Na Benjamin Masese
TAARIFA za walimu wa Shule ya Msingi Buguruni Kisiwani kudaiwa kugoma kufundisha zimeishtua Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na kutuma ujumbe
kufanya mahojiano na uongozi wa shule hiyo kwa zaidi ya saa tano.
Vyombo vya habari jana viliripoti kuwa walimu hao wamepanga kugoma kutokana na mwalimu mwenzao, Bi. Rosemary Haule kushikiliwa na polisi kwa madai ya kumjeruhi mwanafunzi.
Maofisa wa wizara hiyo wakiongozana na Ofisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na wakaguzi wa elimu wilaya na viongozi wengine wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala walijumuika katika kikao hicho cha kutafuta ukweli wa taarifa hizo.
Baada ya kikao hicho kumalizika Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Bw. Wilfred Luyagaza aliwasindikiza maofisa hao kuondoka, huku walimu wengine wakiwa katika ofisi yao wakilalamikia kutohusishwa katika kikao hicho.
Mwalimu mmoja wa kike aliuliza sababu za wao kutoshirikishwa katika kikao hicho lakini ombi lake halikutiliwa maanani, kwani maofisa hao waliondoka bila kumpatia majibu.
Hata hivyo, kabla ya maofisa hao kuondoka, Bw. Luyagaza alizungumza na waandishi wa habari na kukana kuwepo kwa mgomo na kusema kuwa kwamba walisitisha masomo kwa muda kufanya kikao cha kutafuta namna ya Bi. Haule kupata dhamana.
Alisema kuwa tatizo kubwa lililopo hapo ni mwalimu mwenzao kukosa dhamana mahakamani na ndio sababu waliamua kusitisha vipindi kufanya kikao.
Akisimulia mkasa huo, alisema Mwalimu Haule alimwadhibu mwanafunzi wake aliyemtaja kwa jina moja la Hamisi wa darasa la nne.
Alisema kwa mujibu wa maelezo yaliyoyapata, Mwalimu Haule alimfinya shavu mwanafunzi huyo aliyekuwa anaumwa ugonjwa wa macho na kumsababishia maumivu makali, na hadi sasa hajarejea shuleni hapo.
Wakati anaendelea kufafanua na kujibu maswali yaliyokuwa yakiulizwa na waandishi, ghafla ofisa mmoja wa wizara alimzuia Bw. Luyagaza na kumwambia kwamba hatakiwi kuelezea suala hilo kwa undani kwa kuwa bado linafanyiwa kazi na wizara.
Ofisa huyo aliwataka waandishi wa habari kutoendelea kuuliza maswali mengine juu ya suala hilo ili kumpa nafasi ya kuendelea kulifanyia kazi kama alivyoaagizwa na wizara.
"Samahani mwalimu naomba uishie hapo suala hilo bado linafanyiwa uchunguzi na ndio maana nimeagizwa na wizara kuja hapa, na nyie waandishi naomba msiendelee kuuliza maswali zaidi nendeni polisi Kituo cha Buguruni ndio kuna maelezo yote juu ya mtuhumiwa huyo," alisema.
Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo (majina yamehifadhiwa) walisema kuwa juzi walimu hawakuingia darasani bali walikuwa katika ofisi zao hadi waliporuhusiwa kwenda nyumbani muda wa saa nane lakini jana walionekana madarasani.
ASKOFU Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amesema viongozi ndani ya Serikali, wamekuwa wakitenda mambo mengi mabaya dhidi ya wananchi na kuficha uozo wao kwa gharama yoyote.
ReplyDelete“Simameni daima katika ukweli; liwalo na liwe. Ukiogopa kufa leo utakufa kesho. Ukiogopa kusema ukweli leo eti ...kwa kuogopa kufa utakufa kesho,” aliasa watanzania Kadinali Pengo, kweli tumechoka tunataka mabadiliko.