15 March 2011

UVCCM hawana mamlaka kutung'oa-Chiligati

*Makamba asema hayo ni maoni ya vijana
*Lowassa ahoji nani asiyeona uchumi ulivyo?


Na John Daniel

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Maponduzi (NEC) Itikadi na Uenezi, Bw. John Chiligati amesema
licha ya Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM) kuwa na haki ya kutoa maoni, lakini hawana mamlaka ya kuiondoa sekretarieti madarakani.

Wakati Bw. Chiligati akitoa kauli hiyo, wajumbe wenzake wa sekretarieti waliotakiwa kuachia ngazi kwa kushindwa kutimiza wajibu wao wa 'kumsaidia' mwenyekiti wametofautina kuhusu kauli hiyo huku wakishindwa kuzungumzia kwa uwazi wito huo wa vijana.

Jana gazeti hili liliwakaririwa vuoa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) ukiitaka sekretarieti ya chama hicho kujizulu kabla umoja huo haujachukua hatua za kuwaondoa kwa kuwa imeshindwa kumsaidia Rais Jakaya Kikwete.

Kauli hiyo ilitolewa na Makamu Mwenyekiti wa umoja huo wa mkoani Pwani, Bw. Abdallah Ulega wakati akifungua Baraza la Umoja wa Vijana Mkoa humo, huku akisisitiza kuwa sekretaeti hiyo haifai kwa kuwa ilisababisha chama hicho kushinda kwa taabu katika uchaguzi mkuu uliopita, na kuwa ndiyo imekuwa ikitoa siri kwa chama cha upinzani cha CHADEMA.

Secreterieti inayoongozwa na Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusuf Makamba, inajumuisha Manaibu Katibu Wakuu Bara, Kapteni George Mkuchika na Salehe Ramadhani Ferouz (Zanzibar), Katibu wa Itikadi na Uenenezi, Kapteni John Chiligati, Katibu wa Idara ya Uchumi na Fedha, Bw. Amos Makala na Katibu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Bernard Membe.

Akizungumza na Majira jana Bw. Chiligati alisema kimsingi vijana hao wametumia uhuru wao ndani ya chama kutoa maoni yao na kwamba haoni sababu ya hatua hiyo kusumbua vichwa vya watu kwa kuwa ni jambo la kawaida kikatiba.

"Ni haki yao kutoa maoni, sioni cha ajabu hapo, vijana wana haki ya kuzungumza na kutoa maoni yao kwa uhuru kabisa.

"Lakini Secretarieti inachaguliwa na NEC na tunawajibika kwa NEC kupitia Kamati Kuu, hao waliotuchagua ndio wana mamlaka ya kutuondoa, lakini hilo haliwakatazi vijana kutoa maoni," alisema Bw. Chiligati.

Alipoulizwa changamoto waliyopata na iwapo wanajiandaa kuwasilisha mapendekezo yao kwenye vikao vya juu kutokana na wito wa UVCCM hakuwa tayari kutoa majibu ya moja kwa moja badala yake alisisitiza kuwa hayo ni maoni ya vijana.

"Nimesema hayo ni maoni ya vijana na wana haki ya kuyatoa," alisistiza Bw. Chiligati bila kufafanua.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Yusuf Makamba alisema licha ya kuheshimu uhuru wa kutoa maoni lakini haamini kama yaliyoandikwa katika vyombo vya habari ndiyo yaliyozungumzwa na UVCCM mkoa wa Pwani.

"Hayo ndio maoni ya vijana, wamekaa kwenye baraza lao na wakaona hivyo. Hayo ndio maoni yao mimi sina cha kusema," alisema Bw. Makamba.

Alipotakiwa kujibu iwapo katiba, kanuni na taratibu za CCM zinatoa nafasi kwa umoja huo kuondoa secretarieti iwapo imeshindwa kutimiza wajibu wake alisema;

"Ni maoni yao, lakini pia sina hakika kama yaliyoandikwa yako sawa sawa," alisema Bw. Makamba bila kutoa ufafanuzi wa kina.

Alipoulizwa hatua atakazochukua kama Mtendaji Mkuu wa CCM kuhusu wito huo wa UVCCM alisema yeye hawezi kujitetea kupitia magazeti na kusisitiza kuwa hayo ni maoni ya vijana.

"Siwezi kufanya kazi ya kujitetea kwenye magazeti, wao ni vijana wa CCM, wamekaa kwenye baraza lao wakasema, sasa unataka nisema nini? alihoji Bw. Makamba na kuongeza, "Nasema hivyo ndivyo walivyoona. wajumbe wengine wa sekretarieti hiyo hawakupatikana kutoa maoni yao kwa simu zao zilikuwa zinaita bila majibu.

Mbali na sekretarieti, vijana hao waliwashambulia mawaziri wakuu wastaafu, Edward Lowassa na Frederick Sumaye wakisema kauli zao za kukikosoa chama hazina lengo zuri bali ni njia tu ya kutafuta urais 2015

Akizungumzia suala hilo, Bw. Lowassa ambaye pia alionywa na vijana hao kutoa maoni nje ya vikao wakati anayo nafasi ya kukutana na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM Rais Jakaya Kikwete, alisema maoni yake kuhusu uchumi hayana sababu ya kusubiri vikao.

"Nilikuwa vijijini kwenye ziara sijasoma magazeti, lakini wewe nikikuuliza hali ya uchumi utasema kuwa ni nzuri?Nani asiyejua kuwa kuna hali ngumu ya uchumi! Hata bei ya nyanya imependa hilo nalo tusubiri vikao? alihoji Bw. Lowassa.

