Na Zahoro Mlanzi
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, timu ya Simba, leo itajitupa tena uwanjani kuumana na maafande wa JKT Ruvu katika mchezo utakaopigwa
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ili.
Simba itashuka uwanjani ikiwa na machungu ya kuondolewa katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika na mabingwa watetezi wa michunao hiyo, TP Mazembe kutoka Jamhuri ya Kidemnokrasi ya Congo (DRC) kwa jumla ya mabao 6-3.
Timu hiyo itashuka uwanjani ikiwa na lengo moja la kuibuka na ushindi na kama ikishinda itafikisha pointi 48 na kubakiwa na pointi mbili tu, iweze kutetee ubingwa wake kwa mara ya pili mfululizo.
Simba ikifikisha pointi 50 hakuna timu yoyote itakayoweza kuzifikia pointi hizo kwani Yanga, ambayo ipo nafasi ya pili kwa pointi 43 ikishinda michezo miwili iliyobaki itafikisha pointi 49.
Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Phiri baada ya kupoteza mchezo wake dhidi ya TP Mazembe, alisema sasa nguvu anazielekeza katika michezo miwili iliyobaki kwa kuhakikisha wanatwaa ubingwa.
Alisema kutwaa ubingwa wa ligi hiyo, itarudisha morali kwa timu yake baada ya kuondolewa katika michuano hiyo mikubwa na itafungua njia kwa ajili ya kujipanga kwa mwakani.
Kwa upande wa timu ya JKT Ruvu, yenyewe haina chakupoteza kwani ipo nafasi ya sita ikiwa na pointi 26 hivyo haina cha kuwania wala hatihati ya kushuka daraja, kwa hiyo itakuwa ikijiimarisha katika msimamo wa ligi hiyo.
Kocha Mkuu wa timu hiyo, Charles Kilinda akizungumzia mchezo huo, alisema timu yake siku zote inacheza soka la kufundishwa na haitakuwa tayari kufungwa na Simba, kwani wanachozingatia ni kupata rekodi nzuri.
No comments:
Post a Comment