Na Dunstan Bahai
BAADHI ya wabunge vijana wa vyama vya upinzani wamelaani kauli iliyotolewa na Katibu wa Bunge, Dkt. Thomas Kashililah na kueleza kuwa wao ni vinara wa
sheria na kanuni kuliko hata Spika wa Bunge, Bi. Anna Makinda.
Vile vile wameahidi katika bunge la bajeti watatoa hoja bungeni na kumtaka katibu huyo kufuta na kuomba radhi kwa kauli yake ya kuwaita wabunge mbumbumbu wa sheria na kanuni.
Dkt. Kashililah akizungumza na vyombo vya habari juzi, alisema kuwa vitendo vya fujo na kutoleana maneno ya kejeli baina ya wabunge wakiwamo ndani ya bunge, ni matokeo ya kuwepo kwa wabunge wengi wapya na wasiojua vema sheria na kanuni za bunge.
Wabunge hao walisema kuwa kauli ya Katibu wa Bunge imewadhalilisha wao, bunge na wananchi kwani amedharau wananchi kwa kuwa wamechagua wawakilishi mbumbumbu wa sheria na kanuni.
Mbunge wa Nyamagana (CHADEMA), Bw. Ezekia Wenje alisema kuwa katika bunge la mwezi wa sita atapeleka hoja bungeni ya kumtaka Katibu huyo wa Bunge kuomba radhi na kufuta kauli yake hiyo.
"Kutuambia wabunge ni mbumbumbu ni madharau makubwa sana na utovu wa nidhamu. Zile kanuni si dictionary wala biblia, huhitaji mwezi mzima kujifunza, ni ndani ya wiki moja tu umeshajifunza kwani ni kajitabu kadogo sana," alisema.
Kwa mujibu wa Bw. Wenje, wabunge vijana hawakubali kuburuzwa bungeni na wanakuja juu pale wanapoona kanuni zinavunjwa kwa manufaa ya kundi fulani.
"Wakiona wamebanwa kwenye vifungu, wanaamua tu kutengua kanuni, sisi hatutakubali na hatutanyamazishwa, tutaendelea kusema," alisema.
Mbunge wa Mihambwe (NCCR-Mageuzi), Bw. Felex Mkosamali alisema kuwa kwa upande wake amesoma sheria na kanuni na kufauli vizuri masomo hayo, hivyo anao uwezo mkubwa na upeo wa masomo hayo.
"Mtu kama mimi ni mwanasheria nimeenda darasani na maprofesa wamenipa A kwenye masomo hayo, sasa anataka hawa maprofesa kutuambia hawana akili?
"Spika tunajua si mwanasheria na ndiyo maana mbunge anapotoa hoja anamkatisha kabla hajamaliza. Tunaijua sheria na kanuni kuliko huyo spika anayemtetea," alisema Bw. Mkosamali wakati akizungumza na gazeti hili jana.
Aliongeza kuwa kauli ya Bw. Kashillilah imewadhalilisha na kusisitiza kuwa, kwa kuwa kipimo cha kwenda shule ni vyeti, hivyo alimtaka Spika kutoa vyeti vyake alivyosomea masomo hayo ili vilinganishwe na vya kwake.
"Wametudhalilisha sana, nia yao wanataka kutunyamazisha tukiwa bungeni...mwezi wa sita tunakwenda kuwasha moto ndani ya bunge," alisema.
Mbunge mwingine wa NCCR-Mageuzi wa jimbo la Kigoma Kusini, Bw. David Kafulila, hali kadhalika alilaani kauli hiyo na kusema kuwa fujo ndani ya bunge hazisababishwi na wabunge vijana tu, kwani wapo wazee wa siku nyingi ambao wamekuwa vinara wa fujo ikiwa ni pamoja na kutojua kanuni na sheria.
Alisema alichotakiwa kusema Katibu wa Bunge ni kuwataja wale wasiojua kanuni na sheria lakini anaposema wabunge wapya hawazijui, ni kuwadhalilisha wao na bunge lenyewe.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Bi. Ester Bulaya naye alipinga kauli ya Katibu huyo wa Bunge kuwa tatizo si kutozijua kanuni, bali wengi wa wabunge wanashindwa kutawala jazba zao na baadhi wana uchanga wa kisiasa.
Hata hivyo alisisitiza umuhimu wa wabunge kuendelea kujifunza taratibu za bunge ili waweze kutoa hoja za msingi huku wakizuia jazba zao.
