*Asema wanaovamia hifadhi ya barabara hawamtakii mema
*Amtaka asiwasikilize kwani wanavunja sheria aliyosaini
Na John Daniel
WAZIRI wa Ujenzi, Dkt. John Magufuli kwa mara nyingine amemweleza Rais Jakaya Kikwete, kuwa wizara yake itaendelea kutekeleza wajibu wa
kusimamia sheria za nchi na kumwomba kutosikiliza wanaolalamika kuondolewa katika hifadhi ya barabara kupisha ujenzi kwa kuwa wanamsaliti na hawamtakii mema.
Amesema watu hao wanamsaliti Rais Kikwete kwa kuvunja sheria namba 13 ya barabara ya mwaka 2007 aliyosaini na kulenga kumkwamisha kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akimkaribisha Rais Kikwete kuzindua upanuzi wa Barabara ya New Bagamoyo Dar es Salaam jana, Dkt. Magufuli alisema watu hao wanaolalamika ni maadui wa maendeleo kwa kuwa wanarudisha nyuma kasi ya kutengeneza barabara za lami.
"Mheshimiwa Rais nataka kukuthibitishia kuwa sisi Wizara ya ujenzi hatutakuangusha, namshukuru sana Mkuu wa Mkoa ameshanisaidia kuwataka wafanyabiashara waliopo pale barabarani Tegeta waondoke.
"Waanze kuondoka leo (jana), wasisubiri tuwaondoe, mkandarasi yupo tukichelewa ataanza kutoza riba, magreda wameyaona, naomba tu watakaokuja kukulalamikia usiwasikilize.
"Mhe. Rais sisi tutasikiliza maelekezo yako na wananchi nao wasikilize maelekezo yako na sheria namba 13 ya mwaka 2007 uliyosaini maana wanavunja Sheria ya Hifadhi ya Barabara, mkandarasi yupo 'site' na matrekta wameyaona.
"Wananchi wa Dar es Salaam wanataka barabara, inawezekana watu wanakufa njiani kabla ya kufikishwa Muhimbili kwa sababu ya msongamano," alisema.
Kauli hiyo ya Waziri Magufuli ilikuja baada ya ile ya Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Meck Sadiki kumweleza Rais Kikwete kuwa baadhi ya wananchi wameanza kutumia vibaya kauli yake kuwa wasubiri miaka mitatu ndio wapishe hifadhi ya barabara.
Alisema wafanyabiashara waliopo katika eneo la Tegeta walijengewa soko na Manispaa ya Kinondoni miaka mingi iliyopita lakini wameliacha na kuvamia hifadhi ya barabara, hivyo akamwagiza Mkuu wa Wilaya hiyo, Bw. Jordan Rugimbana kuwaondoa, huku akimhakikishia Rais Kikwete kuwa suala hilo liko ndani ya uwezo wao, hivyo hawahitaji msaada wake.
Kuhusu wafanyabiashara hao, Waziri Magufuli alisema wananchi hao walitengewa eneo kwa gharama kubwa alipokuwa Waziri wa Miundombinu lakini wameacha na kukimbilia kwenye hifadhi ya barabara.
Machi 21, mwaka huu akiwa katika mfululizo wa ziara zake katika wizara mbalimbali, Rais Kikwete alipotembelea Wizara ya Ujenzi alimtaka Waziri Magufuli kuacha ubabe wa kubolea watu nyumba zao bila kutoa muda wa kutosha, huku akihoji watendaji wa wizara walikuwa wapi wakati nyumba hizo zikijengwa hadi kukamilika.
Rais Kikwete alitoa kauli hiyo ikiwa ni siku chache baada ya Waziri Mkuu, Bw. Mizengo Pinda akiwa katika Jimbo la Uchaguzi la Chato anakotoka Dkt. Magufuli, kusitisha bomoabomoa katika hifadhi ya barabara iliyokuwa imetangazwa na waziri huyo nchi nzima kwa lengo la kuharakisha ujenzi wa barabara za lami.
