MUNICH, Ujerumani
KLABU ya Bayern Munich imemtimua kocha wake, Louis van Gaal mara moja kwa mujibu wa taarifa zilitoka Ujerumani jana.Van Gaal mkataba wake ulikuwa
unaisha mwishoni mwa msimu huu, lakini bodi ya Bayern imeamua kumtimua kocha huyo wa kidachi mwenye umri wa miaka 59, huku zikiwa zimesalia mechi tano kabla ya msimu kuisha.
Klabu hiyo tayari ilikuwa imetangaza kuwa Van Gaal nafasi yake itachukuliwa na kocha wa Bayer Leverkusen, Jupp Heynckes mwishoni mwa msimu, lakini matokeo ya bao 1-1 ugenini dhidi ya Nurnberg Jumamosi yamefanya timu hiyo kuharakisha kumtimua.
Sare hiyo imeifanya Bayern kuwa katika nafasi ya tatu na inataka kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya, wako nafasi ya nne nyuma ya Hannover katika msimamo wa ligi ya Bundesliga huku zikiwa zimesalia mechi tano.
Van Gaal aliiongoza Bayern katika ligi hiyo na kutwaa makombe mawili msimu uliopita, lakini mabingwa hao wa Ujerumeni mara 22 kwa sasa wako nafasi ya nne katika Bundesliga, pointi 14 nyuma ya vinara Borussia Dortmund.
Magazeti ya Bild na Kicker yote yalisema kuwa Bayern imemtimua Van Gaal, kutokana na matokeo ya sare ya bao 1-1, Msaidizi wake Andries Jonker anatarajia kukabidhiwa mikoba kwa kipindi kilichobakia.
Wajumbe wa bodi Karl-Heinz Rummenigge, Uli Hoeness na Karl Hopfner wanaamini walikutana na Mkurugenzi wa Michezo, Christian Nerlingerna kuchukua uamuzi Jumamosi usiku.
Klabu hiyo imefanya vibaya katika mashindano ya ndani msimu huu na na iko katika hatari ya kukosa mashindano ya Ulaya msimu ujao ambayo fainali yake itachezwa Munich.
katika mechi ijayo Bayern, itacheza dhidi ya Leverkusen ikiwa na maana kuwa Heynckes ataiongoza timu hiyo kupigania nafasi ya kuwemo katika mashindano ya Ulaya.
No comments:
Post a Comment