Na Edmund Mihale
MCHUNGAJI wa Kanisa la Maombezi, Anthony Lusekelo 'Mzee wa Upako' amesema kuwa wanaompinga, Rais Jakaya Kikwete katika utawala
wake wapo katika ushindani lakini hawatashinda katika vita hiyo.
Akizungumza na mwandishi wa habari Dar es Salaam jana kuhusu kile alichokiita Afya ya Amani, Umoja, Upendo na Uvumilivu, Mchungaji Lisekelo alisema kuwa ili nchi iwe na afya inahitaji matunzo na si kelele za kulaumiana.
Alisema kulaumiana kumeshika kasi tangu Rais Kikwete ashike madaraka kwa miaka mitano lakini mazuri aliyoyafanya hayasemwi bali mabaya ndiyo yanayozungumzwa hata kama yamejificha.
Kauli za Mchungaji Lusekelo zimekuja kukiwa na malalamiko ndani ya jamii, kuhusiana na utendaji kazi wa serikali ya awamu ya nne, hasa kushindwa kupunguza mfumuko wa bei za bidhaa muhimu na kupunguza umaskini.
Lakini yeye alisema, "Unapojenga afya ya kitu chochote ni lazima ujue misingi ya nchi ni lazima tuheshimu na kuwapenda viongozi wetu tuliochagua na kuwapigia kura. Hata katika maandiko kiongozi anatakiwa aonywe kwa hadhari, heshima na hekima na si kwa makelele.
"Utawala ni mamlaka inayowekwa Mungu lakini inaashiria wazi kuwa tumeanza kuondoka katika misingi hiyo na sasa mtu yeyote anasimama na kumsema Rais Jakaya Kikwete anavyotaka. Hapana. Hili jambo halipendezi mbele ya Mungu," alisema Mchungaji Lusekelo.
Alisema imejengeka tabia kuwa ukimsema Rais Kikwete ndiyo unaonekana kuwa jasiri na mzalendo, utamaduni ambao ni mbaya.
"Hatupo tayari kumpongeza kiongozi akiwa hai, watu wanasifu maiti kuliko mtu akiwa hai hizi ni fikra za kishetani na hazipaswi kunyamaziwa.
"Mfano Mwalimu alipokuwa hai hakuwa na sifa hizi tunazoziona sasa, walisema wazi wamechoka na 'unyerere' leo hii tunamasifu kwa kila nderemo. Watu wamebadilika wanasifu viongozi wanapotoka ndani ya madaraka.
"Inakuwaje Rais Kikwete tunayemfahamu aliingia madarakani akiitwa Masia na chaguo la Mungu leo ni adui wa kwanza. Hili linatokana na wachache wanaomsaidia rais kukiacha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwa na nguvu na kikaacha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwa dhaifu. Hivi sasa kukitokea tatizo kama la kutonyesha mvua basi lawama atatupiwa rais," alisema
Alisema kuwa ana imani kuwa rais atakayekumbukwa maishani ni Rais Kikwete hivyo aachwe atekeleleze mchakato wa katiba kupunguza mfumko wa bei na kujenga barabara za hewani.
Tapeli with sterile urguments special for laymen[walei]
ReplyDeleteMheshimiwa sana mchungaji, mawazo yako nayaheshimu japo siyaafiki. Rais anatakiwa kuchukua hatua madhubuti dhidi ya matatizo yanayolikabili taifa nasio kukaa kimya huku nchi ikienda kombo. Matabaka yanayo jengwa na huu ubepari wa kikasino ktk nchi yetu yataleta balaa sio muda mrefu. Sijui wewe mzee wa upako hulioni hili? au Mungu wako haja kuotesha? nilidhani ungemuomba Mungu wako atuepushe na balaa hilo badala ya kumfagilia rais anayelea mafisadi na ubepari wakikasino unaoruhusu viongozi kukusanya mtaji kwanjia za kifisadi
ReplyDeleteMchungaji umenena hasa. Wanamsakama bure JK. Je, mabaya ya utawala wake yanazidi Mazuri na mema aliyoyafanyia taifa letu?
