24 March 2011

Mengi aomba kesi yake ihamie korti kuu

Na Rehema Mohamed

WAKILI Michael Ngaro anayemtetea Mwenyekiti wa Kampuni ya IPP Bw. Reginald Mengi katika kesi ya madai ya sh. 1 iliyofunguliwa na mfanyabiashara Bw. Yusuf Manji, ameiandikia
barua Mahakama Kuu kuomba ichukue kesi hiyo kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wake katika Mahakama ya Kisutu.

Bw. Ngaro amewasilisha barua hiyo kwa Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ili ampe Jaji Mfawindi wa mahakama hiyo jalada la kesi hiyo ili aone mwenendo wake katika Mahakama ya Kisutu.

Habari za kuaminika kutoka Mahakama Kuu zilibainisha kuwa katika barua iliyoandikwa na Bw. Ngaro inadai kuwa hakimu aliyekuwa akiendesha kesi hiyo, Bw. Aloyce Katemana anaegeme upande mmoja na kutolea mfano wa moja maamuzi ya Februari 11, mwaka huu.

Maamuzi hayo yalikuwa ya kutupitilia mbali nyaraka 14 zilizowasilishwa na Bw. Mengi ili vitumike katika mwenendo wa kesi hiyo kwa sababu hazina msingi na hazikuhusiana na kesi hiyo.

Miongoni mwa nyaraka hizo zilitupiliwa mbali na Hakimu Mkazi, Aloyce Katemana ni mkataba kuhusu Kampuni ya Quality Finance Cooparation Group na Kagoda Agriculture kwa sababu hazimhusu Bw. Manji bali kampuni yake, na hazina kibali kutoka kwa ofisa wa serikali.

Uamuzi huo ulitokana na Wakili wa Manji, Bw. Mabere Marando kuomba mahakama kufuta nyaraka hizo zilizowasilishwa na Mengi kwa sababu haziendani na sheria.

No comments:

Post a Comment