*Asema wamekumbuka shuka asubuhi
Na Elizabeth Mayemba
BAADHI ya wanachama wa Klabu ya Yanga, wamepinga hatua za Makamu Mwenyekiti wake, Davis Mosha kujiuzulu katika wadhifa wake.Juzi Mosha
aliandikia barua kwa Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya kujiuzulu wadhifa wake kwa madai ya kudhalilishwa na kutishiwa maisha na baadhi ya wanachama.
Wakizungumza Dar es Salaam jana baadhi ya wanachama wa klabu hiyo, walisema kwamba wanamuomba Makamu huyo asitishe maamuzi yake ili waweze kuunganisha nguvu na kuisaidia timu yao katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara zilizosalia.
"Bado tunahitaji mchango wa Mosha katika Yanga, tulimchagua kwa kura nyingi sana ambazo hakuna kiongozi yeyote aliyefikia, hivyo tunamuomba arudishe moyo nyuma," alisema Mohammed Kondo mwenye kadi namba 2237.
Alisema kama kuna tatizo lolote wanamuomba Makamu huyo awapelekee kwenye Mkutano Mkuu wa wanachama ili wao walitolee maamuzi, kwani kipindi walichopo kwa sasa ni kigumu mno.
Naye mwanachama mwingine, Soud Tall mwenye kadi namba 2711, alimuomba Mosha asichukue uamuzi huo kwani katiba inamtambua na wapo tayari kufanya lolote ilimradi arudi kwenye wadhifa wake.
Alisema ni kweli Mosha amekuwa akifanyiwa vitendo vingi vya udhalilishaji, ikiwemo kumvunjia kioo cha gari laki, kitendo ambacho hakuna mtu yeyote ambaye anaweza kuvumilia, lakini kwa uamuzi wake huo utawaumiza wengi.
"Mosha ndiye alikuwa tegemeo letu lililobaki, baada ya mdhamini wetu Yusuf Manji kujiondoa sasa kama na yeye ataondoka, tutakuwa katika kipindi kigumu sana," alisema Tall.
Mbali ya wanachama hao, pia wanachama wengine kutoka mikoa ya Morogoro, Iringa na Mbeya, wamepinga kitendo cha Mosha kujiuzulu na kumtaka aendelee kushikilia wadhifa wake na wameiomba Kamati ya Utendaji kumsihi kiongozi huyo asiondoke kwa manufaa ya klabu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Wazee la klabu hiyo, Jabir Katundu alisema wanaisubiri Kamati ya Utendaji itoe tamko lake ndipo na wao waweze kutoa msimamo wao.
"Tumepata nakala ya barua hiyo, kwa sasa tunasubiri Kamati ya Utendaji ikae ndipo na sisi tuseme yetu kwa manufaa ya klabu," alisema Katundu.
Katika hatua nyingine, Msemaji wa klabu hiyo, Louis Sendeu alisema kikao cha Kamati ya Utendaji kilichokuwa kikae jana kwa ajili ya kupitia barua ya Mosha, kimeahirishwa kwa sababu wajumbe wengi hawakuwepo.
Alisema kikao hicho kitapangwa baada ya kolam ya wajumbe kutimia.
Akizungumzia kuhusu kauli hizo, Mosha alisema wanachama hao wamekumbuka shuka asubuhi kwa kuwa tangu mapema walikuwa wakijua kuhusu usumbufu aliokuwa akiupata, lakini hakuna hata mmoja aliyejaribu kuingilia.
"Inashangaza mno, hivu wanadhani ni kwa nini nilikuwa naandamwa peke yangu kwamba ninaihujumu timu wakti kiongozi nilikuwa si mimi peke yangu, ngoja niwaachie Yanga yao waendelee na watu wanaowataka," alisema Mosha.
Davis ni mpiganaji wa maendeleo na kilichopo katika vilabu vyetu ni viongozi wengi wanajali matumbo yao sasa inapotokea mpiganaji yumo kati yao basi ni vita vinakuwa vimeanza..yanga mtamkumbuka Davis kijana mchapa kazi aliyependa kuplant football leadership strategies and not propagandaz...
ReplyDeleteSimba na Yanga za miaka ya sabini na themanini zimeshapitwa na wakati,Wanachama wa hizi timu bado wanamawazo ya kwamba wao ndio wenye timu na anapotokea kiongozi mwenye mawazo endelevu basi huwa adui wa timu.Kwa staili hii ya sasa kwa hizi timu kutakuwa na matatizo mengi sana hasa kwa wafadhili wa hizi timu.
ReplyDeleteIli iwe fundisho kwa wanachama wasiona mbali naona labda wafadhili wote wangekaa mbali na hizi timu japo kwa msimu mmoja tu alafu tuwaone hao wanachama wanao jidai kuwa yanga ni yao au simba ni yao.
Wanatakiwa waendesho hizo timu kwa huo muda kama haujaona timu inashindwa kwenda mkoani wachana na nje ya nchi.Timu kubwa haziendeshwi kwa kutegemea mapato ya mlango peke yake.Lazima kuwe na mipango ya kudumu na yamuda mrefu ya jinsi ya kuendesha hizi timu.Mfano mzuri ni kwa klabu ya yanga.Yanga wana uwanja wao pamoja na jengo kubwa tu lenye vyumba vya kutosha kwa wachezaji sioni sababu ya kwenda kupiga kambi sehamu nyingine ambayo timu inahitajika kuwaweka wachezaji katika hoteli alafu wakati wa malipo inakuwa matatizo na saa nyingine wanaweka basi lao rehani kwa kukosa pesa.
Sasa hivi wanatakiwa kuimarisha uwanja wao wenyewe pamoja na jengo ili kuepukana na matatizo yote hayo,Na hayo yote yatafanyikaje bila ya pesa? na hizo pesa mtazitowa wapi bila ya kuwa na wafadhili wa kuanzisha huo mradi?
Mimi nilishasema toka miaka kumi iliyopita, timu zetu za bongo hatuangalii maendeleo yetu ya mbele, kama miaka mitano au kumi ya baadaye. Mie si shabiki wa timu yoyote bali shabiki wa maendeleo ya mpira Tanzania. Timu kubwa kama Simba na Yanga nilishasema inabidi zibadilike kuwa kama kampuni au ziwe na vitega uchumi, mfano Simba wanajengo, wangelitengeneza liwe kama hotel. Haya mambo yamewakuta ata timu kubwa kama Man.United, ndiyo kisa cha kununuliwa na Mmarekani ingawa mashabiki wao walikuwa wanagoma,lakini hela inaongea. Timu zinatakiwa kuwa miradi fulani, kama mashamba, maduka, mabasi, viwanda,etc kuwaletea pesa. Mashabiki wengi hawajui nini kinafanyika mpaka timu inatua uwanjani. Vile vile viongozi inabidi wawe waaminifu na kuwafundisha mashabiki nini kinaendelea.
ReplyDelete