ReplyDeleteNa iwapo angemsifia SLAA, mngemtuhumu mchungajiLUSEKELO
A.M CHILENDU
ReplyDeletelusekelo you dont have a stable church ,bado unajipendekeza kwa serikali, wewe unajua shida za watanzania au unaropoka , una uwezo wa kwenda Naigeria waTanzania wanalala na njaa unayoongeea yanaoyesha limits za upeo wako ,pole MTUMISHI WA " mungu "
NINACHOKIONA HAPA NI UPOTOSHAJI TU .HUYO LUSEKELO TUNAMFAHAMU .... AACHE UPOTOSHAJI .AKUMBUKE HATA YESU ALIWAHI KUMUITA HERODE "MBWEHA" ANATAKA KUTUAMBIA KWAMBA YESU HAKUMTII MUNGU?.SUALA LA MUNGU KUCHAGUA VIONGOZI NA MAMLAKA YA KIBINADAMU LILIKUWA SPECIFICALLY KWA WAYAHUDI NA LILIKOMA MARA MOJA HASA PALE WALIPOMTAKA MUNGU KWAMBA NAO WANAHITAJI MFALME ATAKAYE WAONGOZA KAMA MATAIFA MENGINE NA NDIPO ALIPO PATIKANA SAULI.KUKOSOA UZEMBE SIYO KOSA HASA UNAPOKUWA NA KIONGOZI MZUBAVU ASIYE JUA WAJIBU WAKE UKUMBUKE ALIWAITA MAFARISAYO "WANAFIKI" NA KUWAFANANISHA NA KABURI JE YESU ALIPOFANYA HIVYO ALIKUWA NA MAANA GANI?HAWA WALIKUWA WATAALAMU WA SHERIA ZA KIYAHUDI NA WABOBEVU KATIKA DINI.TATIZO LA WATUMISHI MASLAHI HAWATETEI WAGONJWA ,MASKINI,YATIMA WAJANE NA WANYONGE AMBAYO NDIYO DINI YA KWELI NDO MAANA HATA KANISANI KWAKE AMEPANGA VITI KIUBAGUZI VIKIWEMO VYA MATAJIRI HII YOTE INAONYESHA KWAMBA ANAONGOZWA KIMWILI ZAIDI KULIKO KIROHO.SI MLAANI ILA MUNGU AMKEMEE
ReplyDeleteHuyu si mchungaji ni kibwetere type,nina shaka kama hatumii njia za giza,fuatilia mahubiri yake kwa makini,uwa anakuwa na kitambaa fulani kikubwa anakiweka begani,chanini icho?na mara kwa mara utamuona anawakung'utia waumin kitambaa hicho wakati wa mahubiri,pia mahubiri yake yanasisitiza zaidi upandaji wa mbegu zaidi ya muamsho,hicho kitambaa inasemekana alikitoa Nigeria ili kivute na kupumbaza waumini.Yeye tunamjua alikoanzia na dhiki zake,leo anavaa mapete makubwa na machain makubwa ya dhahabu,ana biashara gani zaidi ya kuvuna mbegu za waumini?nimesema yote haya ilimuone jinsi mwenye shibe asivyomjari mwenye njaa,yeye hata hatambui kuwa kuna waumini wake wanaojitolea sadaka wakati hawajui kesho watakula nini,hajui umaskini unaoikabili nchi na hajui kuwa kuna watu wachache sana wnaomiliki uchumi wa nchi hii na ku control siasa ya nchi,hajui kuwa umaskini wa nchi hii si wa kuletwa na Mungu bali ni manmade,yote haya anataka watu wayanyamazie na kuendelea kusujudia viongozi heti Mungu ndivyo anavyotaka,hakuna Mungu wa hivyo Lusekelo anayependa waumini marofa na mabwege.Uko tunakoenda watu wanazidi kuamka,Tanzania ya leo sio ya mwaka 47.Kanisa kama Roman wametuzidi sana kwani wao ili mtu awe mchungaji au askofu lazima asome kweli kweli na ndio maana wachungaji wa dhehebu ili wana upeo mkubwa na wanapo hamua kuonge wanaongea mantiki tofauti na wachungaji wa vijidheebu vyenu mtu akilala akiamka anafungua biashara ya kanisa na kujipachika uchungaji,ukifuatilia hata sekondary alifeli,na ndio mwanzo wa kutoa nasaha mgando bila kujali kuwa zinatufikia hata sisi wenye upeo
ReplyDelete"utawala ni mamlaka iliyowekwa na Mungu".Huyu Mchungaji anajua anachokisema? je na awa waliwekwa na Mungu? IDD AMIN,Mobutu Seseseko,Ngwema,Hitler,Ghadafi,P.W Botha,AL Bashir,Taylor,etc etc.Kama akiniambia waliwekwa na Mungu basi Mungu wa Lusekelo ni Tofauti na Mungu tunayemuamini wengi.
