14 April 2011

CCM waenda mikoani kuukana ufisadi

*Wapeleka ujumbe wa NEC mkoa kwa mkoa
*Nape asema watapambana hadi washinde


Na Edmund Mihale, Dodoma

CHAMA Cha Mpinduzi (CCM) kimeanza ziara mikoani kupeleka ujumbe wa
Halmashauri Kuu ya CCM kwa wanachama kuwa kimedhamiria kupambana na ufisadi ndani na nje ya chama hadi kishinde.

Katibu wa Itikadi na Uenezi, Bw. Nape Nnauye aliyasema hayo Makao Makuu ya chama hicho mjini Dodoma jana, wakati akitangaza ratiba ya mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Wilson Mukama na Sekretarieti ya chama hicho mkoani hapa.

Alisema chama hicho kimeandaa ziara kwa ajili ya kufikisha ujumbe wa Halmashauri Kuu kwa wanachama wake kuanzia leo ambapo watafanya makutano katika Uwanja wa Nyerere Square na kesho Mkoani Morogoro.

Alisema kuwa mapokezi hayo yataendelea katika Mkoa wa Pwani Wilaya ya Kibaha ambapo yatapokelewa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete. Alisema kuwa siku hiyo hiyo yataendelea katika Mkoa Dar es Salaam na Aprili 17 mwaka huu yatakuwa Zanzibar.

"Tutapambana na ufisadi hadi tushinde," alisema Bw. Nnauye.

Alisema kuwa CCM haitavumilia kuona inachafuliwa na watu wachache na kuwataka wanachama waliohama kwa hasira kutokana na kashfa ya ufisadi kurudi kundini.

Alisema uamuzi uliofikiwa katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa utafanyiwa kazi.Alisema uamuzi wa kuwachukulia hatua wanaojihusisha na ufisadi uko pale pale, hivyo wasidhani kuwa chama kimeishia hapo.

"Ndugu zangu Halmashauri Kuu iliamua kuwa tutapambana na ufisadi hadi tushinde, hivyo kama alivyozungumza mwenyekiti, wanaotuhumiwa wajiandae, tumefunga milango na madirisha yote, ili kuhakikisha tunashinda," alisema Bw. Nnauye.

26 comments:

  1. hata mkipita nchi nzima hamna lolote hamuwezi kushinda tena!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. Mimi nataka nione kwa macho yangu kuwa Rostam, Lowasa, Chenge, na wengine waliojulikana wazi kuwa ni mafisadi wanaenda jela, hapo nitaamini. lakini haya mnayotuambia ni changa la macho tu. uwezo wenu ni mdogo sana kupambana na hawa watu. msitudanganye.

    ReplyDelete
  3. Nape hiyo sio njia ya kuushinda ufisadi. ccm itashinda tu ufisadi ikiwaweka ndani mafisadi wote na kutaifisha mali zote walizofisadi

    ReplyDelete
  4. nyie mnaosema mpo mjini ndiomaana shudia maandamano ya ccm ndio utajua kuwa wanapendwa na wananguvu kubwa kaeni pembeni nendene mboe club mkaombe kazi mtapewa tu

    ReplyDelete
  5. Ni ngumu CCM kushinda ufisadi kwani mwenyekiti haamini kama upo. Itakuwaje amnyanyue mkono Lowasa mbele ya watanzania kuwa ndiye mgombea anayefaa Monduli? Hata kama maakama hajasibitisha lakini ripoti ya mwakyembe si ameisoma na Lowasa alipewa nafasi hakukana mbele ya bunge.Ufisadi ni best fiend wa CCM huwezi kuwatenganisha.

    ReplyDelete
  6. We unayesema twende tukaone jinsi CCM inavopendwa, unafikiri hatujua kuwa huwa mnakodi malori na mabasi kusomba watu kutoka sehemu mbali mbali ili wakajaze mikutano ya chama kionekane bado kina ungwa mkono. Na ukimuuliza huyo mtu kilichompeleka pale hajui, tazama serengeti boys (watoto) waliopelekwa kufanya fujo Karimjee, walipelekwa kwenda kufanya fujo na kupiga kelele.

    ReplyDelete
  7. Dawa si kuzunguruka mikoani, bali kushughulikia vilivyo mafisadi watuhumiwa wote. CCM hamjashtuka tu!kuwa watanzania wanaelimika kwa kasi kuhusu siasa!

