI KTK HII SEMINA NI KUWAKUMBUSHA NA KUWAHIMIZA WAJIBU WAO WATENDAJI NA MAJUKUMU YAO,WAWAJIBIKE SIO KUKAA MAOFISINI KUSUBIRI RIPOTI KAMA ZIMAMOTO NI SEMINA KAMA ILIYOFANYIKA NGURUDOTO 2006,RAIS KAHIMIZA KASI ZAIDI KUONGOZA SIO LELEMAMA KAMA MNAVYOKAA MKAANZA KUBWABWAJA UPROFESA AU UKURUGENZI SIO SABABU YA KUJIONA UNAJUWA KILA KITU AU NI UHODARI KULIKO WENGINE KUKUMBUSHANA NA KUHIMIZANA NI WAJIBU YEYE KAMA KIONGOZI MKUU AMEWAAMBIA MAPEMA WAWAJIBIKE ILI WASIJE KUWAJIBISHWA WAKAANZA KULALAMIKA. NI WAJIBU WENU KUMKOSOA LAKINI PAWE PAKUKOSOLEWA SIO KUWA KINYUME NA KILA KITU SIO SAHIHI.TUKO KATIKA JAHAZI MOJA TUWE NA UMOJA TUACHE CHUKI BINAFSI!!
ReplyDeletetatizo la JK hakuwa na visions wakati anataka urais wa Tanzania.Hakuwa na malengo ya kwamba ataifanyia nini Tanzania na wananchi wake.Madhara yake tunaona sasa anazidi kuwalalamikia watendaji wake aliowateua mwenyewe.kama mtu hatendi unavyotaka fukuza na weka mwingine mchapa kazi.Kwa kulalamika hivi maisha bora kwa kila mtanzania utayasikia tu mjomba hadi mwisho wa ufalme wako na huku watanzania ukiwaacha maskini wakutupwa.pole sana rais wangu kiti hicho ulikitaka kwa sifa tu na huwa kuwa nania njema na wananchi wenzako.pole tena
ReplyDeleteNI KAZI MBAYA YA KIONGOZI WETU,WANATUMIA PESA OVYO ZA SERIKAALI KAMA HIYO SEMINA INAMAANA GANI KUWAKUMBUSHA .
ReplyDeleteOFISINI KILA MTU ASIYEFANYA KAZI VIZURI ANAYELELEGA UWA ANAPEWA BARUA KUMBE TZ TUNAPEANA UONGOZI KWA USHOGA NDIO MAANA RAIS ANAITISHA KIKAO CHA VIONGOZI.
SIRI ILIYOJIFICHA UKIONA WATU WANAGOMBANA OFISINI UJUE NDANI YAKE KUNA UFISADI AU MATUMIZI NABAYA YA FEDHA SASA KUNA UGOMVI WA KUGAWANA TUWE WAJUWAJI WA SIRI NA UNAYECHANGIA MAONI UWE UNAJUA UTENDAJI WA SERIKALI SIO KUSEMA NGURUPAPA AU DOTO HIYO NI HISTORIA TU
Hivi kiongozi hakiteua mtu katika nafasi fulani ya uongozi, mfano uwaziri au ukuu wa mkoa, na huyo mteuliwa hawajibiki, ni hatua gani anapaswa kuzikuchukua yule aliyemtueua? Je kwa nafasi hii ya Rais Kikwete, anapaswa kuchukua hatua gani dhidi ya aliowateua lakini hawawajibiki? Kulalamika, kuwachekea na kuwapigia makofi? Je na sisi wananchi ambao tunaona kuwa rais hawajibiki, tutamshtaki wapi?
ReplyDeleteHotuba ya Mhe. Rais, ikiwa ni pamoja na ili ya Ngurudoto ya 2006, haina agenda yoyote ya kiutendaji.
ReplyDeleteUkilinganisha hotoba yake ya sasa na ili ya 2006 utagundua hotuba ya sasa si ya kuwaelekeza, bali kuwakalipia watendaji mbele ya macho ya wananchi.
Hotuba ya sasa imekuwa na sura ya kukalipia watendaji kufuatana na matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2010 yaliyoonesha kushuka kwa uaminifu wa wananchi kwa serikali ya Chama Cha Mapinduzi.