ReplyDeleteNampongeza rais kikwete kwa uungwana wa kuruhusu watu wamseme wanavyotaka! vinginevyo watu wengi wangepotezwa. Kwa hilo naamini tutamkumbuka Kikwete Milele!.Ninahofia watu wakiendeleza hulka hii kwa awamu zijazo watakiona cha mtema kuni hata kama wataingia hao wanaowashabikia!.Najua hapendi watu wanavyomsema lakini amelikubali hilo akijua ni jambo la muda!.Ukweli unabaki kuwa serikali yake imeshindwa vibaya kuliko awamu zote zilizomtangulia!. Lakini ni ukweli pia kuwa ameongoza katika kipindi kigumu kuliko watangulizi wake wote. Wanaomkosoa walione hilo.Amekuta misingi ya ufisadi ikiwa imesimikwa barabara!
ReplyDeleteMaaneno ya Mzee wa upako ni sahihi kabisa Kiongozi huwa ana wekwa na Mungu kulinga na uma uliopo mkiwa waovu basi mtapata kiongozi mwovu, kwa hiyo turudi kwa Mwenyezi Mungu ndipo tutapata viongozi wadilifu.
ReplyDeleteASANTE SANA MZEE WA UPAKO KWA KULIONA HILO SIKU ZOTE MTI WENYE MATUNDA MENGI NDIO UNAOPOPOLEWA,KAMA HAUNA MATUNDA HATA NDEGE HAWATUI,JK KAFANYA MENGI MEMA KULIKO MABAYA
ReplyDeleteLAKINI AKUTUKANAE HAKUCHAGULII TUSI,BABA WA TAIFA ALITUFIKISHA WAKATI HATUPATI HATA KIBERITI,SUKARI,SABUNI NA HATA CHAKULA KILA KUKICHA WIMBO TUFUNGE MIKANDA,MPK ALIPOKUJA MZEE RUKSA TUKAOKOKA TUKAANZA KUONA NEEMA YA KILA KITU CHA AJABU MZEE RUKSA AKAANZA KUKEBEHIWA NA KUCHAFULIWA NA MAGAZETI KUDAI UHURU WA MAGAZETI WAKATI YY NDIO ALIYARUHUSU,MZEE WA WATU KAKAA KIMYA NA HAKUJIBU ILA ALISEMA MAZURI YETU WOTE MABAYA NIACHIENI MWENYEWE NA MTANIKUMBUKA!!NI AJABU HAOHAO LEO BABA WA TAIFA ANASIFIWA, WANAKWENDA KUTAMBIKA KTK KABURI LAKE KILA KIONGOZI ANAJIFANYA ANAMTETEA NA KUMUHESHIMU WAKATI NI WANAFIKI,LEO WANAVAA NGOZI YA UDINI AU UPINZANI KWA KUMKASHIFU RAISI WETU JK,NI KUKOSA NIDHAMU NA SI WAKWELI, MAANA HATA DINI ZOTE ZINAAMRISHA KWANZA KUMUABUDU NA KUMHESHIMU MUNGU MUUMBA KISHA KUWAHESHIMU WAZAZI (WALEZI) WAKO NA KUWAHESHIMU VIONGOZI WAKO HATA KAMA NI MAKAFIRI.JK ALIYOYAFANYA MAZURI NI MENGI KULIKO MABAYA YAKE,NA UKIFATILIA NI HUO WEMA NA HURUMA YAKE NDIO VINAVYOMCHONGEA,TUTAMKUMBUKA AKIONDOKA NA TUTAYAONA MAZURI YAKE WAKATI HUO!!
