21 April 2011

Timu ya ngumi kuanza mazoezi Aprili 27

Na Mwali Ibrahim

TIMU ya taifa ya ngumi za ridhaa, inatarajia kuanza mazoezi kwa ajili ya mashindano ya Mataifa ya Africa 'All African Games' Aprili 27 mwaka huu katika Uwanja wa
ndani wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT), Eckland Mwaffisi alisema timu hiyo itaanza mazoezi ya kwenda na kurudi kwa ajili ya kujiandaa na mashindano hayo, yanayotarajia kutimau vumbi Desemba 3 hadi 15 mwaka huu Maputo, Msumbiji.

Alisema katika mazoezi hayo, timu hiyo itakuwa chini ya Kocha Mkuu Mcuba Hurtado Pementel, akishirikiana na makocha wazawa ili kuhakikisaha kikosi hicho kinakuwa imara kiushindani.

Mwaffisi alisema, katika kuhakikisha wanaipima nguvu timu hiyo watasikiliza mawazo ya makocha jinsi watakavyokiona kikosi hicho, kama wataweza kushiriki katika ya 'Community Championship' yanayotarajia kufanyika Juni 5 hadi 12, mwaka huu nchini Uganda.

Alisema mashindano hayo ni makubwa na yatashirikisha timu 14, ambapo timu nyingi kati ya hizo zitashiriki katika mashindano ya All African Game hivyo kushiriki kwa wachezaji kwenye michuano hiyo kutwasaidia kupata uzoefu zaidi kwa timu hizo.

"Mashindano hayo yatawasaidia kuwasoma washiriki wenzao, kwani pia watakutana nao katika michuano ya Africa, hivyo tutawasikiliza makocha wakiona wamewaandaa wachezaji kiasi cha kutosha tutaipeleka timu Uganda kwenda kujipima na timu hizo," alisema Mwaffisi.

No comments:

Post a Comment