Na Florah Temba, Moshi
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Kilimanjaro inamshikilia Askari wa Idara ya Uhamiaji katika kituo kidogo cha Holili kwa
tuhuma za kupokea rushwa ya sh. 100,000.
Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari, Mkuu wa TAKUKURU mkoani Kilimanjaro, Bw. Lawrence Swema alisema mtumishi huyo alikamatwa Aprili 6, mwaka huu baada ya kupata taarifa kutoka kwa mwananchi mmoja ambaye alikamatwa kwa kudaiwa kuwa si raia wa Tanzania.
Bw. Swema alimtaja mtumishi huyo kuwa ni Koplo Kizito Kashinje Masaka ambapo aliyekamatwa katika mgahawa wa Fresh Coach mjini Moshi ambapo alifika kwa lengo la kupokea fedha hizo ili kumuachia huru raia ambaye alikuwa amekamatwa kwa kudaiwa kuwa si raia wa Tanzania.
Bw. Swema alisema Aprili 5, mwaka huu mwananchi huyo akiwa Himo lilifika kundi la askari 12 wa idara ya uhamiaji kati yao 10 wakiwa wanafunzi walioko mazoezini, walimkamata mwananchi huyo wakitaka kujua uraia wake kutokana na kutojua lugha ya Kiswahili vizuri.
Alisema baada ya kumkamata raia huyo alitoa vitambulisho vyake vitatu vinavyoashiria kuwa ni Raia wa Tanzania kikiwemo kitambulisho cha kupigia kura, kitambulisho cha mkazi na shahada ya muda ya kusafiria lakini askari hao hawakumuamini na walimtaka waende kituo cha polisi.
Alisema wakati wakielekea kituo cha polisi cha Himo walimuambia kuwa wakifika huko kituoni mambo yatakuwa marefu zaidi, hivyo atoe kiasi kidogo cha fedha ili wamuachie.
Aliendelea kuwa baada ya raia huyo kuambiwa hivyo alikuwa hana fedha kamili ambayo askari hao waliihitaji. Alikuwa na sh. 242,000 na kuwapatia sh. 240,000 na kubakiwa na sh, 2,000 ambapo 500 alinunulia maji na sh 1,500 walimuambia atumie kama nauli ya kumfikisha benki mjini Moshi kuchukua fedha nyingine za kuwaongezea.
“Baada ya kukubaliana hivyo na askari hao aliwasiliana na ndugu zake walioko jijini Dar es Salaam ili kuangalia uwezekano wa kumsaidia ambapo ndugu zake hao walimshauri kufika ofisi za TAKUKURU kutoa taarifa ili apate msaada,” alieleza.
alipofika TAKUKURU walimpa fedha za mtego na kufanikiwa kumkamata askari huyo baada ya kuwasiliana naye kwa namba 0757012510 ambazo walimpatia na kumueleza kuwa tayari ameshafika mjini na kwamba yupo eneo la Fresh Coach.
Alisema baada ya raia huyo kufika eneo hilo alimkuta na kumkabidhi sh.100,000 na papo hapo kukamatwa na maofisa wa TAKUKURU, na kumfanyia upekuzi ambapo walikuta fedha hizo zikiwa zimefichwa kwenye soksi ya mguu wa kushoto.
Alisema kuwa walimfikisha katika Ofisi za TAKUKURU ambapo baada ya muda aliomba kwenda kujisaidia, na aliporuhusiwa, aliingia chooni na kutupa swichi ya gari kwenye tanki la maji ili nyaraka ambazo walimnyang’anya raia huyo ambazo zilikuwa kwenye gari yake T 559 BEM Carina zisipatikane.
Hata hivyo, maofisa wa TAKUKURU walishtukia jambo hilo na kwenda kufanya upekuzi chooni na kukuta ufunguo huo, alipoulizwa alikiri kuwa ni wake.
Walipofungua gari hilo walikuta nyaraka zote ambazo walimnyang’anya raia huyo ambazo ni Shahada ya Dharura ya kusafiria yenye namba AB 09046529 iliyoonyesha kutolewa Februari 25, mwaka huu huko Ngara, kitambulisho cha mpiga kura cha Tanzania pamoja na Kitambulisho cha mkazi ambavyo vyote vina jina la raia huyo.
Mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayomkabili wakati wowote mara baada ya uchunguzi kukamilika.
WAMEZOEA KUNYANYASA WATU HAO WACHA WAKOMESHWE
ReplyDeleteETI MTU SAA ZINGINE KAA HIVYO UNAVIELELEZO VYOTE BADO ANAKUULIZA UNAENDA WAPI NA HAPO UKO TZ,
NAKUJA NYUMBANI KWAKO.