14 March 2011

UVCCM wataka kumtimua Makamba

*Wamo pia Membe, Chiligati na Makala
*Yadai wameshindwa kumshauri mwenyekiti


Na Edmund Mihale, Bagamoyo

UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umeitaka sekretarieti ya chama hicho kujizulu kabla umoja huo
haujachukua hatua za kuwaondoa kwa kuwa imeshindwa kumsaidia Rais Jakaya Kikwete.

Akifungua Baraza la Umoja wa Vijana Mkoa wa Pwani jana, Makamu Mwenyekiti wa umoja huo wa mkoani humo, Bw. Abdallah Ulega alisema kuwa sekretaeti hiyo haifai kwa kuwa ilisababisha chama hicho kushinda kwa taabu katika uchaguzi mkuu uliopita.

"Katika uchaguzi uliopita tulishinda kwa kupata asilimia 61  ya kura zilizopigwa ukilinganisha na mwaka 2005, ukijiuliza ni kweli CCM imepoteza imani kwa wananchi kwa kiasi hicho jibu linakuja kuwa sekretarieti haikuwajibika ipasavyo, hivyo tunasema kama wamechoka waondoke kama hawataondoka lazima waondolewe hawafai," alisema Bw Ulega. 

Alisema kuwa watu walimo katika sekretarieti hiyo ndiyo wanatoa siri kwa Chama cha Demkrasia na Maendeleo (CHADEMA) na imeshindwa kumshauri na kumtetea rais katika mambo mengi ya msingi hadi anaposimama na kujitetea mwenyewe.

Mkutano huo ulihudhuliwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa na wenyeviti umoja huo kutoka katika Mikoa ya Kagera, Lindi Kigoma, wabunge kadhaa na Mjumbe wa Baraza la Utekelezaji la jumuiya hiyo, Bw. Ridhiwan Kikwete.

Secreterieti inayoongozwa na Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusuf Makamba, inajumuisha Manaibu Katibu Wakuu Bara, Kapteni George Mkuchika na Salehe Ramadhani Ferouz (Zanzibar), Katibu wa Itikadi na Uenenezi, Kapteni John Chiligati, Katibu wa Idara ya Uchumi na Fedha, Bw. Amos Makala na Katibu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe.

Mbalio na sekreterieti hiyo, Bw. Ulega alisema kuwa watu wengi walio katika serikali wanatakiwa kujibu hoja za dhidi ya serikali akutokana na vitengo vyao na si lazima wasubiri Rais Kikwete kujibu hoja hizo.

"Kuna watu wa kujibu hoja, katika mfumuko wa bei yuko gavana na watu wa kumsaidia amewekewa, kuna naibu gavana na wakurugenzi wengine, shughuli yake ni kujibu hoja ya mfumuko wa bei lakini anainuka rais na kujibu hoja hiyo wao wanafanya nini.

"Labda watuambie kama wanamilikiwa na bwana wengine na kumuacha rais akihangaika pekee yake, naomba niseme tena bila kumung'unya, kama wanahisi hawezi kazi wakae pembeni  na kama wanatumukia mabwana wawili watachanika msamba," alisema Bw. Ulega.

Alisema ni kitendo cha kushangaza kwa Mawaziri Wakuu Wastaafu, Bw. Edward Lowassa na Bw. Fredrick Sumaye kushindwa kukutana na rais na kumpa ushauri, na kukimblia katika magazeti na kutoa shutma.

"Hawa watu ni mwaziri wakuu wastaafu, wanaweza kufanya ahadi kwa dakika 30 tu wakaonana na rais lakini wanakimbilia katika magazeti na kutoa kauli zinazohatarisha amani na kukivuruga chama," alisema.

Alisema Bw. Lowassa ni Waziri Mkuu mstaafu, mbunge na mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa, alipaswa kuwa mwangalifu katika kauli zake anazotoa hususani kutaka mishahara ipande huku akijua kuwa hali ya uchumi si nzuri.