Alisema kama mtu anataka kuwania urais mwaka 2015 hawezi kuanza kampeni kwa sasa kwa kuwa kufanya hivyo ni kutoa nafasi ya kushughulikiwa na kuchafuliwa na maadui. Bw. Sumaye hakupatikana jana kwenye simu yake.

Majira ilipomtafuta Makamu Mwenyekiti Taifa wa CCM, Bw. Pius Msekwa ili kuzungumzia wito huo wa UVCCM, alisema hawezi kusema lolote kwa kuwa hayo ni maoni ya vijana na kila mmoja anayo haki ya kutoa maoni yake.

"Hayo ni maoni ya vijana, sasa unataka nitoe maoni gani?" alihoji Bw. Msekwa.

7 comments:

  1. chiligati wacha unafiki, usiwazibe uvccm mdomo kuna mitumba (mambo mengi umeharibu ukiwa waziri wizara ya kazi, hata ccm utaiharibu kama ulivyofanya.
    uvccm na ninyi mnakosea kuwazuia mawaziri wakuu wasizungumze, huu si wakati wenu wa kuwazuia, hali ya nchi ni mbaya sa, msijaribu kushika matawi, siku ya kufa nyani imefika.
    kutokana na nyadhifa walizonazo wana haki ya kuzungumza bila hata kuwasiliana na chama katiba inawaruhusu, hata njaa ikiwepo mpaka wamsubiri kikwete au vikao vya makamba!, hivi kukiwa na msiba wamsubiri kikwete au wasiseme, nini maana ya uhuru wa kutoa mawazo iliyomo kwenye katiba ibara 18?.
    ninyi uvccm ni watoto mnaotaka kurithi uongozi, mmetumainishwa hivyo na wazazi wenu, tabia ya kifalme imekwisha, eleweni hilo. mbumbu nyie.

    ReplyDelete
  2. Hivi, kunaubaya gani kwa viongozi wakuu waliopita kutoa kauli zao juu ya mambo mbalimbali ya nchi yetu kutokana na uzoefu wao? Mbona Marehemu baba wa Taifa alifanya hivyo na hata kuandika kitabu cha kukosoa? Kwani alikuwa anataka klurudi kwenye nafasi ya Uraisi? Sijaona sababu ya kuwakemea Mawaziri wastaafu/waliojiuzulu kuongelewa namna hii. Na kama watataka kugombea Uraisi, pia ni haki yao ya kikatiba. wenyemaamuzi ya kuwakubali ama kuwakataa ni vikao halali vya chama wakati wa mchakato maalumu wa kupitisha mgombea, ama wananchi. Tusikurupuke jamani, siasa/uongozi si lelemama.

    ReplyDelete
  3. kuhusu Lowasa ni kweli hali ya uchumi ni mbaya tena ni mbaya sana, lakini wewe ukiwa chini ya CCM ni moja ya watu waliotufikisha hapa, sasa kujibu maswali kama yesu si kujivua lawama ya kutufikisha hapa, kilo ya sukari 2500, nyama wanakula mafisadi tu, na wafugaji iwapo tu mifugo yao inaumwa, usafiri shida, watu wanashindwa hata kufika kule lolondo kwa babu kujipatia dawa ambayo hata serikali imeshindwa kuwasidia wananchi wake, kweli huu ndiyo muda muafaka wa ccm kwenda zake. tumechoka na maisha haya tunataka mabadiliko na mabadiliko si kutoka CCM ni kutoka chadema, na wala si CUF kwa vile CUF na CCM wameozana na kufunga ndoa ya mkeka,CUF sasa kimya kama vile si chama dume kama enzi zile!! ama kweli ufisadi ni hatari!!!!!

    ReplyDelete
  4. HAO VIJANA WAMETUMWA NA BWANA WAO WASEME WALIYOYASEMA. Umoja wa vijana wana nguvu gani ya kukemea wakubwa (MAPAPA WA UFISADI) wakati wao wanasubiri kinachodondoka mezani kwa bwana wao. Huu ni kama mchezo wa nyani na ngedere tu, wote wanachezea miti ileile na wanakulala na kilekile. Maisha bora ya 2005 yako wapi? Mwenyekiti wenu alituahidi tunayasubiri au ndiyo haya ya sukari, nyama, umeme, usafiri-----juu? I wapi tanzania yenye neema? U wapi utu tuliochiwa na waasisi wa taifa hili? Au ni kubadili sheria ya manunuzi ili kufavor mabwana zenu??????

    ReplyDelete
  5. Hii muvi inasisimua. Juzi hapo UVCCM, wakiwa ndio steringi, walimshambulia Dr. Slaa kwamba ndio mchawi wao. Inaonekana sasa wanatambua kuwa mchawi ni CCM yenyewe au yumo ndani ya CCM.

    Ili hii muvi inoge zaidi, steringi wafanye kweli; watoroke CCM na kuhamia kwa Dr. Slaa.

    ReplyDelete
  6. Yaani hovyoo,hakuna hata sababu ya kutoa maoni.WANASIASA WOTE AKIWEMO HUYO SLAA MNAYEMUONA MKOMBOZI NI MWIZI NA HATA NYIE WATANZANIA MNAOJIDAI KUTOA MAONI NI MAFISADI WA SIZE YENU LAKINI MNANYOOSHEA VIDOLE WENZENU .NCHI HII WATU WENGI NI MAFISADI LAKINI MAHODARI WA KUWANYOOSHEA WENGINE KIDOLE. HIVI ULIWAHI KUONA MCHAGA ANAMLALAMIKIA MWIZI NA UKIONA HIVYO KAZIDIWA MAARIFA

    ReplyDelete
  7. Yaani ukisikia yale mamuvi sterling anakufa kwenye trailer ndio hili sasa. Yaani kabla ngoma halijaanza steling chali

    ReplyDelete