Bw. Pinda alisema hatua hiyo ilikuwa imetokana na malalamiko mengi yaliyotoka kwa wananchi ambao wangeguswa na operesheni hiyo.
Mbali na barabara hiyo ya njia mbili yenye urefu wa kilometa 12.9 kutoka Mwenge hadi Tegeta, Waziri Magufuli alisema jumla ya kilomita 11,105 za lami zenye thamani ya sh. tilioni 3.7 inatarajiwa kujengwa katika kipindi cha miaka mitano ijayo na kwamba kila kona ya Tanzania kuna mradi wa ujenzi wa barabara ya lami.
"Mhe. Rais tunakushukuru sana tukuongezea fedha za barabara, hatutasubiri ufe kwamba ndio tuseme pengo lako halitazibika tunasema sasa, sisi tutatekeleza miradi yote, na Daraja la Kigamboni linajengwa," alisema.
Alisema mradi wa ujenzi wa barabara za mabasi yaendayo kasi sasa umeanza, pia barabara za juu (flyovers) nazo ziko mbioni kuanza.
Akizindua mradi huo unaogharimu sh. bilioni 88 unaotekelezwa na Kampuni ya Konoike, Rais Kikwete alisema lengo lake ni kuweka historia ya kutengeneza barabara zenye urefu mkubwa zaidi kuliko awamu zote za utawala kwa maslahi ya taifa.
"Miundombinu ndio injini ya maendeleo, barabara na maendeleo ni sawa na mshipa wa damu kwenye mwili wa binadamu, utengenenezaji wa barabara za lami ni sehemu ya maamuzi ya CCM kuboresha maisha ya wananchi.
"Nataka kuweka historia ya kujenga barabara zenye urefu mkubwa kuliko wakati wowote," alisema Rais Kikwete.
Alionesha kukerwa na tabia ya wahandisi na watendaji wa serikali wanaoshirikiana na baadhi ya makandarasi wasiokuwa waaminifu kujenga barabara chini ya kiwango kwa manufaa yao binafsi.
"Mwandisi msimamizi anasimamia barabara lakini inajengwa chini ya kiwango na anapitisha kuwa huyu alipwe, kisha TANROADS na wizara pia mnalipa.
Waziri hili nalo liishe, mnayo haki kukataa kupokea barabara, huyu mwandisi bado anapewa kazi nyingine kusimamia, na huyu mkandarasi naye bado anapewa kazi nyingine hivi inakuwaje?" alihoji Rais Kikwete.
Alisema kutokana na hali hiyo amemwagiza Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kukagua miradi husika badala ya kuishia kwenye makaratasi.
Alimwagiza pia Dkt. Magufuli kusafisha eneo lote la hifadhi ya barabara iliyosalia, Mwenge-Moroco, yenye urefu wa kilomita 4.3 kwa kuwa wafadhili wameshaafiki kuijenga. Gharama za kusafisha eneo hilo zilitajwa kuwa ni sh bilioni 10.7.
Alisema upanuzi wa barabara hiyo ni faraja kubwa kwake kwa kuwa alianza kuishughulikia kwa muda mrefu sana na kuwataka wanaobeza ziara zake nje ya nchi kutambua kuwa hilo ni moja ya matunda ya kazi hiyo.
Pia Rais Kikwete aliomba umati watu waliofika katika hafla hiyo kusimama dakika moja kama ishara ya kuwakumbuka waliopoteza maisha katika tukio la tetemeko na Tsunami ambapo zaidi ya watu 10,000 waliripotiwa kufa.
Barabara hiyo iliyozinduliwa na Rais Kikwete jana ina urefu wa kilomita 12.9 chini ya udhamini na serikali ya Japan na inatarajia kukamilika kabla ya Mei mwaka 2013.