Bw. Ulega alisema kauli hizo zimelenga kutaka urais mwaka 2015, jambo ambalo kwa sasa wamechelewa kwa kuwa liko mikononi mwa mwenyekiti wa chama, Rais Jakaya Kikwete kuwa kuwa ndiye anayemjua rais wa 2015.

Alisema viongozi hao wameacha utaratibu mzuri wa chama hicho kutoa maoni yao kupitia vikao na kutoa shutuma zao kupitia magazeti wakidhani wanakikomoa chama, nchi itaendelea kusonga mbele na kuwapa pole wale wanaodhani rais lazima atoke kaskazini.

"Kama wanataka urais wasubiri muda wachuke fomu na kuwashawishi wajumbe wawachague lakini kwa kumtukana mwenyekiti hawatapata kamwe kwa kuwa yeye ndiye anayejua ni nani muadilifu, hivyo wasiharibu nchi kwa maslahi yao. Wao wameshiba na sasa wamevimbiwa watauache na sisi tule kama wao.

"Mimi nasema hapa simung'unyi maneno tuziogope sana fedha zao, mimi sijala hata shilingi moja ya mtu na sihitaji kufanya hivyo," alisema.

34 comments:

  1. UVCCM ndo kawaida yenukukurupika na kutoa vijineno vya kujikosha, baada ya hapo mkikaa na hao hao wakubwa mnafyata mkia kama mbwa mwizi.

    You are never proactive- you are a plainly reactive arm of the party.You never assist the gorvernment, the party, or the country at large.

    ReplyDelete
  2. ulega unaota, au umelewa mvinjo wa CCM kama hauna ajenda basi una lako jambo....una maana gani kusema kuwa "Rais Kikwete ndiye anayemjua Rais wa 2015"... ina maana unakubali kikwete wako akimchagua Lidhiwani awe Rais? au Rostam? au Rowasa? kipofu wewe kaa kimya

    ReplyDelete
  3. huwezi kusema hali ya uchumi Tanzania ni mbaya wakati Wabunge wanagawana mamilioni ya pesa eti kwa ajili ya kununulia magari wakati wafanyakazi mishahara wanayopewa hata nusu mwezi hautoshi kila siku ni kulia njaa tu.

    ReplyDelete
  4. huyu dogo kweli ni ahmada mlevi. angalijua kuwa matatizo ya nchi hii yanasababishwa na watu wachache asingewalaumu watendaji wa serekali na mawaziri wastaafu kuwa hawamsaidii raisi. kimsingi kila mtu anatakiwa kuubeba mzigo wake wenyewe.hata watendaji wa serekali wenyewe wamechoka sasa.

    ReplyDelete
  5. Hii migongano ya Ulega na Lowasa, Sumaye, ukichanganya na kauli za kukurupuka za Sophia Simba na Membe ni dalili tosha kwamba SIKU ZA MWISHO KWA C.C.M. ZIMEFIKA.

    SISI WANANCHI YETU MACHO TU, TWASUBIRI KUONA MWISHO MBAYA WA CHAMA HICHO.

    KWANI KIMESABABISHA UCHUMI KUYUMBA KWA MUDA MREFU NA KIMESHINDWA KULETA MATUMAINI MAPYA KWA WATANZANIA NA SASA WANAGOMBANA WAO KWA WAO. KWISHA HABARI YENU.

    ReplyDelete
  6. mijitu mingine bwana? Ikikosa hoja huja na ukaskazini, kusini, udini, uhaini nk. Ulega ushindwe na ulegee, huna akili kabisa nyamaza!

    ReplyDelete
  7. Haya, huyu Bwana Ulega amefungua box na tumejua yaliyomo, CCM si tu kunafukuta bali wanategana! Hizo ndizo za Mafisadi wako kama Mbwa mwitu wanakula halafu aliyechafuka damu zaidi wanamtafuna! Kiketwe nchi na chama vilishamshinda siku nyingi! Hizi kelele za Ulega ni mwangi tu!