    ReplyDelete
  8. HAWAWEZI KUSHUGHULIKIA MAFSADI KWA KUZUNGUKA NCHI NZIMA. KWANI HIYO SI DHAMIRA YAO, NI HADI VYAMA VYA UPINZANI NA WANANCHI WAPIGE KELELE WE, NDO WAJUE KUWA KUNA MAFISADI NDANI YA CHAMA. NI MIAKA MINGAPI SASA KELELE HIZO ZIMEPIGWA. UNAONA WANAVYOKURUPUKA HATA JINSI YA KUPAMBANA NA UFISADI NDANI YA CHAMA, ETI KUZUNGUKA NCHI NZIMA KUWAELEZA WANANCHI. HEBU WAFUKUZENI KABISA UANACHAMA TUONE KAMA MNA NIA YA DHATI KWELI YA KUPINGA UFISADI.

    ReplyDelete
  9. nakuaminiya Nnauye ccm chama makini na ishallah mungu akipenda kitaendelea kushinda tu siku hadi siku hawa chadema chama cha kibaguzi tushakiishutukizia kazi yao kueneza chuki tu ila kwa uwezo wa mola tutashinda tu ubunge ,udiwani,Uraisi na katika chaguzi zote za kisiasa hawa ambao wanapiga kelele ni wehu tu na wahuni ila ccm chama makini na kitaendelea kutawala mpaka kiama hapa hatutoi nchi mtazunguruka nchi nzima mpaka mtoke majasho ya ulimi lakini ccm itashinda tu na itaendelea kutawala daima

    ReplyDelete
  10. Wanaoipenda CCM ni wale wanaojilimbikizia mali kupitia hicho chama, na wale wasiojua lolote kinachoendelea kuhusu siasa ya nchi hii.Ila pakacha walimowekwa wapenzi wa CCM lina matundu mengi na letu lipo chini yake linajaa.

    ReplyDelete
  11. Wewe unayesema hamtoi nchi unamaana gani? ni ya mjomba wako kwani? unadhani Bhagbo alipenda kuiachia hata nyie tutawalazimisha kama mkikiuka utaratibu.

    ReplyDelete
  12. NAPE HUWEZII! UMEWEKWA HAPO CHAMBO TU.Wewe na wenzio mnao ubavu wa kuumaliza ufisadi?Jitahidi lakini chunga sana usije poteza moto.wenye pesa huwawezi.Ndio maana wazee wamekutanguliza wewe!

    ReplyDelete
  13. Nape atanusa kama paka likimshinda anajeza nduki. Yetu macho kama wenye damu ya CCM WAMESHINDWA SEMBUSE SISIMIZI.

    Nape usianza kupiga yowe tafadhali, wenzio wamevua mpaka gamba la nyoka lakini wako kimya. Usije kutuletea habari za akina KOLIMBA HAPO BAADAYE, kalelee familia yako.

    ReplyDelete
  14. CCM hamna aibu, eti mtazunguka nchi nzima kwani nyie ndo mligundua huo ufisadi? c mliutengeneza wenyewe hala umewabeba. sasa kama ufisadi umewapandisha kwenye tawi halafu mnatuambia mtahakikisha mnashinda yaani kukata tawi mlilokalia sijui kama mtapona. Kwa watu wenye akili wala wasingezungumza kitu. mnaonesha mlivyo mazuzu. Mlidai mfalme kavaa nguo isiyoonekana, leo nguvu ya umma imeambiwa mfalme yuko uchi nanyi mnashabikia yuko uchi! MMEKWISHA. kuzunguka nchi nzima ni kuipa nguvu CHADEMA ambao ndo walituamsha.Mtacheza muziki wa CHADEMA mpaka mtawaweka madarakani.

    Hebu zungukeni muone mtakavyoaibika. hao kina Lowasa Rostam na Chenge ni wa kutupwa jela na mali zao kutaifishwa. Mkiweza kufanya hivyo mnaweza kukiridishia chama heshima kwa 25%

    Mliichafua ccm, mmewafanya wtz. mafukara huku mkiishi kama mpo peponi. Mmepumbaza watu kwa t-shirt za kijani ambazo kwa ufukara uliopo vijijini zile zimeonekana ni nguo za
    kutokea ! Kwa kweli ccm mnastahili adhabu.

    ndege zinaruka kutoka migodini bila kukaguliwa ! miaka 50 baada ya uhuru hatuna umeme huku tukiwa na rasilimali za kutosha kuzalisha umeme!

