Na Agnes Mwaijega
MKUU wa Jeshi la Polisi nchini, Bw. Said Mwema amekiagiza Kikosi cha Usalama barabarani kwa kushirikiana na vikosi vingine vya jeshi hilo kufanya operesheni kali
ili kudhibiti ajali zinazotokea kwa uzembe.
Operesheni hiyo itahusisha kudhibiti mwendo kasi kwenye barabara kuu kwa kutumia kipimo maalum kiitwacho 'speed rader', madereva wote kupimwa kiwango cha ulevi kabla ya kuanza safari na kudhibiti magari mabovu barabarani.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamishina Mwandamizi wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Bw. Mohammed Mpinga alisema kutakuwa na wakaguzi wa magari ili kubaini magari mabovu kabla hayajaanza safari.
Alitoa mwito kwa Jeshi la Polisi, abiria na wananchi kwa ujumla kutoa taarfa kuhusu madereva wanaokiuka kanuni na sheria za usalama barabarani hususani mwendo kasi, ulevi, uendeshaji hatari wa magari pamoja na uzembe wa aina yoyote.
"Tunaomba wananchi waoneshe ushirikianao kwa kufichua uhalifu wowote unaofanywa na madereva," alisema.
Aidha Bw. Mpinga aliwataka wamiliki wa magari na madereva kuyatengeza haraka na kuyaondoa barabarani pindi yanapoaribika.
Vile vile jeshi hilo limewaagiza wamiliki wa malori makubwa yanayobeba makontena na mafuta kuweka viashiria vya kuonekana wakati wa usiku ili kudhibiti ajali zinazotokea.
Alisisitiza kuwa jeshi hilo litachukua hatua kali za kisheria dhidi ya wamiliki na madereva wote watakaokiuka kanununi, sheria na taratibu za usalama barabarani.
Tatizo la Tanzania hasa hao polisi wanasubiri mpaka ajali mbaya zitokee ndo wanakuja na ZIMAMOTO OPORESHENI.
ReplyDeleteTuache siasa tufanye kazi kwa ufanisi (standard) sio mpaka wakati wa ajali tu.
mfano gari inatoka MWZ saa 1 asubuhi na kufika DSM saa 1 jioni , njiani matrafiki wapo ila haiingii akilinini .
Afande Saidi Mwema acheni usanii! Hebu siku moja endesha nyuma ya mabasi haya makubwa ya abiria ucheki kilomita za gari lako kulinganisha na spidi ya mabasi hayo. Nakuhakikishia utaogopa ku overtake. Halafu nakushauri uendeshe gari la mizigo utaona utakavyo nyanyaswa na hao traffic police wako kwa kusimamishwa kila utakapokutana nao, lazima uombwe rushwa. Waambie hao traffic police waache manyanyaso. Hako katabia kao ka kukusanya pesa kila siku mabarabarani kimetuchosha...Aaaghhh!
ReplyDeletePWA,PWA, PWA,Good job....
ReplyDeleteDoria za usiku na mchana zianzishwe
ReplyDeleteJeshi la Polisi halina tena cha kusubiri bali kuanzisha doria za mchana na usiku katika barabara kuu.Tumeona viini vya ajali hizi kubwa ni magari makubwa kuharibika barabarani kisha magari mengine kuyagonga kutokana na kutokuwa na alama inamuarifu dereva mwingine kuwa mbele kuna gari limeharibika.Aidha madereva wa magari ya abiria kusafiri usiku kinyume cha sheria nako kumechangia sana katika ajali za hivi karibuni mkoani morogoro na pwani. Ni wajibu wa Polisi sasa kuhakikisha kuwa wanawajibika vya kutosha hasa kwa kufanya doria usiku na mchana kuhakikisha kuwa hakuna magari mabovu yanayoegeshwa vibaya barabarani, kuzuia magari ya abiria kusafiri usiku na kudhibiti mwendo kasi kwa madereva.
Iwapo kila Polisi wa kila mkoa watafanya doria katika barabara kuu usiku na mchana basi tunaweza kabisa kuepusha ajali hizi.
IGP Mwema kama unasikia ushauri huu fanyieni kazi hili.
Aziz Faruk
DSM