    ReplyDelete
  8. Enyi wa TZ acheni siasa za udini,ukabila na ukasumba.jueni hivi vyote havina nafasi katika kujenga nchi na athari zake ni kubwa sana.hebu leo angalieni amani inavyotoweka na kuirudisha inakuwa shida kwa baadhi ya nchi,nyie huko mpo na kila kitu kwa nini hamkai chini mkapanga mipango yenu ya maendeleo!kama chama kinachoongoza ni kibaya au watu wake ni wabaya basi msubiri mpaka 2015 muwapige chini.ni aibu kubwa kwa nchi kama hio kuomba misaada mpaka leo au nyie hamjioni!nyie mlitakiwa kusaidia nchi nyingine na si kusaidiwa kutokana na vitu vingi MUNGU alivyokupeni.mkitaka muendelee haraka kwanza undeni serikali ya umoja wa kitaifa,pili udini na ukabila visipewe nafasi na tatu hio amani mliyonayo muilinde kwa gharama zozote zile bila amani hakuna maendeleo.

    ReplyDelete
  9. safi sana UVCCM, wasaidieni wtz kupigilia msumari wa mwisho ktk jeneza la ccm. safi sana!

    ReplyDelete
  10. nchi yetu viongozi wote ni wezi. majuzi hapa nilikuwa ushirombo/Bukombe, taarifa za kule zinasema Rostam na Ridhiwan kikwete wana hisa katika mgodi usiorasmi unaoendeshwa na kampuni ya Tancan mining, nimeuita usiorasmi kwa vile serikali haitangazi kuwa tuna mgodi mwingine mdogo kwenye hifadhi ya kigosi.

    Halafu Ridhiwan huwa anaenda siku moja moja night kubeba mzigo. kuna uwezekano kikwete ndio mwenye hisa ila ana mtumia mwanaye ili watu wasimtuhumu yeye.

    ReplyDelete
  11. Kwa UVCCM hongereni kwa tamko lakini je lina nguvu? Kuna mnoja wetu alivyoandika hapo juu kuwa mtafyata mkia mkiwa na wakubwa wenu wa chama, ni Ukweli mtupu! Mara ngapi mmepiga kelele na kuishia kimya kimya? sijui mnapewa kitu kidogo? Lakini pia nyie UVCCM ni kichekesho kuona mnapiga piga kelele eti mtawapiga chini viongozi wa sekretarieti ya chama? kweli? ubavu mnao? Kama chama chenu na watu wengine wanawalaumu CHADEMA eti wanaleta machafuko; nanyi je mtakuwa wapi? hamtaonekana mna uroho wa madaraka na mnaleta machafuko CCM na kisha kwa wananchi? Mtajiondoaje katika lawama hii ya fujo na kuharibu amani ambayo mnawalaumu wenzenu wa CHADEMA? Kazi kwenu na chama chenu!!!!!

    ReplyDelete
  12. CCM NI MATAPERI WAKUBWA MNAANZA KUTOA SIRI .MOJA MFANYE MAANDAMANO YA KUWATOA WALE WOTE WALIOSHIRIKIA KUTUTAPERI SISI WATANZANIA RICHMOND ROWASA NA ROSTAM NA WENGINEO .MUANZE MAANDAMANO YA KUWATOA WARUDISHE KADI ZA CCM ILI KUIKOA CCM CHAMA CHA MAJAMBAZI

    ReplyDelete
  13. Ulega anasema Sekretariati imekula mno, sasa ni wakati wab wao UVCCM kula. Kumbe, huyu Ulega anaona anachelewa naye kufilisi mali ya watanzania! Huyu ni fisadi mtarajiwa! Kama mna uchungu ya watanzania, ondokeni huko CCM. Mnangoja nini? Mwl. Nyerere alisema CCM inanuka ufisadi. Je, mnapenda kukaa kwenye dampo hilo? Subirini tsunami ya democrasia inayoendelea Afrikla!

