07 March 2011

Makada CCM wazidi kuirarua CHADEMA

*NCCR nayo kuanza mikutano mikoani

Na Waandishi Wetu

MAANDAMANO yaliyoambatana na mikutano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa takriban siku tisa yamezidi kukisumbua
Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho wanachama na jumuiya zake wamezidi kutoa matamko ya kulaani na kuomba hatua zaidi zichukuliwe dhidi yake, ikiwamo kufutwa kwenye daftari la msajili wa vyama vya siasa.

Mbali na matamko ya Mwenyekiti wa CCM taifa, Rais Jakaya Kikwete, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Bw. John Chiligati na Waziri wa Mahusiano na Uratibu, Bw. Stephen Wassiara; Jumuiya ya Wazazi ya chama hicho waasisi wa chama mkoani Mbeya na CCM mkoa wa Shinyanga wameungana kulaani harakati za chama hicho.

Waasisi wa TANU waibuka Mbeya


Mkoani Mbeya, waasisi wa TANU na CCM wamemtaka Rais Kikwete kutoa tamko la kalipio kwa CHADEMA kutokana na kauli zao zinazoonesha dhahiri kupinga ushindi wake na kutangaza vita kwa namna ya kujificha kwenye hoja ya malipo ya Dowans.

Mzee Michael Mwamkinga (89) alisema kuwa tangu wakiwa na chama cha TANU chini ya muaisisi wake na Rais wa Kwanza wa Tanganyika, Hayati Mwalimu Julius Nyerere walijifunza kutunza amani na utulivu huku hata vyama vilivyokuwepo wakati huo kikiwemo chama cha ASP viongozi wake wakiongozwa na kuiheshimu na kuipenda nchi.

Mimi nasema, sisi wazee nikiwemo mimi tunaposikia maneno mazito yakitamkwa na watoto wetu hawa wanasiasa na kisha wakiachwa bila rais kuwaambia wazi kuwa wakiendelea atawachukulia hatua kali za kisheria sisi tunaanza kuona kuwa yawezekana yeye anawaonea huruma au ana urafiki nao na hivyo wanataka umwagaji wa damu ufike na kisha viongozi wakimbie na kutucha tukipata shida, alisema.

Alisema kuwa viongozi wa CHADEMA wanatafuta umaarufu na   huruma ya kusifiwa na mataifa yanayotaka kuiona Tanzania ikiangamia na kuwapokea viongozi hao watakapokuwa wamekimbilia huko na kupata maisha mazuri huku Watanzania wengine wakifa kutokana na vita.

Naye Muasisi na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, Wilaya ya Mbeya vijijini Mzee Patrick Nswila, alionya kuwa wanaocheza na amani ya nchi wanapaswa kuonywa na rais kwa ukali pasipo kuwaogopa, kwani Watanzania wakati wa uchaguzi mkuu walimchagua kwa kura nyingi wakiamini kuwa kura zao ndio dhamana ya maisha yao na hivyo asisite kutoa maamuzi mazito.

Mimi nasema kuwa Kikwete amepewa nchi hii na Mungu na Watanzania pale walipompa kura nampongeza kwa uvumilivu wake wa ajabu ambapo kama mwenzetu hayati Mwalimu Nyerere angefufuka leo akapewa aongoze nchi hii naamini kuwa kwa jinsi alivyokuwa mkali na asiyependa mtu kuchezea usalama wa nchi angeweza kutoa maamuzi mazito ambayo yangetingisha   dunia, alisema.

CCM Shinyanga

Halmashauri Kuu ya CCM ya Mkoa wa Shinyanga imemuomba Rais Kikwete kuwa makini na viongozi wa vyama vya upinzani ambao wameanza kutumia vibaya majukwaa ya kisiasa.

Ombi hilo lilitolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM mkoani Shinyanga kufuatia tukio la maandamano ya CHADEMA yaliyofanyika mjini humo hivi karibuni.

