LONDON, England
NAHODHA wa timu ya Arsenal, Cesc Fabregas amewashutumu wachezaji wenzake kwa kushindwa kuzishinda nafsi zao, jambo ambalo amesema ndiyo chanzo
cha kushindwa kutwaa ubingwa.
Katika mahojiano na waandishi wa habari jana, Cesc alieleza kufadhaishwa kwake na Arsenal kwa kushindwa kutwaa ubingwa wowote.
"Ni vigumu kwangu mimi kwa kushindwa kuzishinda akili na vilevile utoto kwa sasa ni tatizo kubwa," alisema.
"Tuna uwezo wa hali ya juu, lakini kujiamni ndiyo tatizo. Tatizo ni kwamba timu inahitaji kushinda kitu chochote na ndiyo maana tunapaswa kushinda Kombe la Ligi," alisema.
Alisema wanahitaji kushinda kombe hilo, ili waweze kujiamini binafsi na akasema kwamba pamoja na mchezaji, Robin Van Persie kutwaa Kombe la FA lakini bado hakujaongezeka kitu.
"Hakuna mchezaji yeyote ndani ya timu ambaye ameshashinda taji lolote. Tumekosa uwezo wa kuongea na kwa sasa nafahamu ni kitu gani cha kushinda na ambacho tutakwenda kushinda," alisema.
Alisema ushindi huo ndiyo utawafanya Arsenal, kuwa timu imara na kufahamu jinsi ya kushinda mechi.
No comments:
Post a Comment