    ReplyDelete
  14. ccm kushineeeee!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!serikali gani isiyokuwa na tamko la pamoja , kila kiongozi anatamka avyoona , huku kupingana katika matamko kunashiria nini ndani ya chama tawala? viongozi wastafu msiwazurie jambo, acha wapumzike, hii serikali ya mafisadi acha izame yenyewe , msitafute mchawi, wachawi mnao wenyewe humohumo ndani ya club yenu,. UVCCM ni wanafiki wakubwa, ndiyo maana ulega anasema anataka na yeye kula, hivyo miiko ya ccm ni kuila nchi hii hadi tone la mwisho! mshindwe na mkakamae kama si kulegea.

    ReplyDelete
  15. NCHI HII TUMEBADILIKA SANA SIKU HIZI MANENO MENGI LAKINI VITENDO HAKUNA. NA WALE WANATAKA KUFANYA VITENDO VYA MAENDELEO KWA AJILI YA WANYONGE WANATAFUTIWA DAWA YA KUTULIZWA. AMINI USIAMINI, USISHANGAE LAWAMA NYINGI KUHAMIA KWA MAGUFULI NA TIBAIJUKA.

    ULAJI WA MALI YA WATANZANIA KWA VIGOGO NDIYO SERA YA MAENDELEO. KAMPUNI ZOTE ZINAZOPATA MIRADI MIKUBWA SASA HIVI NCHINI KUNA KIGOGO KATIKATI AU NYUMA YAKE.

    UBINAFSI - HAUKO CCM TU HATA VYAMA VYA UPINZANI. NA HUO NI UDHAIFU MKUBWA, NI KAMA SIMBA ALIYEKULA DAMU YA MTU, HAWEZI KUACHA. AMANI BADO IPO, LAKINI UMOJA HAUPO NA WAPINZANI WAMETHIBITISHA KUWA HAWAWEZI KUUNGANA HADI CCM WAMALIZE RASILMALI ZOOOTE, MADINI, GAS, ARDHI.

    ReplyDelete
  16. ULEGA AMEKUSUDIA KUANZISHA VITA NA MAWAZIRI WAKUU WASTAAFU. AMETUMWA NA PENGINE AMELAZIMISHWA KUYASEMA MBELE YA RIDHIWANI KAMA USHAHIDI KWAMBA YAMEFIKA. TUSUBIRI TUONE KAMA WAZEE HAWA WAWILI WATAINGIA VITANI KUPAMBANA NA KIVULI WASICHOJUA NI CHA NANI. LABDA SIO LOWASA NINAYEMJUA MIMI. MTU MSAFI ASIYEKUWA NA DOA LEO HII ANASINGIZIWA ETI KISA URAI 2015??????? WAPI ALISHATAMKA NAUTAKA URAIS??????

    ReplyDelete
  17. Yangu macho, Hivi ccm kila mtu ni mtoa tamko waache wazee watoe ushauri wao.Mnadai wafate taratibu tatizo hakuna wa kumsikilza mwenzake nyie wazee endeleeni kuwambia labda siku moja watakujasikia watakapo kuwa nje ya madaraka

    mungu ibariki tanzania

    ReplyDelete
  18. Yaani wewe uliyeandika hapo juu kumtetea L umenithibitisha kitu kimoja. Huoni wala husikii, wala hutaki mafisadi waonewe bali waendelee kuwa juu, juu juu zaidi. Nakuomba uwatetee na wengine ili tuwafahamu. Usimsahau na Bosi wao.