Kwa mujibu wa tamko rasmi lililotolewa na Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM mkoani Shinyanga, Bw. Hassan Mwendapole jana, Halmashauri Kuu ya mkoa imemtaka Rais Kikwete ambaye pia ni Amiri Jeshi mkuu kuwa makini na macho kwa kutozipuuzia kauli zinazozotolewa hivi sasa na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani nchini.

Tamko hilo la Halmashauri hiyo ya mkoa limedai kuwa ni vyema viongozi wa vyama vya upinzani wakaelewa kuwa Tanzania ni ya Watanzania wote hivyo ni wajibu wa kila kiongozi kujikita katika harakati za kuwaletea maendeleo wananchi wake badala ya kuhamasisha vurugu.

Wajumbe hao wameziomba mamlaka zenye dhamana ya ulinzi pamoja na zile za haki za binadamu ziwe macho na makini juu ya hali hiyo inayochomoza katika baadhi ya maeneo ya nchi ya Tanzania kwa baadhi ya watu kutaka kutumia ndivyo isivyo uhuru wa demokrasia nchini.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM mkoani Shinyanga, Bw. Hamisi Mgeja alisema matukio ambayo hivi sasa yanatokea huko katika nchi za kaskazini mwa Afrika hayawezi kutokea hapa nchini kwa vile Watanzania wanaamini hawajafikia hatua hiyo.

Bw. Mgeja alisema matatizo yaliyotokea huko Tunisia na Misri na sasa Libya yanatokana na viongozi wa nchi hizo kutoheshimu misingi ya demokrasia, tofauti na ilivyo hapa nchini ambapo misingi hiyo inaheshimika.

Alisema Tanzania ni nchi inayoongozwa kwa kufuata misingi ya kidemokrasia kwa kuwaweka viongozi wake madarakani kila baada ya miaka mitano ambao wanatokana na matakwa ya wananchi wenyewe kwa njia ya sanduku la kura bila kutumia mabavu, maandamano wala mitutu ya bunduki.

Wakati huo huo baadhi ya wakazi wa mji wa Shinyanga wameushauri uongozi CCM wa ngazi ya juu pamoja na serikali yake kuacha kulumbana na viongozi wa CHADEMA kwa vile wanachokifanya viongozi hao hivi sasa ni moja ya majukumu yao nchini.

Wakazi hao walisema moja ya kazi ya vyama vya upinzani nchini ni kukikosoa chama tawala kinachoongoza serikali kila wanapoona mambo hayaendi kama inavyotakiwa na kwamba CCM isifikiri kuwa Watanzania wa leo ndiyo wale wa miaka ya sitini na sabini.

Binafsi yangu sioni sababu ya CCM na serikali yake kuamua kuwashambulia hawa watu wa CHADEMA, moja ya kazi ya upinzani ni kukikosoa chama kilichoko madarakani pale wanapoona mambo hayaendi sawa, ni ajabu kusikia CCM ikidai eti CHADEMA wanataka kuleta vurugu nchini, hii siyo kweli,

Haiwezekani hata siku moja Rais Kikwete akiri kuwa maandamano na mikutano ya kisiasa nchini ni ruhusa kwa mujibu wa katiba ya nchi, halafu ategemee viongozi
hao wa upinzani wapande majukwaani kukisifia chama tawala, itakuwa ni miujiza, na viongozi watakaofanya hivyo watakuwa wamefilisika kisiasa, alieleza Bw.  Fredy Mmassy.

Kwa upande wake Bw. Said Kalindile alisema CCM na serikali yake walichopaswa kufanya mara baada ya CHADEMA kuamua kufanya maandamano ya amani nchini na mikutano ya hadhara, ilikuwa ni kutekeleza yale yanayolalamikiwa, kwa mfano kuwapunguzia Watanzania ukali wa maisha na kudhibiti mfumko wa bei za bidhaa.

