Na Mwajuma Juma, Zanzibar
CHAMA cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA), kimesema kinatarajia kupendekeza nafasi ya Msemaji wa chama hicho na Katibu Msaidizi Unguja, ili
ziwemo katika katiba ya chama chao.
Akizungumza mjini hapa jana Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya ZFA, Mussa Soraga alisema kwamba mwambia mapendekezo hayo yatatolewa katika Mkutano Mkuu wa dharura utakaofanyika wakati wowote kuanzia sasa.
“Nafasi hizi hazimo katika katiba ya chama, lakini katika mkutano huo tunatarajia kupendekeza na kama zitapitishwa zitaingizwa katika katiba yetu,” alisema Soraga.
Alisema mbali na pendekezo hilo, pia wanatarajia kupendekeza kufanyiwa marekebisho kwa Kamati ya Usimamizi ya Uchaguzi, ili iweze kutumika wakati wa uchaguzi pekee na baadaye kuvunjwa.
Mjumbe huyo alisema kwamba Kamati ya Uchaguzi inayotumika hivi sasa imekuwa ikikaa kwa muda mrefu bila ya kufanya kazi, hasa ikizingatiwa kwamba uchaguzi wake hufanyika kila baada ya miaka minne.
“Sasa hivi katiba hiyo inakaa kwa muda wa miaka minne, jambo ambalo imeonekana kuwa inakaa muda mwingi huku uchaguzi ukiwa unafanyika kila baada ya miaka mine,” alisema.
Hata hivyo Mjumbe huyo hakuweza kutaja ni lini mkutano huo utafanyika, lakini alisema kuwa kati ya ajenda watakazozizungumza katika mkutano huo na nafasi hizo nazo zitakuwa miongoni mwa ajenda zao.
No comments:
Post a Comment