25 March 2011

UWT yafuata nyayo za Umoja wa vijana

*Yaonya wanaokosoa CCM hadharani

Na Grace Michael

BARAZA Kuu la Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT), limewaonya baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao wameanza
kujipanga na kuweka mikakati binafsi ya kuwania nafasi ya urais 2015 kwa kuwa jambo hilo ni hatari kwa chama.

Mbali na hilo, pia UWT imeonya tabia ya baadhi ya viongozi wa chama na serikali kukemeana hadharani na kwenye majukwaa kwa kutafuta umaarufu wa kisiasa badala ya kutumia vikao sahihi vya chama.

Hayo yanatokana na maazimio ya kikao cha Baraza Kuu ambalo lilikutana Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo lilijadili mambo mbalimbali likiwemo la kutathimini changamoto zilizokikabili chama katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana.

Hivi katibuni, Umoja wa Vijana wa CCM ulifanya kikao cha Baraza Kuu mkoani Dodoma na kutoa maazimio mbalimbali, likiwamo la kuwakemea na kuwatisha wanachama wa CCM wanaokikosoa hadharani badala ya kwenye vikao, na kuweka bayana kuwa chama kisiwateue kuwania nyadhifa mbalimbali baadaye.

Akizungumza na Majira, Katibu Mkuu wa UWT, Bi. Amina Makilagi alisema mbali na kukemea tabia hiyo, pia jumuiya hiyo imewataka wanachama wote wa CCM kurejea utamaduni wa kujitolea kwa moyo ndani ya chama na kuachana na tabia iliyojengeka miongoni mwa wanachama wake ya kudai malipo wakati wa shughuli za kujenga chama.

Pia UWT iliazimia suala la kuimarisha uhai wake na wa CCM kwa ujumla ambapo iliwahimiza wanachama kuendelea kuimarisha uhai wa jumuiya na chama kwa kuingiza wanachama wapya na kulipa ada kwa mujibu wa katiba na pia iliazimia kuandaa mpango utakaowajengea wanawake uwezo wa kuchangia maoni katika mabadiliko ya katiba ya nchi yanayotarajiwa kufanyika.

“Mbali na hayo, UWT na chama ni lazima viendelee kujiimarisha kiuchumi kwa kuboresha rasilimali na miradi yake ili kuondokana na tabia ya utegemezi...na katika kujiimarisha zaidi UWT itaweka utaratibu maalumu wenye msingi thabiti wa kuajiri kulingana na mahitaji ya soko la sasa la ajira na kwa kuzingatia maendeleo ya sayansi na teknolojia,” alisema Bi. Makilagi.

Katika suala la kulinda amani na utulivu, baraza hilo lilivitaka vyama vya siasa kuepuka kutumia vibaya fursa na haki za sheria ya vyama vya siasa kufanya maandamano na kuendesha mikutano kwa nia ya kueneza siasa za uchochezi na chuki miongoni mwa wananchi kwa lengo la kuwahamasisha wananchi kuichukia serikali yao.

“Kwa upande wa wanawake, baraza liliwataka kuepukana na siasa za uchochezi zinazoenezwa na CHADEMA kwani zinawagawa wananchi kisiasa na kiitikadi badala yake wajizatiti kufanya kazi za kujiletea maendeleo,” alisema Bi. Makilagi.

Akizungumzia ilani ya CCM, aliitaka serikali kuendelea kuboresha sekondari za kata kwa kuwa zimepanua fursa ya kupata elimu kwa watoto wengi wa kike na pia kupunguza kwa kiwango kikubwa tatizo la mimba za utotoni.

Wakati akifungua kikao cha baraza hilo Mwenyekiti wa UWT, Bi. Sophia Simba aliwataka wanawake kuvunja ukimya kwa kujibu mapigo yanayoelekezwa kwa CCM na vyama vya upinzani kwa kuwa siasa zimebadilika kwa kiasi kikubwa.

12 comments:

  1. HAYA BWANA NYIE BILA KUTAJA CHADEMA NAFIKIRI KWA DUNIA YA LEO HUJAONGELEA SIASA, TUTAANDAMANA MPAKA MATAKWA YETU YATIMIZWE NA MKIYATIMIZA TUTAANDAMANA TENA KUWAPONGEZA
    KAMA MWENYEKITI WAKO MWISHO WA MWEZI ULIOPITA ALIWAASA WATU WASISHIRIKI HAYO MAANDAMANO LAKINI WATU WALIOJITOKEZA KESHO YAKE NI WENGI MPKA MWENYEKITI WA CCM WA MKOA WA KAGERA TULIKUWA NAYE , KAMA UNATAKA PICHA SEMA NIKUTUMIA SEMBUSE WEWE SISIMIZI MDOGO KATKA SIASA ZA TANZANIA NA KUUWADI WA MAFISAD

    ReplyDelete
  2. chadema lzm watajwa sababu ni wadini na wakabila kabila hama gani kina wachaga watupu?