    Kilio cha njaa kila kukicha huku tukiwa na mabonde yenye rutuba isiyo kifani. Mazao yanakauka pale bonde la rufiji meta zisizo zidi 10 kutoka mtoni kwa kukosa mvua!

    ccm kama mtazunguka nchi nzima tuambieni RUBADA ni nini na wanafanya kazi gani, mbona hakuna kinachofanyika bonde la mto rufiji? Njaa inatoka wapi wakati Gadafi analima jangwani?

    CCM mmejengea wananchi uvivu wa kufikiri. angalia kila kijana anataka kuwa mmachinga, kuzunguka na soksi 2. Na kuwamaliza kabisa mkabuni jengo la Machinga complex. Ule ni mradi kichaa kwa vile walioko pale wala sio walengwa. miradi kama hii inafanikishwa kwa manufaa ya wachache.

    Pia mnadai yajengwe kila manispaa ya dsm ili muwavute vijana kutoka vijijini waje dsm. nilifikiri wangewezeshwa hukohuko vijijini wakaweza kuzalisha tukaondokana na njaa ya kila siku.

    Angalia msongamano ulioko dsm, serikali imekataa kuhamia ddm yalipo makao makuu ya nchi. tumeng'ang'ania dsm na kusababisha msongamano unaokera huku tukiwa tumekamuliwa fedha za kujenga makao makuu ya nchi. dsm ni bandari sio mji mkuu ! ccm hawajui ! wanawaza barabara za juu na magari yaendayo kasi. serikali ingehamia ddm hakungekuwa na msongamano dsm. CCM poleni sasa ni nguvu ya umma kwa kwenda mbele.

    ReplyDelete
  15. Kama CCM inasema imevua magamba, itafanyaje ili magamba haya yasiendelee kuwa wawakilishi wa wananchi?

    Imagine, mtu anaitwa gamba halafu anaendelea kuwa mbunge!
    Mtu anaitwa fisadi huku anaendelea kuwa kiongozi!
    Only in Tanzania can this happen!

    ReplyDelete
  16. mtoto wa nyoka ni nyoka, sembuse nyoka aliyejivua gamba!

    Bora wangejifananisha na kitu kingine, wanajifananisha na joka!

    ReplyDelete
  17. Pia tusisahau ni wajibu wao CCM kujitetea, ingawa siyo rahisi kubadilisha tena watu kutokana na vuguvugu la demokrasia lianloikumba bara la Afrika. Mimi nashngaa hadi sasa watu hawajaamua kuwaondolea mbali viongozi walio madarakani. Hawajibiki hata kidogo, lao ni kuangalia mambo yao kwa kuhangaikia chama cha siasa huku watu wakiendelea kuteseka kwa umaskini. CCM waache usanii na wabuni njia za kuondoa umaskini unaondelea kukithiri Tanzania. Kutokomeza ufisadi siyo lazima kupitia hicho CCM bali kuwashughulikia na watu waone, hapo tunaweza kuwa na imani. Kwa kheri CCM, hata mkibadilisha uongozi ni bure. Wanachotaka watu ni mabadiliko ya vitendo kwa kuwashughulikia waoibia taifa fedha ambazo zingetumika kuwaletea watu maendeleo.

    ReplyDelete
  18. CCM haiwezi kumtoa Lowassa, Chenge na Rostam kwenye chama, kama hawaitakii mema CCM basi wajaribu waone! Msitudanganye kuwa mmejivua GAMBA hii ni kukimbia kivuli chako! Iweje Mafisadi wapewe Siku 90 za kupima waone kama wanafaa kuendelea au? Huu ni uhuni na uonevu mkubwa hasa viongozi wa chini maana wao wakifanya makosa kidogo tu,atakimbizwa kama kuku kwenye nafaka! Kama kweli mwenyekiti alikuwa na nia ya kuwaondoa kwenye uongozi hao watu ni siku ile ile angewambia wajiuzulu! Mbona secretariete haikupewa muda wa kupima wao wamepewa? Huu ni uonecu na inathibitisha kuwa chama chetu ni cha watu wachache tena wafanyabiashara wakubwa na sio wakulima na wafanyakazi kama ilivyo kuwa hapo mwanzo! Kama tunataka kupata imani kwa wananchi kuvunja secretariet pekee hakutoshi! Waondoke wale wote wasiokitakia mema chama na wamekifanya kikose dira kwa vijana walio wengi! (maana wazee (Makada) waliowengi wanazidi kupungua kila kukicha)!
    Kingine kinachofanya chama kikose Mvuto kwa jamii ni kule kuendekeza ufamilia katika chama, eti kisa ni mtoto wa fulani basi apewe nafasi (Mfano Ridhiwan, Nnape, Makamba, mwinyi, Karume, na wengine) Najua wengine mtarukia hoja kuwa kama wanasifa wasipewe? Lah hasha! Wapewe kwa kufuata utaratibu kama wengine wanavyofuata sio kwa kutoa favor (Kwa kuwa baba au mama ake ni fulani...). Tukumbuke yanayotokea Misri Libya na kwingine yalianza hivi hivi na mwishoe tukaona viongozi wakitaka kuwasimika watoto wao nyadhifa fulani kama hali hii haita dhibitiwa katika chama basi tutegemee yaliyotokea Misri.