    ReplyDelete
  19. watanzania wasio taka mabadiriko ni wezi na wanyonyaji wa watu wengine haki huja kwa kuidai kamwe haki haiombwi

    ReplyDelete
  20. bw Ulega, IQ yako iko chini ya kiwango, yote uliyosema ni utumbo. Wala hufai kwa kingozi hata wa nyumba kumi sababu huna quality ya uongozi

    ReplyDelete
  21. Uongozi si lelemama jamani, hasa kwa watu wanaoamka. Nawaombea kila la heri wale wote walio katika nafasi yoyote ya uongozi. Mungu awajalie neema ya kutumikia wananchi kwa uadilifu, pasipo ubinafsi, chuki, unafiki, kisasi, kujinufaisha nk.

    ReplyDelete
  22. eng.mwakapango,E.PAMarch 14, 2011 at 10:06 PM

    umoja wa vijana wa CCM wana kazi kubwa sana. wanapojaribu kushindana na wakubwa zao kwenye hadhara ni tatizo la kimaadili. kunatofauti gani kati yao na akina sumaye na lowasa kilekile walichosema ndicho vijana wanakisema. mimi nadhani tufike wakati watu wafanye kazi tuache longolongo. tupende tusipende Rais ndiye aliyesababisha yote haya. Rais anatakiwa asiwe legelege ili kuweza kuhimili mikikimikiki ya utawala ya wakati huu. CCM iamuke kujibu hoja za wapinzani. UVCCM endeleeni kujifunza siasa sawa vijana! lakini naomba niwafagilie kwa kutumwagia changa la macho.

    ReplyDelete
  23. Huyu Ulega ni mjinga kabisa! Dhambi yake kubwa ni ubaguzi, ameanza na ubaguzi wa ukanda na atakuja na ubaguzi wa udini na baada ya hapo ukabila! Hivi kweli Kikwete bila Lowasa na Rostam angelikuwa Rais wa Tanzania? Ufisadi uliopo leo Tanzania ni matokeo ya ubia wa mtandao wa mafisadi na Kikwete. Yaani huyu bwana mdogo hajui hilo? Leo tena anatuambia rais ajaye anajulikana na Kikwete! Je yeye Kikwete ni Dictor hata ajue kabisa nani atakuwa rais wa Tanzania? Tujuavyo watu hupiga kura na kura huanzia kwenye chama. Mkapa alipenda kabisa Salim Ahmed Salim awe rais lakini alishindwa kwenye kura za chama kwa ajili ya mtandao wa mafisadi CCM na Mkapa akashindwa kumweka Salim kuwa rais wa Tanzania. Sasa utasemaje Kikwete anamjua rais ajaye Tanzania? Ulega watanzania wa sasa ni watu waliosoma wanajua sana kikundi kinachokutumia kwa ajili ya kuhakikisha rais anatoka kwenye mtandao ule ule. Umepewa fedha za mafisadi ili uwashambulie wale wanahohisiwa watagombea urais. Kwa taarifa yako urais ni haki ya kila mtanzania si mali ya kikundi fulani. Na ujue 2015 haki isipofanyika Tanzania haitatawalika ujue kabisa!! watu wako tayari kwa lolote bwana mdogo. Ule tu fedha za hao wanaokutuma lakini utaambulia patupu ndugu yangu. Kikwete na mtoto wake hawatakuwa na nafasi ya kutawala Tanzania. Tutawakataa kwa gharama yeyote. Tanzania si nchi ya kiarabu na upotelee mbali na mtazamo wako wa kiarabu kwamba utawala utakuwa wa kifamilia hapana haitawezekana hata kidogo! Hiyo nitaarifa kwako.