Hivyo, kwa hotuba hii Mhe. Rais hatafuti kitu kingine zaidi ya Kukubalika. Neno zuri wataalamu wa Sayansi ya Siasa na Utawala wanalotumia hapa ni "LEGITIMACY"
Serikali ya chama tawala sasa imepoteza "LEGITIMACY" kufuatana na uchaguzi wa 2011. Hivyo, kiongozi Mkuu anafurukuta kwa kuwakalipia watendaji wake hadharani ili wananchi warudishe imani na ukubali kwake.
Kitakachofuata hapo nawaambieni msishangae baadhi ya viongozi wakipigwa chini hapo baadae kwa lengo hilohilo la kutafuta "LEGITIMACY"
Lakini JK si amemwambia Dr. Magufuli aache ubabe? Sasa anategemea mawaziri wengine wafanye kazi? Wakikashfiwa kama Dr. Magufuli? Yeye mwenyewe JK ndiye kisababishi kikuu cha kuzorota kazi. Watu wanajua fika kuwa wakifanya kazi kwa juhudi sana, wataambiwa wapunguze kasi; wakifanya kazi kwa kufuata sheria wataambiwa waache ubabe. JK imekula kwako!
ReplyDelete...Nakumbuka kuna hotuba moja mwl. Nyerere alisema tatizo la viongozi ni wale wanautaka urais...hawako wazi wanautafuta uraisi kichinichini.Mwl aliuliza kama wapo waje tuawaulize wewe unataka kuwa rais wetu lakini unajua tuna nyufa hizi.....
ReplyDeleteTatizo letu Watanzania kwa sasa ni kujengeka,kila asemalo au atendalo Rais wetu,kuwa halina maana au halifai.Tumekaa kungoja kutoa maoni ya lawama na kebei tu.TUTAFIKA WAPI?Mi nadhani watu wanataka Rais wa matendo si kila siku watu kukumbushwa kila jambo,wkt wao walikula kiapo cha utii kwa TANZANIA NA WATANZANIA.Ila washauri si wema sana kwake na kwetu,hizo hela zote zilizotumika hapo Dodoma c zingeongeza hata wodi ya wagonjwwa Temeke hospital.
ReplyDeleteSASA MSEKWA NA MSUYA NAO WATENDAJI? NILIDHANI RAIS ANGEENDA KUCHUKUA MAPROFESA UDSM KUWAFUNDA WATENDAJI MAANA MAZINGIRA YA KINA MSEKWA NA MSUYA SASA NI WAZI NI TOFAUTI NA KUWATUMIA WAO NI COUNTER-PRODUCTIVE TU. RAIS KIKWETE ANALALAMA MNO SIJUI ANATAKA ASIDIWEJE.TATIZO NI RAIS MWENYEWE KWA MAANA NYINGI NA PANA HASAA.UFISADI UMEMALIZA NCHI.
ReplyDeleteKWANZA, HAIKUWA BUSARA KUWASEMA MAWAZIRI HADHARANI WAKATI ANGEWEZA KUZUNGUMZA NAO KTK BARAZA LA MAWAZIRI. PILI, SEMINA HIZI ELEKEZI HAZINA TIJA YEYOTE KWANI HATUJAONA UFANISI AU TOFAUTI YEYOTE TOKA WALE WA KWANZA KULE NGURUDOTO. TATU, RAIS MWENYEWE ALISEMA AMEJITAYARISHA KUWA RAIS KWA MUDA WA MIAKA KUMI, LAKINI UTENDAJI WAKE UNAONYESHA KAMA VILE HAKUWA NA MATAYARISHO YEYOTE YA KIUTENDAJI BALI KUSHINDA UCHAGUZI NA KUANZA KULA NCHI SIO KUJENGA NCHI.SERIKALI HII NI YA MATANUZI TUU HAKUNA UZALISHAJI AU MAENDELEO. SERIKALI IMETUMIA FEDHA ALICHUMA MKAPA NA SASA ZIMEKWISHA, WANANCHI TULIE TU!
