08 April 2011

Miss Tabata 2011 waanza mazoezi Da West Park

Na Mwandishi Wetu

WASHIRIKI 23 kutoka sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam, wamejitokeza kushiriki katika mashindano ya kumtafuta 'Malkia wa Tabata, 'Miss Tabata 2011', ambalo
limepangwa kufanyika mwezi ujao.

Mratibu wa mashindano hayo, Joseph Kapinga alisema kuwa warembo hao walianza mazoezi tangu Jumapili kwenye Ukumbi wa Da West Park Tabata, Dar es Salaam.

“Warembo wetu tayari wameshaanza kufanya mazoezi pale pale Da’ West Park kila siku kuanzia saa nane mchana hadi saa moja jioni," alisema mratibu huyo.

Aliongeza kuwa bado Kamati ya Mashindano hayo inawaomba warembo wenye sifa kujitokeza kwa wingi, ili hatimaye waweze kupata wawakilishi bora katika mashindano ya Kanda ya Ilala.

"Bado milango iko wazi, mrembo yeyote anayejiamini kwamba ana vigezo anakaribishwa. Tunataka mashindano ya mwaka huu yawe na ushindani zaidi,” Kapinga alisema.

Kapinga alisema kuwa Kampuni yake ya Bob Entertainment, ambayo ndiyo inaandaa mashindano hayo imepanga kuandaa sherehe maalumu ya kuwatambulisha washiriki wote kabla ya kupanda ulingoni kuwania taji hilo.

Aliwataja warembo ambao tayari wameshajitokeza kuwa ni Marion Augustino (18), Neema Marwa (18), Esther Simon (18), Sweetylily Suleiman (21), Malaika Abdallah (18) na Theckler Benedict (19).

Wengine ni Happiness Emmanuel (18), Irene Jafari (19), Janeth Marandu (21), Shadya Ally (21), Victoria Amon (20) na Mgayo Salehe (21).

Pia wamo Sarah Hangaya (20), Neema Stanford (21), Upole Athumani (19), Asia Amiri (22), Lucy Paulo (21), Johanita Kanyika (22), Mariamu Lameck (19), Blandina Paul (18),
Catherine George (19), Lilian  Brayson (24) na Lucia Joseph (20).

No comments:

Post a Comment