*Wachomoza nafasi 10 za kwanza
*St. Marian yaongoza kitaifa
Na Edmund Mihale
BARAZA la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha sita uliofanyika Februari, 2011 yakionesha kuwa wavulana wameongoza kwa kushika nafasi kumi za mwanzo, lakini Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Marian ya mkoani Pwani ikiendelea kushika nafasi ya kwanza kitaifa.
Wavulana walioshika nafasi kumi za kwanza kitaifa ni Muhagachi Chaha kutoka Shule ya Sekondari Kibaha, Samweli Katwale (Mzumbe), Amir Abdalah (Feza Boys), Aron Gerson (Tabora Boys), Shaban Omari (Tabora Boys), Kudra Baruti (Feza Boys), George Assenga (Majengo), Comman Ndulu (Feza Boys), Francis Joseph (Tabora Boys) na George Felix (Mzumbe).
Hata hivyo, pamoja na wavulana hao kujitahidi na kuibuka kidedea na wasichana kushindwa kuona ndani katika nafasi 10 za mwanzao, juhudi hizo zimeshindwa kuipiku Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Marian ya Bagamoyo mkoani Pwani ambao imeibuka ya kwanza kitaifa.
Kwa matokeo ya mtihani huo kwa mwaka 2009, wasichana waliibuka kidedea ulikinganisha na wavulana kwa kufaulu kwa aslimia 90.92 ukilinganisha na 88.89% za wenzao.
Wasichana kumi bora ni Doreen Kabuche (Benjamin Mkapa), Rahabu Mwang'amba (Kilakala), Mary Moshi (Kifungilo Girls), Nuru Kipato (Marian Girls), Zainab Hassan (Al Muntazir Islamic), Catherine Temu (Ashira), Athonia Lugomo (Usongwe), Cecilia Mvile (Kifungilo Girls), Mriam Mtovolewa (Kilakala) na Suzan Makoi (Tarakea).
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo, Dkt. Joyce Ndalichako alisema kuwa matokeo hayo yamepatikana kwa kuangalia kiwango cha jumla cha alama (GPA) kwenye masomo ya michepuo pamoja na wastani wa alama za jumla walizopata.
"Ufaulu wa masomo kwa watahiniwa wa shule unaonesha masomo ya Hisabati, Geografia, Fizikia, Kemia, Uchumi, BAM (Basic Applied Mathematics) yalifanya vizuri zaidi ukilinganisha na mwaka 2010," alisema Dkt. Ndalichako.
Alisema kuwa watahiniwa 49,653 sawa na asilimia 87.24 ya watahiniwa waliofanya mtihani huo wamefaulu (hawana daraja 0), kati ya hao ni wasichana 18,351 sawa na asilimia 88.74 wakati wavulana ni 31,302 swa na asilimia 86.38.
Alisema kuwa ubora wa ufaulu umepatikana kwa kuangalia madaraja waliyopata ambapo kwa watahiniwa wa shule unaonesha kuwa 34,949 sawa na asilimia 78.53 walipata daraja la kwanza hadi tatu ni wasichana 12,868 (79%) na wavulana 22, 081 sawa na asilimia 78.25.
Dkt. Ndalichako alizitaja shule zilizofanya vizuri na kuwa katika kumi bora kuwa ziko katika makundi mawili ambayo ni zile zenye wanafunzi zaidi ya 30 (334) na zenye wanafunzi pungufu za 30 (113).
Alisema kuwa shule zenye watahiniwa 30 za zaidi na idadi ya wanafunzi katika mabano kuwa ni Marian Girls (137), Feza Boys (53) Kifungilo (52), Kibaha (182), St. Marys Mzinde (84), Ilboru (162), Tabora Boys (155), St. Mary Goreti (240), Mzumbe (122) na Mafinga Seminary (32).
Alisema kuwa kundi la pili ni lile lenye wanafunzi pungufu ya 30 ambazo ni Uru Seminary (25), St. James Seminary (21), Maua Seminary (28), Same Seminary (28), Dungunyi Seminary (11), DCT Jubilee (7), Parane (17), St. Joseph Kilocha Seminary (16), Mlama (14) na Msama Girls (22).
Jumla ya watahiniwa 59,112 wakiwemo wasichana 21,291 sawa na asilimia 36.02 na wavulana 37,821 (63.98) ndio waliofanya mtihani huo mwaka jana.
No comments:
Post a Comment