Mimi sioni sababu ya serikali kupigizana kelele na CHADEMA, wanachokifanya ni sahihi kabisa, wala hawalengi kuleta vurugu nchini, kama vurugu zitaletwa na serikali iliyoko madarakani baada ya wananchi kuchoshwa na jinsi serikali inavyoendeshwa, ulikuwa ni wakati muafaka wa CCM kujibu mapigo kwa vitendo badala ya vitisho, alieleza Bw. Kalindile.

Kauli ya Jumuiya ya Wazazi

Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kinondoni, imemuomba Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kuangalia uwezekano wa kuifuta CHADEMA kutokana na vitendo vya kuchochea vurugu katika mikutano yake na kuhatarisha uvunjivu wa amani.

Akizungumza katika mkutano wa wajumbe wa jumuiya hiyo Dar es Salaam jana, Katibu wa Wazazi wa Wilaya ya Kinondoni Bw. Stanley Mkandawile alisema vurugu hizo huchochewa kupitia maandamano yanayodaiwa kuwa ya amani yenye lengo la kuiondoa serikali halali iliyopo madarakani.

Bw. Mkandawile alisema wanalaani vitendo hivyo kwa kuwa vinakwenda kinyume cha sheria na kukiuka katiba ya nchi.

"Nchi yetu ni ya kidemokrasia, hivyo tunawaasa ndugu zetu wa CHADEMA wasubiri hadi uchaguzi ujao wanadai sera zao na sio kutumia mikutano kuchochea vurugu zisizo na faida katika jamii," alisema Bw. Mkandawile.

Katika hatua nyingine, Bw. Mkandawile aliiomba serikali na Jeshi la Polisi kuwachukulia hatua za kisheria viongozi wa chama hicho bila kuwaonea haya kwa kuwa wanachokifanya ni uhaini unaoweza kugharimu maisha ya wananchi.

NCCR nayo kuanza mikutano

Chama cha NCCR-Mageuzi kimeandaa mikutano ya kitaifa ya hadhara kwa ajili ya kuwashukuru wapiga kura kutafuta wanachama wapya na kutoa semina kwa madiwani wao nchi nzima.

Mkuu wa Idara ya Itikadi na Mafunzo wa NCCR-Mageuzi, Bw. George Kahangwa alisema kuwa ziara hiyo ikatayoongozwa na viongozi wa kitaifa inaanzia mkoa wa Kigoma ambako leo uongozi wa kitaifa wa chama hicho utakutana na viongozi wa wilaya ya Kasulu.

Alisema kesho kutakuwa na mkutano wa NCCR-Mageuzi utakaofanyika Kasulu mjini kwa ajili ya madiwani wao 19 waliochaguliwa katika mkoa wa Kigoma kupata mafunzo ya kiutendaji.

Bw. Kahangwa alisema Machi 9 kutakuwa na mkutano wa hadhara utakaofanyika Kasulu vijijini na siku iyakayofuata kutakuwa na mkutano mwingine wa hadhara Kasulu mjini na Manyovu.

Bw. Kahangwa alisema Machi 11 mwaka huu NCCR-Mageuzi itafanya mkutano wa hadhara Buyungu na Muhambwe na kufuatiwa na mwingine utakaofanyika Kigoma Kusini na Machi 13 utafanyika Kigoma Kaskazini na Kigoma Mjini.

Alisema katika mikutano hiyo NCCR-Mageuzi itazungumza na wananchi kuhusu masuala mbalimbali ya kitaifa kuhusu maendeleo, uchumi na huduma za jamii.

Imeandikwa na Rehema Mohamed na Peter Mwenda, Dar; Suleiman Abeid, Shinyanga; na Charles Mwakipesile, Mbeya

25 comments:

  1. Wewe mzee wa tanu ni fala, hujui dunia ilipofikia kwa wazee wengine wote wa hiyo 5 walishakufa. Kunywa ulanzi ukalale!

    ReplyDelete
  2. CCM na vibaraka wao wanataka kututisha kwamba CHADEMA wanataka kuleta vurugu nchini. SI KWELI.

