14 March 2011

Hakuna tishio la tsunami nchini-TMA

Na Fatuma Kitima

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imewataka wananchi wanaoishi katika mwambao wa Bahari ya Hindi kuondoa wasiwasi wa kukumbwa na
hali hiyo, hivyo wanapaswa kuendelea na shughuli zao.

Tamko hilo limekuja baada ya tetemeko la adhi na kimbunga cha Tsuamani kuikumba Japan Machi 9, mwaka huu na kusababisha maafa makubwa kwa kwa wananchi na mali zao, ambapo zaidi ya watu 1,000 wamepoteza maisha.

Akizungumza na waandishi wa habari juzi Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi TMA, Bi. Agnes Kijazi alisema kuwa walipokea taarifa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Japan, kwamba Tsunami kilitokea nchini humo ipo katika latitudo 38.322 Kaskazini na Longitudo 142.369 Mashariki na kusababisha maafa mbalimbali.

"Kutokana na taarifa hizo TMA inafuatilia kwa kina nguvu za mawimbi ya Tsunami yalitokana na tetemeko hilo. Wakati tukiendelea na ufuatiliaji ninawashauri wananchi waendelee kufanya shughuli zao bila wasiwasi wowote," alisema Bi. Agnes.

Aliongeza kuwa katika eneo la Japan katika Bahari ya Pasifiki tsunami inaelekea Kusini Mashariki mwa nchi hiyo katika visiwa vya Caribian hivyo kuondoa hofu ya kusababisha madhara yoyote katika upande wa magharibi mwa Bahari ya Hindi iliyopo Pwani ya Afrika Mashariki hasa Tanzania haitegemewi kutokea.

"Kama ikitokea ongezeko la nguvu madhara hayo yanatarajiwa kuishia Mashariki mwa Bahari ya Hindi ambayo hayawezi kuifikia Tanzania kwa namna yoyote," alisema Bi. Kijazi.

1 comment:

  1. Taarikfa hii haitusaidii, tungepewa usibitisho huu kuwa Tz hatuna tishio la tsunami kabla haijatokea, baada ya forecast. sasa kama ingetokea sanjari na yale ya japan mngewaambia nn watanzania. TMA inapaswakutoa taarifa za hali ya hewa kabla haijatokea na hilo ndo lingekuwa na maaaana na faida kwa watumiaji wa taarifa hizo.

    ReplyDelete