Kwa upande wake Balozi wa Japan nchini, Bw. Hiroshi Nakagawa, alimuhakikishia Rais Kikwete kuwa licha ya nchi hiyo kupata janga la tetemeko na Tsunami watatekeleza miradi yote waliyoahidi kwa Tanzania na nchi nyingine za Afrika.
kzikwete huna ubavu kwa magufuli. subr mkufa na ccm yako.chadema zhoyeeeeeeeeeeee
ReplyDeleteHUYU MCHANGIAGI WA KWANZA NI MCHONGANISHI ILA MIMI NASEMA RAIS MUUNGE MKONO WAZIRI MAGUFULI TUSAFIRI KWA BAJAJI SISI WA KIPATO CHA CHINI.
ReplyDeleteMuwaambie hao wanaoendesha bajaji kwanza wajifunze sheria za barabarani na wakachukue leseni halali. Hao wanaendesha ovyo sana kwa vile hawafuati sheria. Na ukimuelimisha anakuwa mkali.
ReplyDeleteNa kwa vile wengi wenu nyinyi aliyewabeba hamujui sheria munaendelea kuwatetea.
Kwanza nasikitika sana kuona baadhi ya watu kusema maneno bila kufikiri kama huyu jamaa hapo juu hana la kusema ila chuki tu mambo kama haya yanazifanya nchi zingine kuingia katika vita visivyo maana hapo zamani tulipokua tukitawaliwa na wakoloni tulikua tukisema kua wakoloni ni wabaya na wana chuki na watu weusi lakini ukitazama sasa hivi sisi watu weusi kila kona tunachukiana wenyewe kwa wenyewe bila ya sababu yoyote ya msingi jambo la kukaa kama binaadam na kuzungumza utakuta ni chuki sasa kweli kutakua na maendeleo katika nchi?? hata wazungu wanatofauti zao lakini mara nyingi hukaa na kutafakari nini watatue kutoelewana kwao kwa manufaa ya raia zao na nchi lakini sisi ni lawama na chuki na kila mara hatutazami mema na mazuri yanayofanywa na viongozi ila yale mabaa tu sasa mema na mazuri tutayazungumza wapi ?? Jamani tujue mjenga nchi ni mwananchi na mbomoa nchi pia ni mwananchituwache lawamma zisizo kua na msingi kwa kifupi kila mmoja ajiulize yeye mwenyewe anaifanyia nini nchi??
ReplyDeleteNaamini JK Rais wetu ana busara ya kutosha kuweza kudharau vichwa vya magazeti vyenye lengo la kumchonganisha na Magufuli. Hivi nyie waandishi hivi kweli mnajua gharama ya uchonganishi?.
ReplyDeleteMheshimiwa Rais, Ukimtumia vizuri Magufuli utalala usingizi kwenye barabara na madaraja!usimchefue kwa ajili ya hao wapambe wenye nyumba kwenye hifadhi ya brbr.Iga mfano wa Mh Mkapa.alimsaidia Magufuli kutekeleza wajibu wake na aliwaheshimu wahandisi wa fani zote, ndiyo maana alikuwa hata anawakaribisha kula naye chakula Ikulu. wewe Je?
ReplyDeleteikibidi kuwa hivyo mheshimiwa kumuachia maamuzi yule uliemteua CCM itanoga naomba kila wizara iige mfano wa magufuri, hakuna atakae kwepa kulipa kodi
ReplyDeletekikwete n rais hewa si lolote kwa magufuli
ReplyDeletekwaasa tunamwomba mungu amuue kikwete kwa maslah ya wanyonge kwan n afadhal mmoja kufa ili taifa liokoke. chadema n chama cha wanyonge na mungu atakibark milele
ReplyDeleteMungu amlinde rais wetu kikwete, mi si mwanasiasa lakini wakati mwingine magufuli ameumiza wananchi bila huruma, wizara ya ardhi ndio inayotakiwa kulaumiwa zaidi kwa kuruhusu watu kujenga barabarani. tunapenda kuona maendeleo lakini pia kuteketeza maisha ya mwananchi kwa siku moja pia sio sawa. if you dont give mercy, you will never get one.GOD is GREAT
ReplyDelete