    ReplyDelete
  19. YAANI CCM KILA JAMBO MPAKA MSHINIKIZWE NA CHADEMA. MFANO UFISADI NI CHADEMA WALIOTOA LIST OF SHAME" THEN KUWADHALILISHA KWA WANANCHI NDIO MMESTUKA. KATIBA MPYA CHADEMA WAMEWATIKISA NDIO MKALETA MSWADA FEKI, MFUMUKO WA BEI MPAKA CHADEMA WAMEWATIKISA NDIO MKAZUNGUMZIA KUPUNGUZA GHARAMA ZA UMEME, DOWANS MLISHAIDHINISHA NA CC YENU, MAWAZIRI, NA PM, NA MWANASHERIA MKUU,BAADA YA CHADEMA KUWATISHIA NGUVU YA UMMA NDIO MNASEMA HAMLIPI, CHADEMA WAKAMFOSI KIKWETE AWATAJE DOWANS AKAENDA KULALAMIKA DODOMA HAWAJUI, NA HATA HUU MUSWADA FEKI CHADEMA WANAUTIKISA MTAUTOA TUU, DUU KWELI CCM MMEPOTEZA DIRA NA MUELEKEO. SASA HIVI MTAPIGWA NA RA & EL NA UPANDE WA PILI CHADEMA. HATA HIYO KUTOA MAFISADI NDANI YA CC HAIKUWA DHAMIRA YA JK KWA HIYO KINA NAPE KUWENI MAKINI, MKUU WA KAYA" TWO IN ONE" HUYO. MCHANA MNAPANGA NAE USIKU ATAWASALITI KWANI ANA MASLAHI NAO OR ANA MADUDU YAKE MAFISADI WANAYAJUA. CCM NI KAMA PUNDA HAENDI BILA KIBOKO NA KIBOKO CHAO NI CHADEMA, BILA CHADEMA IMARA NCHI YENU INGEKUWA MIFUKONI MWA MAFISADI. GO CHADEMA GO SLAA. WABILLAH TAWFIQ!!

    ReplyDelete
  20. jamani nasema tena CCM ni chama makini chama cha wasomi sio chama cha kihuni au cha kikabila kama chadema ccm ni chama cha watu ambao walokwenda shule sio chama cha kichaga au cha kihaya hichi sisi msimamo wetu ni maendeleo kwa wananchi na hatutosita kuleta maendeleo kwa kelele zenu mwenye macho hambiwi tazama nchi toka alipoondoka nyerere maendeleo mangapi yamepatikana mpaka sasa acheni kelele zenu hizo nyinyi chadema ni watu hatari kama sumu ni wabinafsi na niwatu wajanja ambao mnataka nchi ili muweze kuitumia kwa masilahi yenu nakwambieni kama mmechelewa sio leo tena CCM sio daladala kila moja akawachiwa abande tu leo aje huyu kesho huyu serekali hatutoi ngo

    ReplyDelete
  21. Rostam na Lowassa walishiriki kwa kiasi kikubwa sana kumweka Kikwete madarakani mwaka 2005. Haiwezekani akawatupa. Hii ni danganya toto. Haiwezekani Lowasa aliilazimisha Tanesco kuingia mkataba na Richmond/Dowans (ambayo Rostam ni mbia)bila Kikwete kujua.Mali ya kifisadi ya akina Rostam ilisaidia kumwingiza Kikwete ikulu; kwa hiyo atawatupa hadharani tu lakini ndani lazima awasidie. Kumbuka Kikwete alipochukua uenyekiti tu, alimfanya Rostam kuwa mweka hazina wa ccm.

