Wanafunzi kulipa sh.150
Na Mwandishi wetu
KATIKA hali ambayo inaweza kutafsriwa kuwa itazidi kuongeza ugumu wa maisha ya kila siku kwa wananchi wa kawaida, siku saba kuanzia leo, wakazi wa
Dar es Salaam, watalazimika kuzama zaidi mifukoni mwao kugharamia usafiri wa kutoka sehemu moja kwenda nyingine jijini humo.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Usafirishaji Majini na Nchikavu (SUMATRA), kupanda huko kwa nauli kunatokana na ombi la Chama cha Wamiliki wa Mabasi mkoani Dar es Salaam (DARCOBOA), ambao walitoa sababu kadhaa, ikiwemo kupanda kwa gharama za uendeshaji.
Katika maombi yao ya kupandishwa kwa nauli, DARCOBOA waliomba nauli za sasa zipandishwe kwa asilimia 100 hadi 200.
"Nauli ya daladala kwa kila abiria mtu mzima kwa kilometa moja katika barabara za lami Dar es Salaam zitapanda kutoka sh 22.9 mpaka sh 27. Nauli za mabasi katika barabara za vumbi kwa baadhi ya maeneo ya Dar es Salaam itakuwa ni sh. 33.0 kwa kila abiria kwa kilometa moja.
Kwa mantiki hiyo nauli za daladala zinazofanya shughuli zake katika barabara ya lami, zimepandishwa kwa asilimia 17.4 ambapo sasa kila msafiri atalazimika kutoa sh. 27 kwa kila kilometa badala ya sh. 22.9 za awali.
Mathalani kutoka eneo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere (JNIA), kwenda eneo la katikati ya jiji (kilometa 16) itamgharimu msafiri takribani sh. 432.
Kwa barabara ya vumbi yenye urefu kama huo msafiri atalazimika kulipa sh. 534.
Kutoka Mbezi Louis mpaka Kariakoo ambapo ni umbali wa kilometa 25, kila msafiri mtu mzima, atalipa sh. 675 kwa safari moja. Kwa urefu kama huo kwa barabara ya vumbi nauli ikuwa sh 825.
Bila kutoa ufafanuzi wa kina juu ya nauli kamili, kwa kila njia ya daladala kutoka eneo moja kwenda jingine, taarifa hiyo ilisema kuwa nauli za wanafunzi nazo zitapanda na kuanzia juma lijalo, ambapo sasa watalazimika kulipa nusu ya wastani wa nauli ya mtu mzima, ambayo inakadiriwa kuwa sh. 150 kwa safari moja.
Uamuzi huo uliofikiwa na Bodi ya SUMATRA iliyokaa Januari 31, mwaka huu, imewaamuru DARCOBOA kuhakikisha wanatimiza masharti yanayosimamia shuguli hiyo ya usafirishaji abiria na mizigo yao mkoani Dar es Salaam.
Hatua hiyo ya kupandisha nauli za daladala mkoani Dar es Salaam imekuja siku chache baada ya SUMATRA kuruhusu kupanda kwa nauli ya mabasi yaendayo mikoani.
Hili la nauli hapa Dar ni sawa kabisa maana, katika miji yote ya TZ na Znz, Dar ndio wanaongozo katika kuishabikia CCM. Sasa kwa ushabiki wao haswa wale waliokuwa wakipokea khanga na T-Shirt na Kofia za CCM lazima waonje adha ya ufisadi kwa kukabiliawa na maisha magumu. Ukiangalia Dar ndi jiji chafu kuliko miji yote ya Tanzania, Dar ndio inakosa maji, Dar ndio kunamaisha ya ufukara sana, na afya duni... lakini hao hao wanawashabikia CCM... Wacha sisi tuliopokea khnga na kofia za CCM tukaichagua tupigike...wenye CCM wao aaah na mashangingi yao. Mapinduzi yatakuja tutakapochoka ufukara wetu na kujiuliza nani chanzo chake? Jibu CCM kick them out!
ReplyDeletehapa naona ni kuzidi kutuumiza sisi watu wenye kipato kidogo kulingana na hali halisi inavyoonyesha kuwa maisha yenyewe ndio hayo, sukauri juu, mafuta juu alafu nauli tena mnapandisha? mtatufikisha wapi sisi watanzania ambao ndio tunatafuta hakishikiki kila siku?