Demokrasia ya vyama vingi nchini bado ni changa sana. miaka 20 tuseme ni kama kijana wa miaka 20. Mazoweya yale yale ya Chama kimoja kushika hatamu ndio inawasumbua Waheshimiwa. Wakati umefika tukubali changamoto ya Demokrasia ya vyama vingi. Ujana na Uzee wala upya Bungeni sio sababu za yanayotokea Bungeni. Tuanze kuzowea changamoto za damu mpya. Tuliwahi kushuhudia Bunge la Uingereza Waheshimiwa wanashikana mashati. Na hawa ndio wanademokrasia iliyo ota mizizi. Tukubali kwamba inafika wakati jazba, ni kweli, inazingira watu inapofika haki na ukweli vinapindishwa kwa makusudi. Mfano hoja ya juzi ya Mhe. Tundu Lissu. Eti tu kwa sababu imetolewa na mpinzani ambapo ilikuwa hoja nzuri kabisa hadi ikaungwa mkono na Mhe. Waziri Mkuu lakini wingi wa chama tawala ilibidi hoja hiyo inyongwe na kutupiliwa mbali. Je, hii tuiite nini? Ni uzoefu au upya Bungeni? Na bado mengi tutayashuhudia kama Wabunge wetu kama wataendeleza usani wao wa kuzidi kukumbatia maslahi ya vyama vya siasa Bungeni.
ReplyDeleteuwezo wa spika ni mdogo mno...kwa udhaifu wake huo amekubali kulishusha bunge na kuligeuza idara ya chama na serekali...na ya mafisadi kwa wakati huo huo....kwa hiyo mgongano wa kimaslahi pamoja na uwezo wake mdogo ndio unaharibu conduct ya bunge.....
ReplyDeletetutarajie mengi mwezi wa sita ambapo upande mmoja kuna wazee wa kujivua gamba, uopande wa pile wanahoji kagoda upande wa tatu kuwasafisha mafisadi...upande wa nne kukandamiza upinzani...lazima zinyukwe....
hl n tatzo la kuongozwa na spka kimada wa mafsad. tulijua tu bunge litamshinda kwan anatekeleza ya mafsad na s ya wananchi
ReplyDeleteNachangia kama mchangiaji huru asiye na affiliation na chama chochote. Huyu katibu wa bunge ambaye pia ni PhD holder awe mwangalifu kutoa fikira zake. Ufahamu na uzoefu hauji kwa umri au kufanya kitu kilekile kwa muda mrefu. Kwangu mimi uzoefu ni kuwa na uwezo wa kufanya kitu/kazi kwa ufanisi unaotakiwa (doing at its best) siyo miaka mingapi au umri gani unao au mara ngapi umefanya. Yeye na sisi ni mashahidi si wafanyakazi wote walokaa muda mrefu ofisini wanafanya kwa ufanisi zadi kuliko walokuja pale wakawakuta. Na si wafanyakazi wazee tu ndo wanatija zaidi kuliko vijana, swala hapa ni ku-deliver uwe mzee, kijana, umefanya siku nyingi au chache haijalishi.Katibu kuanzia sasa nakushauri upime uwezo wa mtu/watu kwa output/delivery siyo kwa umri, tenure, jinsia au rank utasaidia sana. Bt kwa vigezo vyako vya sasa daktari unawakilisha watu wote wenye mawazo finyu ati kuwa umri na kukaa sehemu muda mrefu ndo uzoefu!! hayo ni mawzo mwitu, mawazo ya dunia ya kale zaidi ambayo wewe hutakiwi kuienzi! Kwa mantiki hii kweli msomi PhD holder umechemka nakupa B plane tena kwa kutumia diplomacy maana si busara kumpa F katibu wa bungu la nchi yangu.
ReplyDelete.......watanzania tunasumbuliwa na ushabiki wa kisiasa lakini ukweli ni kwamba mambo wanayoyafanya wabunge wapya pale bungeni ndiyo yanayomfanya katibu wa bunge aseme haya...Anapozungumzia maadili ya utumishi wa umma anajua kwa sababu mtu anpotoka chuo na kwenda kazini ndani ya utumishi wa umma ni lazima atajua taratibu na sheria za kuendesha mambo mbalimbali kwa mujibu wa kuutumikia umma ,huwezi kuulizwa swali na mwananchi unayemhudumia ukaanza kukwepesha mada...Kupata A chuo kikuu sio kipimo kuwa umeelimika na unaijua sheria kwani elimu yetu inanakilisha zaidi kuliko kupanua fikira zenye uelekeo wa kufanya tafakuri jadidifu sasa mambo kama haya yanpatikana kwa kuutumikia umma ...unaweza kufikiria mtu ametoka chuo au mfanyabiashara hajawahi kufanya kazi za umma popote leo anaingia bungeni si ndio wale wanosema fungeni milango tupigane...mambo mengine hata yanashindwa kueleweka kwa mtu mwenye utimamu wa akili....Kati ya mambo ambayo mtu anatakiwa afanye jitihada ni kutambua mambo katika uhalisia wake...(Hivi msomi anayejiita msomi anaweza kuam,rishwa na mtu ambaye hana uelewqa wowote kuwa asusie kikao cha bunge naye akafanya hivyo hata kama ni kwa shingo upande bado uelewa wake tunautilia shaka hata kama ni profesa wa sheria tunajua tu kwamba ni kweli amesoma lakini hajaelimiaka)...Think big,act big.....a real man need no advice...