    WENYE KULETA VURUGU NI CCM na serikali yao ambayo imeshindwa kuwaletea maendeleo wanachi na KUWASHEHENISHA AHADI ZA UONGO. MWISHO WA UTAWALA HUU UMEFIKA. CCM itaondoka sio kwa mabavu bali kupitia chaguzi. Thru the ballot box.

    CHADEMA keep up the fight: -

    "WHEN THE WATER STARTS BOILING IT IS FOOLISH TO TURN OFF THE HEAT" Nelson Mandela.

    ReplyDelete
  3. we mzee pumzika ww acha uzee wako wa busara hapa. sisi sio zama zako ulizokuwa mnaogopa viongozi wenu wa serikali pindi wakipotea katika maadili ya uongozi. Basi ieleweke wazi kwamba raisi wetu wa Jamhuri ya TZ kashindwa kazi. kazidi kukumbatia ufisadi na utawala mbovu anaouonesha kwa raia zake. Hatumtaki tena, tumechokwa nae...tunataka maendeleo.
    hata kama CHADEMA itasimamishwa kufanya mikutano, wananchi tutaingia mtaani kwa nguvu ya umma (PEOPLES' POWER ) kuhakikisha vitu vinaeleweka.
    KIKWETE kuwa makini na uongozi wako... tumechoka BANA.

    ReplyDelete
  4. WAZEE WETU PUMZIKENI KWA AMANI KWANI HAMNA MUDA MWINGI WA KUTESEKA NA MATESO YA CCM SISI VIJANA NA WASOMI WOTE TUNATAKA CHANGES NA SIO MANENO MAKAVU NA KUTISHIANI BUNDUKI. NA MSIFIKIRI CCM MKO SALAMA MAANA HATA JESHI LIMEGAWANYIKA NA NDIO MAANA UNAONA WIMBI LA SIRI KUVUJA HASA KWA WAKUBWA WANAOTUMIA MADARAKA VIBAYA NA MALI ZA JESHI.

    ReplyDelete
  5. KWELI KINA MTU NA AKILI ZAKE HV WEWE ELIMU YAKO UMEKIMBIA UMANDE UNATARAJIA KILA KITU UFANYIWE KILA KUKICHA WIMBO SHIDA WE SHIDA, JITAHIDI KWA BIDII ZAKO UNAAMKA ASUBUHI UNATEGEMEA ULE KWA JASHO LA NANI? VIJANA HANGAIKENI TUINUE MAISHA YETU ANGALIENI WATU WANAVYOBANGAIZA WEWE KILA KUKICHA MAANDAMANO UNAKULA UKIMALIZA KUANDAMANA UNAPATA CHAKULA/ AU SHIDA ZAKO ZINAISHA? TUAMKE TUSIWE BONGO LALA UNAHANGAISHWA NA SHINIKIZO HUYO ANAEZUNGUKA AKAKUHAMASISHA WEWE AKITOKA HAPO POSHO YAKE SWAAFI KILA SIKU LAKI 2 WEWE UNAIGA ACHENI USHAMBA

    ReplyDelete
  6. INAONYESHA WAZI WENGI WA HIZI COMMENT NI WAIGAJI NA HAWANA MAWAZO YA MSINGI WAMEFANYA KIJIWE CHA KUTOA UOZO WAO NA NJIA ZA KUWATUKANA WATU WENGINE WAKATI WENGI NI ZAIDI YA BABA ZAO AU BABU ZAO NAWASIKITIKIA SANA TUWE WASTAARABU TUACHE UTOTO HIZI COMMENT ZINAENEA ULIMWENGU MZIMA ACHENI KUCHAFUA HALI YA HEWA KAMA HUNA CHA KUSEMA KAA KIMYA

