08 April 2011

Yanga yaipiga kumbo Simba kileleni

*Bingwa kupatikana Jumapili
*Majimaji, Toto zashikilia ubingwa


Na Zahoro Mlanzi

TIMU ya Yanga jana imewapiga kumbo kileleni mabingwa wa Tanzania Bara, Simba baada ya kuifunga African Lyon Mabao 3-1 katika
mechi ya Ligi Kuu iliyopigwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na hivyo kuifanya kuongoza kwa tifauti bao moja.

Kwa matokeo hayo Yanga sasa inaongoza ikiwa na pointi 46, sawa na Simba isipokuwa vinara hao wamefungwa mabao saba na kufunga 26  wakati wapinzani wao wamefunga mabao 36 na kufungwa 15 hivyo kuifanya Yanga kuongoza kwa tofauti ya bao moja.

Katika mechi ya jana Yanga iliingia kwa uchu wa kufunga mabao ambapo katika dakika 11, Fred Mbuna aliunganisha kwa kichwa krosi iliyopigwa na Davies Mwape ambayo kipa Ivo Mapunda wa African Lyon aliipangua lakini hata hivyo mpira huo ulitoka nje ya lango.

Yanga ilirudi tena langoni mwa African Lyon ambapo dakika ya 18, Mwape aliachia kombroa kali akiwa nje ya 18 ambalo hata hivyo kipa Mapunda alilipangua na kupata maumivu yaliyomsababishia maumivu na mpira kusimama kwa dakika kadhaa.

Juhudi za Yanga kusaka bao lilizaa matunda dakika ya 32 baada ya Idd Mbaga kufunga baada ya kupokea pasi ya Mwape na kuwazidi ujanja mabeki wa Lyon na kuutumbikiza mpira wavuni.

Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kuingia kwa nguvu na kufanikiwa kupata baoa la pili dakika ya 46 kupitia kwa Mwape ambaye alipiga shuti kali lililomshinda kipa Mapunda ambaye alijaribu kupangua lakini kutokana na kasi ya mpira ya alijikuta akiusindikiza wavuniu.

Dakika ya 61 Yanga ilifunga bao la tatu kupitia kwa Mbaga tena ambaye baada ya kupokea pasi ya Nurdin Bakari alikimbia na mpira na kukutana kipa Mapunda ambaye alimhadaa na kufunga bao kirahisi.

African Lyon ilipata bao lake la kufutia machozi dakika ya 78 baada ya beki Chacha Marwa, kujifunga wakati akiwa katika harakati za kuokoa mpira baada ya Benedicto Ngassa kuachia shuti kali lililokuwa likienda wavuni.

Dakika ya 88, Mbaga alipata dhoruba kali na kuzimia na kutolewa uwanjani kwa machela, baada ya kugongana na Zuberi Makame ambao walikuwa wakiwania mpira wa juu na nafasi yake kuchukuliwa na Razakh Khalfan.

2 comments:

  1. Yanga kuukaribia ubingwa itakuwa ni fundisho kubwa kwa wachezaji wa Simba kwani naona baada ya kutolewa na TP Mazembe wao walijiona kama ni bora sana kwa kucheza kwa bidii na walipoingia uwanjani kucheza na JKT Ruvu waliingia kwa zarau ya kwamba hawa JKT si kitu tuwafunga tu,Na JKT waliingia uwanjani kwa ari na nguvu ili waitoe nishai timu kubwa.Hili ni tatizo kubwa tu kwa simba
    na wachezaji wetu wa kitanzania.Wanaposifiwa basi vichwa huwa vikubwa na kujisahau kwa sifa na matokeo yake wapoingia uwanjani wanashindwa kufanya walichotakiwa kufanya.

    ReplyDelete
  2. Jamani mi ni shabiki wa Simba na 1 huu ubingwa Simba wamechezea shlingi chooni, sasa kinachotakiwa Kesho wamchape Majimaji magoli mengi ili tuweze kuchukua ubingwa huu, endepo tutashindwa huu uzembe utakuwa umefanywa na wachezaji na wala kocha hana kosa lolote.

    Tulijiamini sna ile mecchi ya Jkt Ruvu wachezaji walikuwa na uhakika wakushinda hivyo waliingia kwa dhalau uwanjani.

    Kwa hyo yanga ikichukua ubingwa Wachezaji wetu ndio wakulaumiwa na wala sio kocha, kwani Phiri yuko Makini sna.

    Nawaombea wachezaji wa simba kesho mcheze mpira mzuri tuweze kuibuka na magoli mengi tuendelee kushikilia ubingwa wa Tz Mungu yupo nasi nina imani ubingwa upo MSIMBAZI Mngu ibariki Simba,na wachezaji wake.

    ReplyDelete