    ReplyDelete
  3. Mchangiaji Na. 2 vipi huyo? Nadhani hana akili timamu hata chembe. Kuna suala la udini au ukabila hapa kama huna la kuchangia si ukae kimya tu jamani. Mbona I-Q za watu wengine zina matatizo tuwasaidieje? Hawa UWT hawana jipya kwani tunawajua wamama hawa wengine ni nyumba ndogo za vigogo kwa hiyo lazima wapalilie unga wao ni sawa tu na hao UVCCM tunajua kabisa mafisadi wanaowatumia Umoja wa Vijana kwa hiyo jumuiya zote hizi mbili hawana lolote wanatumiwa na mafisadi. CHADEMA CHADEMA CHADEMA kila siku nyie kweli hamjui kusona alama za nyakati mnawapandisha hawa bila nyie kujijua maanake inaelekea mna hofu sana nao.
    Zungumzeni mambo ya muhimu kwa watanzania yenye manufaa

    ReplyDelete
  4. Bahati mbaya viongozi wa jumuia hizi mbili UWT na UVCCM hawajui kwamba kimuundo zimebaki na viongozi tu lakini hazina wanachama kwani zilisha poteza mvuto siku nyingi. Kama hawaamini wajaribu kuiitisha mikutano ya hadhara bila kugawa rushwa waone mahudhurio yake.

    ReplyDelete
  5. Mmm! Nadhani huu uitwe UWD kwani ni kinamama wa DSM tu.Kijijini siku hizi hakuna mama anayejua UWT kama ilivyokuwa zamani! Wanashindwa kujadili namna bora ya kuwatoa akinamama katika wimbi la umasikini kwa kuhakikisha wanawake wote wanapata ngaa mikopo midogomidogo na kuwaelimisha njia bora ya ujasiriamali. Instead wanaitatana ili kupaza sauti kukishutumu CHADEMA kwanini wanawaamsha Watanzania kujua haki zao za msingi. Nadhani wangetumia muda mwingi kubuni njia za kuwasaidia akinamama wote kuanzia ngazi ya kijiji ili kuleta tija na kwavyovyote wangeamsha ari mpya kwa akinamama kurudisha imani kwa sisiem iliyooza badala ya malumbano ambayo yanazidi kukibomoa.

    ReplyDelete
  6. mh!!!!!!!!!!!!!!!!! siasa zitatumaliza kila pakikucha CHADEMA badala ya kujadili mambo yanayleta maaendeleo kwa wananchi tunaelekea wapi????????????????nauliza hata nyie wanawake kweli hekima ni kitu bora sana

    ReplyDelete
  7. ukiona hivyo jua chadema ikojuu na inawakosesha mafisadi usingizi, mm nasema keep it up chadema msiogope mtu fichueni maovu ilimradi msivunje sheria za nchi elimisheni wananchi ipasavyo kwni japo wanawaita waahini, ilamatundayenu tunayaona bei zimeanza kushuka na mjomba(kikwete) ameanzakuwajibika utazani si yeye, kumbealikuwa anafanyakusudi mm nlizani hana uwezo safi sana chadema na mshindwe wote mlio nania ya kuwazima

    ReplyDelete
  8. Udini ndani ya CHADEMA?Nani mdini CHADEMA na CCM jamani?Rais wa TZ Jakaya Mrisho Kikwete(Muislam),Makamu wa Rais Dr Bilal(Muislam),Rais wa ZNZ Dr Shein(Mwislam)Makamu wake Balozi Seif Idd na Maalim Seif(wote waislam),Katibu Mkuu CCM Yusuf Makamba(Muslam)Katibu Mkuu CCM-ZNZ Mzee Ferouz(Muislam)Jaka Mwambi(Makamu Katibu Mkuu cc-bara)muislam pia!

    ReplyDelete
  9. Kwenda kwa Mkurugenzi Manispaa ya Ilala.
    Ufisadi huu hadi lini Ofsi ya Maji Ilala.
    Inashangaza kuwa watu wachache ndio wanaokula pesa kizembe tu ofsi ya maji ikiongozwa na Fisadi namba moja Selestina Magesa, na group lake Opitaty Kwembe mtu alie na darasa la kwanza ila wizi anaujua kupta mtu yeyote, pamoja na Wilfred Kavishe, Alex Odena, na Kahema amekuja ofsi ya maji kuja kuiba vzr pesa za miradi ya maji maana kahema na Optaty kwembe ni mahawara waliobobea! Mkurugenzi tunapenda kukutaarifu kuwa pesa ya wiki ya maji haijafaya kazi yoyote kwani baadhi ya madiwani walichoshwa na upuuzi wa viongozi hawa wa ofis ya maji na kususia uzinduzi wa wiki ya maji visima havina ubora na pia miradi mingi ni hewa tunakuomba utoe samaki wabovu ofisi ya maji ili ili kuwasaidia warengwa wa miradi husika. Tunashangaa kuona kuwa huyu kahema kaja kinyemera ofisi ya maji kisa ni mpenzi wa Optaty kwembe tunashangaa pia kuona kisima cha depot kuchimbwa kwa miliion 9 badala ya million 5, na kisima hakina ubora wa utoaji maji ya kutosha pia watumishi hapo depot bwanakosa maji vyooni na hakuna anaelishughulikia swala hili.
    TUTAENDELEA KUKUPA TAARIFA ZAIDI KUHUSU UOZO WAO NA TUNAOMBA UWAKALISHE NA KUWATIMUA IKIBIDI KWANI HAWANA NIA NZURI NA MATAKWA YA SERIKALI ZAIDI YA KUJINUFAISHA WAO TU.

