Na Cresensia Kapinga, Songea
ASKARI 26 wa Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma wamepatiwa tuzo na nishani kwa utendaji uliotukuka baada ya kukamata silaha zilizokuwa zikitumiwa na majambazi
waliouawa wilayani Tunduru.
Askari hao wamepatiwa tuzo na nishani juzi kwenye viwanja vya Kituo Kikuu cha Polisi ambako Kamanda wa Polisi mkoani hapa na Bw. Michael Kamuhanda kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Saidi Mwema na kuhudhuriwa na mamia ya wakazi wa Songea wakiwemo askari polisi.
Bw. Kamuhanda alisema kuwa askari 13 wamepatiwa vyeti vya utumishi uliotukuka kwa niaba ya askari wote wa mkoa wa Ruvuma na askari 14 wamepata vyeti na pesa taslimu kati ya sh. 100,000 na sh. 150,000 kwa utendaji mzuri wa kujituma ambapo walifanikisha kukamatwa kwa bunduki tatu za SMG wilayani Tunduru.
Alifafanua kuwa askari watano ambao walizawadiwa cheti na sh.100,000 kila mmoja walifanikiwa kukamata bunduki iliyokuwa imefichwa kwenye makaburi maeneo ya Msamala mjini hapa ambayo ilikuwa imezungushiwa kwenye kiroba ambayo inadaiwa ilikuwa imeporwa na majambazi kwenye Kituo cha Mafuta cha OTTAWA kilichopo Msamala, Manispaa ya Songea.
Askari polisi tisa wa Wilaya ya Tunduru walipewa cheti na sh. 150,000 kila mmoja kwa kukamata bunduki tatu aina ya SMG ambazo zilikuwa zikitumika na majambazi ambao waliuawa katika majibizano ya risasi na polisi
Kamanda Kamuhanda aliwataka askari wote mkoani hapa kufanya kazi kwa bidii, kwa uamainifu na uadilifu kwa lengo la kupunguza uhalifu nchini.
No comments:
Post a Comment