    ReplyDelete
  22. umakini utoke wapi we mjumbe wa nyumba kumi, kazi yako dobi, watoto wako wahalifu sugu, hujui kusoma hata kuangalia picha huwezi, amka mzee, CHADEMA YA WATZ NA SI YA UKABILA KMA UNAVYODHANI, CCM MLITUSALITI KWA MDA MREFU, SASA BASI, KUTULAZIMISHA NI KUTAFUTA MUHARI.

    ReplyDelete
  23. Maandamano ya chadema yalionekana kuleta fujo sasa je ya CCM ni baraka kutoka kwa Mungu? Ama kweli nyani haoni kundule!!! Acheni kujidhalilisha ndugu zangu wa CCM! Mlipinga kwa nguvu zote maandamano ya Chadema, sasa yenu mnayaona mazuri!! Kisha mnajiita wasomi! kama usomi ndio huu,basi tutafute maana mpya ya usomi!!!Fikirini!!!!

    ReplyDelete
  24. CCM ni chama cha siasa. chama cha siasa kinawezaje kumpeleka mtuhumiwa mahakamani? hiyo ni kazi ya dola,,walaumiwe serikali na watu wake, maana hata watu wa Chadema wamo serikalini ndo mna wanaweza kusema uwongo na wasichukuliwe hatua.

    ReplyDelete
  25. KWA CHENGE, LOWASA NA ROSTOM-KWA VILE MZEE MAKAMBA ANAFURAHI KWAMBA AMETOKA NA WENGI NDANI YA KAMATI KUU, BASI KWA NJIE HAMNA LA KUFAYA NI KUFANYA MCHEZO MMOJA WA KUFA KWA WENGI NI HARUSI, KWA MAANA HIYO KWA VILE CHENGE UNAWAJUWA WATU WOTE MLIOGAWANA MSHIKO WA RADA NA WEWE WAWEKE HADHARANI NAO WATOLEWE NDANI YA CHAMA, PIA MZEE LOWASA KWA VILE UNAWAJUWA WALE WOTE WALIOKUKATIA MSHIKO WA RICHMOND BASI USIKUBALI KUFA PEKE YAKO, WATAJE WOTE NAO WATOLEWE CCM, NA PIA MHESHIMIWA ROSTOM WEWE NDIYO JEMBE, WALIME WOTE UNAOWAJUWA KUWA ULIWAPA MSHIKO ILI KUPITISHA DEAL ZAKO, USIKUBALI KWENDA MWENYEWE, HUONI MAKAMBA, NI LAZIMA UWE SHUJAA USIFE KIVYAKO KUFA NAO WOTE WALIOPOKEA FEDHA KUTOKA KWAKO

    ReplyDelete
  26. Hii ndio CCM naamini ni Chama Cha Siasa na Si Chama Cha SI HASA.wanajua wanacho kifanya.Wanauzoefu wa kushughulikia WAKENGEUFU wa Malengo na IMANI ya chama chao ambao kwa sasa tunawaita MAFISADI. wakati wa chama kimoja walikuwepo pia lakini walishughulikiwa kwa OPERATION maalum kama Azimio La Arusha, Uhujumu wa Uchumi, Fagio la Chuma nk kwa kizazi kile.

    Kwa kizazi hiki cha watu waliojaa ujanjaujanja naamini wanawashughulikia kwa MTINDO maalum. Wakikurupuka tu,hao hao wanaoitwa MAFISADI watahamia kwao na kwa kuwa wamejaaliwa kuupepeta watawasafisha na kwa hakika watakuwa safi wao na mihela yao.

    Imani yangu kuwa MTINDO wa CCM wanaoutumia uko sahihi DELAYING TACTICS ili HAO,WEWE NA MIMI tuwasemeeeeeeeeee Tuwachafuweeeeee Tuwaumbueeeeee na kama ushahidi upo tuendelee kuwaanikaaaaaaaaaa
    wasifae kabisa kabisa si kwa CCM na Kwa WAO hapo lengo la CCM linakamilika bila KUIATHIRI. Halafu sasa mdogomdogo haooooooooooooooooooo

    Mambo ya Shule sio KUKOPI NA KUPESTI baba kuwa mpole HII NDO CCM

    ReplyDelete