ReplyDeletewabunge wengi wazoefu hapo bungenei hata hawasomi miswada mbalimbali wao wanalala tu bungeni na kusema imepita hiyo , ni wavivu wa kufikiri si wabunifu hata kama kitu hakina maslahi kwa taifa au litaletea taifa hasara wao wanasema imepita hiyo.......taabu kwelikweli . wabunge wengi vijana wameenda shule bwana hawawezi kuburuzwa ..alafu watu wengine kama huyu katib wa bunge yeye ndiyo anajiona ni mtanzania kuliko wengine asijisahau cheo ni dhamana usiwaletee watu dharau kwa sababu ya cheo chako .
ReplyDeletePossibly huyo Katibu alitumwa aseme aliyosema. He is employed by the govt so he was speaking on behalf of the govt. the current speaker has totally failed in her duties. Luckly there are no prefoformance indicators to fulfill, she will continue to underperform for the next five years. It is a total joke.
ReplyDeletewewe mchangiaji unayesema think big, act big. kwahiyo wewe unamtetea katibu wa bunge kuwatukana wabunge wapya kwa ujumla wao eti tu kwasababu ya mtu mmoja aliyesema funga milango tupigane. Sasa wewe unathink big kweli kwa kuwatetea wabunge wa zamani wamefanyanini cha maana, mikataba mibovu iliyotufikisha hapa waliiona na wakawa kimya miaka yote, ivi unajua kinachoendelea ktk migodi yetu, bandari zetu na shirika la umeme Tanesco? Nasema wazi kuwa wabunge vijana- Zitto,Halima mdee etc na wazee wapya ktk bunge km kina mwakyembe, sita, anna kilango, Dk Slaa bila kujali vyama wametusaidia sana. Kukaa muda mrefu bungeni si kipimo cha tija, kukaa kimya unapoona madudu ati unatii maadili ya umma ni upuuzi mtupu! Kwahiyo wizi wote uliokuwa ukitokea na hao wabunge wazamani unaowasifia wakazidi kukaa kimya bila kuhoji ndo maadili ya umma na uzoefu?. Kwakuwa alisema taazizimwe wazichape anajulikana ndo mbunge ambaye katibu wa bunge na taratibu zilizopo wangemchukulia hatua, na siyo kujitokeza kutukana wabunge vijana. Katibu alichemka msimutetee hata km kakosea. Unajua nchi yetu watu wengi hata baadhi ya wasomi nahisi mfumo umewateka na hawezi kufikiri vizuri tena ndo maana hata uozo wanakaa kimyaa au kuutetea waziwazi majukwaani. Jamani sisi tunaoishi ughaibuni tunaulizwa kila mara kwanini tumeachia rasimali mfano madini watu wanabeba tu- GDP, Exports zinaonekana kubwa wakti uhalisia kwa maisha ya watanzania ni mbovu? Wewe unayetetea wabunge wazoefu na katibu wa bunge ungejibu nini? Najua ungeleta siasa nyingi za ajabu badala ya kujibu straight kwamba tuna corrupt government at Executive level na wabunge wa ndiyo imepita.... bila kuhoji na bila kusimamia vizuri utendaji wa serikali. Nw we have some MPs who real want to fine tune the govt's conducts hafu mnawapuuza?. Jamani hebu tuwe objective siyo kum-back mtu hata km kakosea humsaidii, naamini katibu amejifunza kwa walosema ukweli na hatorudia kuropoka, mnaom-back up hamjamsaidia!
ReplyDeleteMchangiaji wa juu yangu hapo big up, nami nilikuwa na mtazamo kama wako. Nahisi huyu anayetetea makosa ya wazi ya Katibu wa Bunge ni FISADI. Viongozi wetu wengi wa juu hawapo tayari kwa mabadiliko yatakayotuletea tija. Wamekuwepo kwenye mfumo wa kuendesha serikali kwa mazoea na kuteteana. Lazima sasa wakubali mabadiliko, na wakiyakataa yatakuja kwa nguvu. Hatuwezi kuangalia nchi inavyofujwa na kunyamaza, eti sababu sisi vijana. Kufuatia kauli yake anataka nasisi tujumuishe kwa kusema wazoefu Bungeni/Wazee wameridhia nchi kufujwa kwa mikataba mibovu na UFISADI uliokithiri.
ReplyDelete