    ReplyDelete
  10. UWT. - Baraza Kuu la Wanawake Tanzania. Tunapenda kutoa ushauri kupitia Mhariri wa gazeti hili, kufikisha ujumbe kwa wahusika ( Waziri anayehusika na masuala ya wanawake pia Raisi ) waelewe kwamba umoja huo ufanyiwe marekebisho. Baraza la Wanawake Tanzania haliwezi kuwa la watu wa CCM tu kisha likapewa baraka za kuwa Baraza Kuu la Wanawake Tanzania. Kutakuwa na makosa mahali yanafanyika huwenda ni makusudi tena kupitia katika gazeti la Serikali ambalo ni mali ya walipakodi wananchi wote bila kujali vyama vyao. Hapa ndugu Mhariri wa gazeti hili la Majira jirekebisheni kwa upotoshaji huo. SIYO WANAWAKE WOTE TANZANIA NI CCM. Tafadhali zingatieni hili. Naomba maelezo kutoka kwako.

    ReplyDelete
  11. WATANZANIA WANA TATIZO LA UWEZO MDOGO WA FIKRA, UBINAFSI, NA KUTOKWA NA VALUES (MAADILI) YANAYOFUATWA NA WOTE. CHAMA AU KIKUNDI CHA WATU WANAPOKOSOA WENGINE KUWA WANAKOSEA KUTUMIA NJIA 'A'KUTATUA KERO AU KUSEMA NA UMMA, NA WAO WAKATI HUO HUO WANATUMIA NJIA HIYOHIYO, NI DALILI YA KUCHANGANYIKIWA AU KUKOSA FIKRA. MARA NYINGI WATU WAMEKOSOA WANAOANDAMANA WAKATI WAO PIA WAKITUMIA MAANDAMANO. WENGINE WANAKOSOA WANAOTUMIA MAGAZETI KUKOSOA CHAMA WAKATI WAO NAO WANATUMIA NJIA HIYO HIYO. UTAONA WENGINE WANAKOSOA WENZAO KUWA WANAKOSEA WANAPOZUNGUMZA NJE YA VIKAO VYA CHAMA WAKATI WAO WANATUMIA NJIA HIYOHIYO KUKOSOA WALE WENGINE. WANAOJARIBU KUFANYA SIASA WANAAMBIWA WANA UCHU WA MADARAKA, HUYO ANAYEMSEMA MWEZIWE ANA UCHU NAYE PIA ANA UCHU. TUACHE UJINGA HUU WA KITOTO.THIS IS CHILDISH. WATU WASEME HOJA ZINAZOWAKERA: KAMA WANAKERWA NA KUKOSOLEWA WASEME. KAMA WANAKERWA KWA KUAMBIWA UKWELI MACHONI WASEME. MBONA WANAPOSIFIWA NJE YA VIKAO HAWALALAMIKI; MBONA WANAPOSIFIWA KUPITIA MAGAZETI HAWALALAMIKI; MBONA WANOANDAMANA KUSIFIA WATAWALA AU CHAMA HAWALALAMIKIWI WALA KUSHITAKIWA KUVUNJA AMANI? MBONA MDUNDIKO, HARUSI, MAZISHI, NA MICHEZO INAZOA WAANDAMANAJI WENGI TENA WASIOOMBA KIBALI POPOTE? UTAAONA TATIZO NI KUWA KUNA MASULTANI WACHAHCHE HAWATAKI KUKOSOLEWA, WALA KUAMBIWA UDHAIFU WAO WAZIWAZI - HATA KAMA NI KWELI WANACHOAMBIWA. HILO NDIO TATIZO. WAKIKOSOLEWA WANAKIMBILIA OOH KUVUNJA AMANI, OOH UCHONGANISHI. SHAME ON YOU!! WATANZANIA TUJIFUNZE KUKUBALI KUKOSOANA KILA WAKATI ILI TUPIGE HATUA ZA MAENDELEO. UNAFIKI NA USANII HAUTALETA TIJA NCHINI BALI UMASIKINI TU.

    ReplyDelete
  12. mchangiaji wa pili alinikera sana! mimi nafikiri hafai kuishi katika ulimwegu wa leo! akili gani hii ya kiuuzi kuita chadema ni chama cha udini na ukabila tena ukitaja moja kwa moja kabila fulani! wewe ndio mkabila wa kwanza!!! Fikiri kabla hujatenda!! kama huwezi kuandika cha maana acha, si lazima kuandika!!

    ReplyDelete