Na Sophia Fundi, Karatu
WANANCHI wa Kijiji cha Chemchem wilayani hapa jana walifukua mwili wa marehemu Matle
Shauri (52) aliyezikwa siku tatu zilizopita na kuuzika
sehemu nyingine karibu na nyumba yake kwa madai kuwa eneo alilozikwa marehemu lilikuwa la kijiji.
Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kwa kaka wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Costantin Shauri walimzika lakini siku tatu baadaye baadhi ya wakazi wa kijiji hicho walipiga yowe kuitana usiku wa kuankia siku ya tukio ambapo walikusanyika wakiwa wamebeba mikuki, mapanga, beleshi na majembe kufukua mwili na kuuzika upya.
Baada ya kifo cha marehemu na ndugu wa zake kuuzika mwili wake mwenyekiti wa kijiji hicho Bw.Tlatlaa Bura alipeleka malalamiko hayo katika kituo cha polisi Karatu ambapo walikaa kikao wanandugu na uongozi wa
kijiji na kukubaliana kuwa mwenye malalamiko ya kuwa eneo ni la kwake akafungue mashtaka.
Alisema kuwa walikubaliana kwa pamoja lakini baada ya saa mbili wananchi hao wakiwa
wamebeba silaha za jadi walivamia kaburi hilo na kuanza kufukua mwili na kuuzika kinyama kwenye kaburi futi tano.
Bw. Shauri alisema kuwa kitendo walichofanya wanakjiji hicho ni cha kinyama kwa kuwa kama eneo ni la kwao wangechukua hatua za kisheria kuliko kufukua mwili wa marehemu na kwenda kuuzika tofauti na familia ilivyopanga.
"kama sisi tuna makosa na tumevamia eneo la kijiji tungefunguliwa kesi kuliko kwenda kufukua mwili wa marehemu ambaye hakuwa na kosa lolote na kuifanyia familia unyama kwa
kumchimbia futi tano, "alisema ndugu wa marehemu huku akilalamika.
No comments:
Post a Comment