15 March 2011

Kipa Van Der Sar apata Presha

LONDON, Uingereza

KIPA Edwin van Der Sar, ameingia katika presha ya kutakiwa kuendelea kubakia katika timu ya Manchaster United, yenye maskani yake Old Trafford kwa
msimu mmoja zaidi.

Van der Sar mwenye umri wa miaka 40, amesisitiza kuwa anataka kustaafu katika majira ya joto na kukaa karibu na familia yake, hasa mkewe ambaye ni mgonjwa.

Lakini baada ya kucheza vizuri katika mechi ya michuano ya Kombe la FA dhidi ya Arsenal ambapo, United ilishinda mabao 2-0 kila mmoja katika timu yake anamtaka kufikiri upya kuhusu suala la kuachana na soka.

Mshambuliaji Wayne Rooney alisema: "Tumefuarahi kwa kushinda na Edwin alifanya kazi ya kusisimua kwa kuokoa  michomo, kitu kilichochangia hilo.

"Wachezaji wanajaribu kumshawishi abakie na kuendelea.

"Nilikuwa nikizungumza naye kwenye vyumba vya kuvalia. Ni maamuzi take, kwa hiyo tunatakiwa kuheshimu hilo.

"Lakini ni kipa mzuri licha ya umri wake, kwangu bado ni kipa mzuri duniani."

Lakini Van der Sar anaonekana kushukilia msimamo.

Mke wake Annemarie amepata nafuu ya ugonjwa kwa kiharusi Desemba 2009 na sasa Van der Sar, anataka kutumia muda wake akiwa karibu naye na watoto wake wawili.

Alisema: "Sikatai wazo la kustaafu na ninaangalia mbele."Unakuwa juu na ninafikiri itakuwa ni kitu kizuri kumaliza ukiwa juu. Ninataimisi soka na mambo yake, ambayo nimedumu nayo kwa miaka 20.

"Lakini kuna baadhi ya mambo mzuri, mke mpenzi na watoto wazuri."

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amempongeza Van der Sar, ambaye alikuwa shujaa Old Trafford.

Wenger anaamini kuwa hata kama United itapata kipa mwingine wa kuchukua nafasi yake, watakuwa dhaifu kwa kutokuwa naye.Alisema: "Ni mmoja kati ya makipa wazuri duniani.

"Kama United inaye akiwa na umri wa miaka 40, haijalishi nani watakayemnunua msimu ujao kama hatacheza, wataona tofauti.

"Si tu ni kipa wa kipekee mwenye uzoefu, ana kipaji cha kipekee."

No comments:

Post a Comment