MADRID, Hispania
REAL Madria inatarajia kumgeuzia mgongo,Emmanuel Adebayor wakati mkataba wake wa mkopo kutoka Manchester City utakapoisha mwezi ujao.Adebayor mwenye
miaka 27, amefunga magoli manne, mawili kati ya hayo aliifunga Tottenham katika muda wake aliochezea Bernabeu.
Mshmabuliji huyo wa zamani wa Arsenal, alifurahi sana kupata kombe lake la kwanza tangu aanze kucheza soka ya kulipwa Ulaya, baada ya Real Madrid kutwaa Kombe la Mfalme kwa kuifunga Barcelona bao 1-0 katika fainali iliyopigwa wiki iliyopita.
Lakini kutokana na City kutaka dau la pauni milioni 12 kwa mchezaji huyo waliyemnunua kwa pauni milioni 25 kutoka Arsenal mwaka 2009, imefanya miamba hiyo kushindwa kufikiri kumsaini, pamoja na safu yake ya ushambuliaji kuanza kufunga magoli.
Karim Benzema ameendelea kufunga magoli wakati, Gonzalo Higuain amerejea uwanjani na kuanza kufunga mabao baada ya kuwa nje ya uwanja kwa miezi minne kutokana na kuumia, Jumamosi katika mchezo dhidi ya Valencia alifunga magoli matatu.
Kocha wa City, Roberto Mancini ambaye anaweza kumkosa mfungaji wake Carlos Tevez, tayari anamkaribisha Adebayor kurejea.
Kocha huyo mtaliano alisema: "Mwishoni mwa msimu, tutaona kama Emmanuel atataka kubakia hapa."
Lakini Adebayor anataka kuondoka City moja kwa moja na angependa kubakia Real.
Mshambuliaji huyo anaweza akawa amesikitishwa sana na habari hizo lakini ana kitu kingine cha kuamua, huku Lazio nayo ikimtamani nyota huyo wa Togo.
No comments:
Post a Comment