    ReplyDelete
  7. Kila anayetetea CCM ni mbinafsi wa hali ya Juu. Huwezi mpaka dakika hii kung'ang'ania amani wakati hakuna Haki. CHADEMA haina Jeshi, Polis, Mgambo wala mabaunsa, so achen hoja zenu za kipumbavu kusema kwamba eti CHADEMA wanataka kumwaga Damu. Nipo very serious, ole wake serikali ifanye kosa la kukifuta au kukichachafya chadema. siku watakapofanya hivyo ujue ndo mwisho wa serikali ya CCM na Huyo Mzaramo wenu. tumechoshwa na CCM na viongozi wake.CHADEMA JUU!......PEOPLE'S POWEEEEER....!!!! Kidumu CHADEMA, adumu Dr. Wilbrod Slaa na Freeman Mbowe

    ReplyDelete
  8. CCM wamekuwa na ndoto ya kutawala milele.Ninaomba mungu awaangaze CCM watoke madarakani.Ninaamini mungu atasikia sauti yangu CCM wataondoshwa madarakani.Kuna mtu kama Mh.Makamba ndio kajisahau kabisa anaongea maneno utafikiri amelogwa.Hongera Chadema kwakuikosoa CCM.

    ReplyDelete
  9. TUMECHOKA NA KUONGOZWA NA CHAMA KIMOJA TUNATAKA MABADILIKO KWANINI? CCM ITAWALE MILELE, IKUBALI KUSHINDWA ISIWE INACHAKACHUA, KWA KUTUMIA NGUVU YA DOLA. CCM HAIWEZI KUJUA MAPUNGUFU YAKE MPAKA IACHIE MADARAKA, KWA CHAMA KINGINE, TUKIENDELEA NA CHAMA KIMOJA KUTAWALA NI BORA TUKAJIITA NCHI YA CHAMA KIMOJA(MONOPARTISM)

    ReplyDelete
  10. mimi nawashauri ccm waache malumbano unajua unapopata mtu anakuambia hapa unafanya vibaya unatakiwa ufanye hivi unatakiwa ushukuru huyo mtu maana nia yake ni kukusaidia wewe ili uweze kufikia malengo yako lakini sivyo ninavyoona kwa ccm leo wanakosolewa wao wanakuwa wakali chamsingi ni kuchukua hatua ya utendaji mapema tuache ubabe ccm tuangalie changamoto na kuzifanyia kazi bado mna nafasi

    ReplyDelete
  11. Kuchoka kutawaliwa na chama kimoja ili Kubadilisha chama basi iandikwe kwenye hiyo katiba mpya,kuwa kila baada ya miaka 10 kije chama kingine,siyo kwa mabavu eti wametawala miaka mingi wakati Viongozi wanabadilika kila miaka 10 ktk CCM, huko nje tatizo lao ni Kiongozi kukaa muda mrefu na kurithishana sasa wewe unadai eti CCM inatawala peke yake kwa hiyo tuachane na uchaguzi tuweke ktk katiba kila baada ya miaka kadhaa tunaanza na CUF,Chadema,NCCR nk, mpk viishe vyote 13 turudie tena!! vichekesho wacheni upotoshaji

    ReplyDelete
  12. CCM wanawalinda mafisadi na kuwatetea wabaki madarakani ili wawape mapesa.Hata kama ni mwasisi hatuwezi kukusikiliza kama unatunyanyasa.Waacheni CHADEMA waelimishe watanzania kwa sababu chama tawala kimeshindwa kuwasaidia wananchi.Kwani chama tawala mkiendelea kupiga kazi bila kulumbana na CHADEMA mtapungukiwa nini? Mimi sioni haja ya kuwafuatilia.Kuna mambo mengi ya kufanya zaidi ya kuwaangalia CHADEMA wanafanya nini.

    ReplyDelete
  13. Naomba watanzania wenzangu muelewe lugha anayoongea rais Kikwete, " Kumwaga damu" ina maana CCM hawako tayari kuachia madaraka mpaka damu imwagike! wakikubali kuachia madaraka kwamba wameshindwa damu itamwagika saa ngapi? maskini wengi wa wale wanaojiita CCM hawajui kwamba CCM ni ya watu wachache sana tena mafisadi pale juu, ni JK, Rostam, Lowasa, Makamba, Chiligati, Ngereja, Maige, Tendwa na Januari wengine wote ni vibaraka tu!

