20 April 2011

Mourinho apondwa kwamba si lolote

MADRID, Hispania

JOSE Mourinho, amepondwa kwamba si lolote baada kutumia mbinu mbaya baada ya timu ya ya Real Madrid kucheza kwa kujihami na kutoka sare ya
bao 1-1 dhidi ya Barcelona.

Madrid inazidiwa pointi nane katika msimamo wa Ligi Kuu Hispania, leo inakabiliana tena na Barcelona katika mechi ya fainali ya kuwania Kombe la Hispania na kisha kucheza mechi mbili za nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Mourinho katika mechi iliyopita alitumia mbinu ya kuchezesha walinzi wanane nyuma lakini mchezaji wake, Raul Albiol  alioneshwa kadi nyekundu kwa kucheza rafu.

Mchezaji wa zamani wa Uholanzi na Barca, Johan Cruyff alisema: "Mourinho si kocha wa soka.

"Kucheza nyumbani ukitumia walinzi saba, lazima utakuwa na hofu kubwa.

"Ilinikumbusha fainali ya Kombe la Dunia mwaka jana. Nchi yangu ya Uholanzi iliamua kuisimamisha Hispania kuliko kucheza wenyewe."

Hata mchezaji wa zamani wa Madrid, Alfredo Di Stefano alisema: "Barcelona inacheza soka na dansi wakati Madrid, inaonekana kukimbia tu. Barca ni simba, Madrid ni panya."

No comments:

Post a Comment