14 March 2011

Watatu wauawa katika mapigano ya kikabila

Na Jumbe Ismailly, Singida

WATU watatu wamekufa katika mapambano kati ya Wasukuma na Wabarabaig yanayotokana na kugombea malisho ya mifugo katika Kitongoji cha
Midibwi, Kijiji cha Munguli, kata ya Mwangeza, wilaya ya Iramba, Mkoani Singida.

Habari zilizopatikana kwenye eneo la tukio zinadai kwamba dalili za mapambano hayo zilianza kuonekana siku nne zlizopita, baada ya Wabarabaig kufanya vikao Jumatano na Alhamisi kujadili kitendo cha Wasukama kuvamia malisho yao.

Inadaiwa pia kwamba katika vikao vyao hivyo, jamii hiyo ilifikia uamuzi wa kuwataka wafugaji wa kabila la Kisukuma kuondoa haraka mifugo yao katika eneo la malisho hayo waliyoyavamia.

Kwa mujibu wa habari hizo wafugaji hao wa kabila la Kisukuma waligoma kuondoa mifugo yao ndani ya malisho hayo kwa madai kuwa ardhi hiyo ni mali ya Watanzania wote.

Kitendo hicho kiliwakera watu Wbarabaig wanaosemekana kuwa
walifanya kikao cha dharura na kufikia uamuzi wa kuwatoa Wasukuma kwa nguvu, katua iliyohusiaha silaha za jadi na kusababisha watu watatu kuuawa.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Munguli, Bw. Gemu Maige amewaja watu wanaohofiwa kufariki dunia katika mapambano hayo kuwa ni Tongo Seni, Makaranga Funganya (wote ni wa kabila la Wasukuma) na Mbarabaig mmoja aliyetambulika kwa jina moja tu la Gambeshi.

Kamanda wa Polisi Mkoani Singida, Bi. Celina kaluba alikiri kuwapo kwa tukio hilo na kuwa ametuma watu wake kwenye eneo la tukio na baada ya hapo taarifa angetoa leo.

No comments:

Post a Comment