    ReplyDelete
  24. Bwana ulega, hizo ni hoja za umoja wa vijana au hoja rais kikwete na mwanae? bila shaka ni muhimu kuona kuwa CCM imekwisha, riziwani ni mhasibu wa kikwete, pesa zote za uchaguzi zililotolewa na waarabu yeye ndiye anatuna tena hakuna zilipotangazwa na ndizo alizotumia kununulia nyumba pale osyterbay,mkusanyaji wa malipo yote ya siri ya makampuni ya madini kwa ajili ya baba yake, sasa ulega anasema tayari kikwete anajina la rais wa 2015? nani January makamba? january mbunge wa mbumbuli? kuwaidi wa rostom aziz! fisadi kijana!awe rais basi itakuwa ajabu kubwa!
    lowasa mwalimu nyerere alisema ni mwizi na mlanguzi hana bao na urais huyo,sumaye amefanikisha ufisadi na kuua azimio la arusha na kuanzisha azimio la zanzibar, ni tajiri anayemili maheka na maheka ya ardhi aliyojilimbikizia alipokuwa waziri mkuu hafai kuwa rais. tusibili chadema

    ReplyDelete
  25. mimi nimemuelewa tofauti huyu bwana wa ccmkwamba anataka makamba amtoe nani ataongoza vizuri ccm.labda babu yake sisi mzee makamba ana historia na nchi hii muacheni mzee aichakachue serikali wewe unajua bila makamba kuchakachua kikwete asingeshinda.tena siyo mwizi labda ataharibiwa na mwanae ambaye anakurupuka

    ReplyDelete
  26. kweli mwisho wa mafisadi umefika awana jipya la kutudanganya waache wapigizane kelele siku zao zinahesabika

    ReplyDelete
  27. ulega kauli yako ya kusema viongozi wako wamekula wamevimbilwa na sasa wawapishe nyie mle,sijaielewa sasa kwa taarifa yako hao hawatakula na hata wewe kama uliingia ccm ili ule ndo kiama chako kimefika,rais hamjui nani mrithi wake,maana wana ccm tutamchagua mtu makini na mwadilifu 2015,usimsingizie rais,na wazee wa ccm nawaambia zama zenu zimepita,pia na walarushwa wa ccm dawa yenu inachemka,mlizani ccm ni chama cha kutafutia fedha ee...

    ReplyDelete
  28. nakushukuru mungu baba wa mbinguni kwa kuwa saa hatimaye imewadia kwa chama kilichoiangamiza nchi kuangamia.tunaomba uanze kuugawa ufalme huu dhalimu ili hatimaye uanguke na kusahaulika kabsa.ccm ikifa tanzania itapona. kikwete na majambaz wenzake wakianguka hatimaye taifa litapona amina

    ReplyDelete
  29. vijana hawa batili ni ishara njema ya kuanguka kwa chama hikki batili

    ReplyDelete
  30. Nyie UVCCM ni vifisadi dagaa. Hamna nidhamu kwanza. Tutaunda tume kuwashauri. Acheni mzukaaaa!

    ReplyDelete
  31. Yote haya ni kuwa, mfa maji haachi kutapatapa, vijana wameona hisia tayari,wameyaona yaliyofanywa na babao zao,wanahisi kuondolewa kwenye madaraka,walitamani waongoze nchi baada ya wazee wao, lakini haitawezekana tena,kutokana na maovu yao.CCM UPUMZIKE KWA AMANI, NA MUNGU WA REHMA AKUPE RAHA PEPONI. AMIN!

    ReplyDelete
  32. Kumbe mnajua kuwa mnaimaliza Nchi, asante kwa kutusaidia kutambua kuwa ni zamu yenu kula mpaka mvimbiwe, nasikitika tu kwamba umechelewa kidogo kutoa tamko hili maana lingeisaidia CCM kupata kura nyingi mno, siku zenu zinahesabika mwisho wenu umefika, CCM (cHAMA cHA mAFISADI)LAZIMA MUONDOLEWE MADARAKANI sababu ni moja ambayo mshaisema kuwa MMESHAKULA MPAKA MMEVIMBIWA. Kwa heri ccm.

    ReplyDelete
  33. I HAVE A DREAM TODAY THAT,2015 RAIS ATATOKEA KANDA YA KASKAZINI NA UCHUMI WA NCHI HII UTAKUWA IMARA NA WANANCHI WATAPATA RELIEF TO THEIR PROBLEM.

    ReplyDelete