ReplyDeletekila kukicha maisha yanapanda tufanyeje? hebu kikwete ukiwa kama rais wetu angalia vzr hali hii ya maisha ya mtanzania tutashindwa kuishi kwa hali hii
sasa wao wamiliki wa magari ya usafiri wanadai ugumu wa uendeshaji na wanataka mzigo huo uwaendee wanyonge, hivi sasa hao walio pandishiwa gharama za nauli, kipato chao kimeongezwa kwa asilimia ngapi? nadhani huo ni msumari wa mwisho kwa Kikwete na serekali yake... Mimi nilikuwa naishabikia CCM lakini sasa "BASI" enough is enough, mabadiliko ni lazima.
ReplyDeleteMzee Kikwete hepu jaribu kupambanua mambo pamoja na jopo(cabinet) lako zima maaana tunakoelekea si kuzuri hii inaweza kutufanya tuingie katika matatizo kama ya afrika kaskazini.Amani tunayoongelea iko wapi kama hali ni mbaya kiasi hiki,halafu tunajifanya kusuluisha matatizo ya wenzetu wakati kwetu kunafuka moshi mimi nadhani tuna utulivu tu nchi hii lakini amani hakuna.
ReplyDeleterais kikwete ameshindwa kazi! anasubiri nini ikulu?
ReplyDeleteHalafu hawa jamaa bwana? Yaani nauli ishafika kiasi hicho? Maisha juu kilichobaki nchi iyuzwe kila mtu apewe chake maana tunaenda wapi? Ni bora kikwete ujiuzuru wanajeshi waongoze nchi ukiwa kama AMIRI JESHI MKUU UMESHINDWA NA UMETUSIKITISHA SANA MAANA WATANZANIA TULIAMINI KITU TUSICHOKIJUA.
ReplyDeleteAchia ngazi bwana kwani umezaliwa IKULU? nchi ishakushinda JAKAYA MRISHO KIKWETE RAIS WA JAMUHURI YA WATU WANAOKUFA NA MABOMU NA MAISHA YA HOFU,VIFO,UFISADI,NA UCHAKACHUAJI KWA KILA MTANZANIA.
ReplyDeleteYote haya yanayotokea inatakiwa kuwa fundisho kwa wananchi wote,Lakini bado utaona siku ya kupiga kura inapofika watu huwa wanasahau yote yaliyowapata katika ugumu wa maisha na badala yake wanamchagua kiongozi asiyewafaa kwa ajili ya Khanga,T-shirt,Skafu pamoja na pilau na Shillingi elfutano.Tatizo bado lipo kwa wananchi kwa sababu hawajui nani wakumchagua.
ReplyDeleteNdugu Kikwete kwa hakika unatufikisha ulipotuahidia, maana maisha duni kabisa kwa kila Mtanzania! Hongera sana najua huna la kupoteza maana ni kipindi chako cha mwisho! Lakini ole wako, hata mawe yatasema!!!
ReplyDeleteUwiiiiiiiiiiiiiii! jamani watanzania wenzangu,kila kukicha hali inazidi kuwa mbaya, Kwa mshahara upi utakaogawia nauli ya wanafamilia kila siku na kwa mwezi mzima, ni mshahara upi utakaolisha familia, utakaolipia kodi ya nyumba, utakaopeleka familia hospitalini, utakaosomesha wanangu,utakao lipia bili za umeme ambao haupo, Kwa mshahara upi utakaonunulia maji ya familia bado wazazi wangu wanahitaji msaada wangu. Ukiangalia woote wanaopinga mikutano ya CHADEMA bili za matumizi ya familia zao wanalipiwa na serikali na mishahara yao ipo safi. Sasa mlalahoi mie nifanyeje ili niishi kama mwanadamu ktk nchi yangu?.
ReplyDeleteHIVI NYINYI MNAOMLAUMU KIKWETE NA SERIKALI KWA HILI MNA NYASI KICHWANI BADALA YA AKILI. DUNIA IPO KWENYE RECESSION. HATA ANGEKUWA BABU YENU MPAYUKAJI SLAA ASINGEKUWA NA LA KUFANYA. KUNAPOTOKEA MISUKO SUKO DUNIANI UCHUMI UKAENDA CHINI KILA MTU ANDHULIKA. BEI ZA MAFUTA DUNIA NZIMA ZIMEPANDA SABABU YA YANAYOTOKEA LIBYA. BAADHI YA WATANZANIA HAWANA ELIMU YA KUCHANGANUA MAMBO. HIVI RAIS ANA NGUVU GANI MPAKA ALAUMIWE KWA KILA KITU? TUMIENI AKILI JAMANI.
ReplyDelete