ReplyDeleteNdugu zangu, wastaafu tangu wa mwaka 2010 Juni wengi wao hawajalipwa mafao yao. Wako wanaokwenda PSPF kila uchao kuulizia wanapigwa danadana nyingi. Mwishowe wakang'atwa siko kuwa hakuna pesa. Nyingi ya pesa zao zilitumika kujengea UDOM na hosteli za Mabibo. Kazi ipo!!!!
ReplyDeleteprofesa ataitwa bereguuuuuuuuuuuuuuuuuuu?hana lolote huyo tumemzoea atamkumbuka huyo kikwete muda si mrefu muache tu achonge tumeona maprof wangapi tangu enzi ya nyerere wamepewa wizara tu zimewashinda?kuongoza nchi sio kuongoza chuo au kanisa na msikiti walijue hilo kuna watu wenyebusara na vichaa utawaridhisha wote?
ReplyDeletemkiambiwa seikali imefilisika mnasema oooh..sasa hali ni mbaya mazee.kama watumishi hawalipwi posho zao ...malimbikizo ya mishahara ...hayalipwi ...ni taabu wao wanaangaia wabunge tu ...hata hao wabunge hawatufai kwasababu hawawatetei wananchi..wanaangalia mambo yao tu...huduma mbovu hospitali ,maji aahh tabu tupu . Hii nchi wamuazime Kagame tu alafu waone mabadiliko .hapo hamna mwenye uchungu na nchi ..JK anawajua wadhaifu inatakiwa awatoe siyo awaambie wajiuzulu nani atajiuzuru kwa hiari hapa ..hata ningekuwa mimi aaaah wapi !!
ReplyDeleteKWANI MZAZI KUWAONYA WANAYE NI VIBAYA? HALAFU SI KILA LA PROFESSOR NI SAHIHI,YEYE NI BINADAMU ANA MTAZAMO TOFAUTI KAMA BINADAMU WENGINE.HALAFU KUWA PROFESSOR SIO KWAMBA NI MSTAAAARABU! KUFAA KUIGWA.KWANI KUNA MAPROFESSOR WENGINE WALEEEVI MPAKA KUJIHARIBIA SURUALINI...
ReplyDeleteMHARIRI NA MWANDISHI WA MAKALA HII WANAONYESHA USHABIKI WA WAZIWAZI KITENDO AMBACHO SI KIZURI KWA PROFESSION YAO.
ReplyDeleteWasomi ni mahodari sana wa kukosoa lakini wenyewe ukiwauliza juu ya usomi wenu hata sindano ya kushonea nchini hawawaji kutengeneza wenyewe hadi itoke india,wao ni baraka ya kujiunga na vyama vya upinzani na kuanza blabla za kisiasa,tuambieni ulaya profesa gani ni mwenyekiti au meneja wa chama cha siasa?
ReplyDeleteAcheni watu waseme , kwani uongo? kwani kuwang'ang'ania hao hao wakati wapo wasomi wapya si angewabadilisha ? ngurudoto hao hao, na ndani ya kipindi kifupi baadae kidogo akabadilisha. Ndio tunawajengea mawazo kuwa wamekwenda kuchukua posho, kodi zetu.Mimi ninavyojua unapoajiriwa kuna kitu kinaitwa JOB DESCRIPTION, kazi na wajibu wako vinaonyeshwa humo, nadhani siku walipoapa walipewa na kama kunahitajika semina kidogo kama kuna mabadikliko ya kazi, halafu jambo lingine MH Rais hivi karibuni alifanya ziara za kushtukiiza kwenye baadhiya wizara, na yeye anazijua wizara anazoziita mzigo angemaliza huko huko kwenye ziara, au angewaita ikulu mawaziri na makatibu wa wizara husika akafanya nao kikao cha kuwakumbusha, au kuwakaripia n.k. angeweza kuokoa hizi gharama zinazotumika bila ya sababu ya dharura.Wtz ndio maana watu wanasema sirikali hii ni ya mapochozi, Mkapa alipoondoka aliacha mipesa kedekede ambayo ingetupeleka kutumia kwa muda wa miezi minane,huku serikali ikiendelea kukusanya, baba akaanza safari za ughaibuni kedekede, na matanuzi mengine, zikaisha fyuuu, sasa tutegemee nini? hapo tumekatia tuffunge mikanda hadi 2015, hamna jinsi.
ReplyDelete