kwanza ngoja niwaambie watanzania wenzangu muogope sana mtu anayejiita mzee wa upako hao watu huwa ni wa hatari sana kwanza mara nyingi huwa ni manabii wa uongo pia walio wa mungu wanajulikana bila hata kujitambulisha kuwa wao ni wa mungu si kama yeye anayejiita mzee wa upako wakati masaa 24 anaruka kwenda naigeri kusaka upako apeleke uagent na huko hawa ndo wale wanao badala ya kusema YESU wanasema YES katika mahubiri yao nani asiye onywa hata yesu aliwaonya wanafunzi wake tena ilifika mahali hata kukaripia
ReplyDeleteAliyoyasema Mchungaji kama binadamu nakubaliana nayo. Jambo kubwa hapa nilionalo mimi ni lawama za watu wengi kumlaumu Rais na pia hata viongozi wengine bila ya kutathimini lawama zetu. Swali kubwa na muhimu ni hili; Je ni kweli ya kwamba JK kwa kipindi cha uongozi wake wa miaka 5 iliyopita hakufanyo lolote jema na kustahili kushukuriwa? Ninakubali kabisa ya kwamba kama mwanadamu JK ana upungufu wake maana hata wanafilosofia wanasema "hakuna mwanadamu aliye sahihi kwa yote" Sipingi kulaumiwa kwa JK maana hata baba au mama unaweza kumlaumu kwa jambo lakini itategemea kauli na maneno yako yalivyo. Wahenga walisema utamtambua mwenye hekima kutokana na maneno na jinsi anavyotembea.Mzee wa upako kwenda Nigeria kunahusiana na nini kuhusu JK? Kakobe je kwenda Korea au Mashehe kwenda Makka (Hijah) na mapadri kwenda Rome kusali kwa Papa!!! Tusichanganye mambo. Maendeleo yetu na nchi yetu hayaletwi na mtu mmoja ila kila mtu ajitume na kujiona ni mtumishi wa nchi katika nyanja aliyonayo.
ReplyDeletehuyu mzee wa upako baada ya kukosa sadaka na matoleo ya kanisani baada ya wafuasi wake kwenda kwa babu baada ya maambezi yake feki ya uponyaji sasa ameona hakuna njia nyingine ya kupata matoleo ila ni kumsema vyema kikwete ili aweze kupata fedha za ufisadi kutoka kwa mafisadi wanaomsaidia kikwete kufisadi nchi.
ReplyDeletekwa msemo mwingine mzee wa upako tayari umeshafisadiwa na mafisadi.
Wewe unayejiita mzee wa upako, umepata wapi huo upako? Au ni wa kujipa mwenyewe? Kiongozi anayejichagua mwenyewe na kujipa sifa za uongo hana tofauti na dikteta! Huna hadhi unayojipa. Wewe wadanganye wa ji nga ule sadaka zao. Ukiingia kwenye anga za werevu utaumbuliwa na hata hizo sadaka utazikosa! michael
ReplyDeleteAma kweli nchi ya Tanzania imeingiliwa. No comment,
ReplyDeletekila mtu ana haki ya kusema lakini mashindano ya maneno sio msingi wa kuikomboa nchi; fanyeni mambo kwa busara sio kuonyesha ufahari wa kumjibu mtu kwa kutamka tuu, tuijenge na kuisaidia nchi kwa busara, kwasababu mabadiliko ya ugali ndani ya nyumba yako hayamtegemei kikwete yanategemea amani katika nchi na bidii yako ya kufanya kazi. Fanyeni kazi kwa bidii hata kama ni kuuza mchicha badala ya magenge ya siasa nchi itakufa na umaskini.
ReplyDelete