    ReplyDelete
  14. Katika kuongoza nchi yoyote ukishafikia hatua ya kugawa madaraka kwa watoto wako.Hapo lazima siku moja kutawaka moto.Wananchi watachukua mishale na wewe utaomba jeshi lako likusaidie.Ki ukweli wanaounga mkono chama tawala ni wale ambao maisha yao ni bora kidogo kwa sababu za hapa na pale.Kwa kuwa mlalahoi amesahaulika anatakiwa aelimishwe hali halisi ya nchi hii tulipo sasa.

    ReplyDelete
  15. VIJANA WENGI WA KIBYA NA MISRI WAMEKATAA KUISHI MAISHA WALIYOISHI BABA NA BAU ZAO YA KUNYANYASWA NA KUONEWA NA WATAWALA WAO. NASI VIJANA WA TANZANIA TUNAKATAA HALI YA KUTAWALIWA KAMA AMBAVYO WEWE ULIVYOTAWALIWA NA CCM KWA MIAKA NENDA NA MIAKA RUDI KIASI KWAMBA HAPO ULIPO UKIUMWA TU UKIFIKISHWA HOSPITALI HATOKUTA DAWA WALA KIPANDE CHA DAWA, SISI VIJANA WA SASA TUNAIKATAA HIYO HALI KWA NGUVU MOJA KWANI TUNAJUA KWAMBA NCHI YETU INAOUWEZO WA KUJAZA DAWA HOSPITALINI ZOTE NCHI KAMA TUKIONDOKANA NA VIONGOZI WABABAISHAKI KAMA KIKWETE.KWAHIYO WEWE UMEKUBALI KUWA HALI YA KUTOKUWA NA DAWA, UMEME NA MAJI KWAMBA NI HALI YA KAWAIDA SISI VIJANA HATUTOIKUBALI HALI HIYO KAMA WEWE TUNAEBDELEZA MAPAMBANO MPAKA KIELEWEKE.

    ReplyDelete
  16. Ni furaha kuona wananchi wanavyofikiri na kutoa fikra zao.Wengi wenu hapo juu mnashindwa kupambanua Sera za kiuchumi katika nchi za kiafrika, ukwlei ni kwamba nchi nyingi kama zi zote afrika hazina uwezo wa kuthibiti uchumi wake hata hao south afrika au Nigeria au Misri kote wapo mabepari wanaosimamia na kutawala kwa namna moja au nyingine. Niwaambie tu kwamba hata hao CHADEMA ambao leo mnawapigia chapuo wanaendesha shughuli zao kwa msaada wa Waingereza ambao wanataka ikiwa madarakani waje kuendesha uchumi wa Tz.Hivyo basi suala la unafuu katika maisha si la chama wala serikali, ni la mtu binafsi, fanya kazi kwa maarifa na kujituma ili upate mafanikio. Serikali ifanye kazi ya kukuwezesha kufanikiwa katika kazi zako. Usitegemee serikali ikupe mkate wako kila siku, au ikuzolee taka nyumbani kwako na ww unafanye nini, kula kulala au? Penye mambo ya msingi tuseme mfano uhaba wa walimu,wafayakazi wa afya, madawa etc lkn si kila kitu serikali, hata nguo zenu za ndani?
    Acheni uwongo, hata Slaa akiwa rais leo mtamchukia baada ya mwaka mmoja kwani uchumi hataushika yeye,ila mwingereza na hakuna Mzungu anayetaka awe sawa na mwafrika hilo tambueni.Mlikataa ujamaa wa TANU na Nyerere mkataka ubepari, sasa hiyo ndo tamu ya Ubepari.

    ReplyDelete
  17. CCM ni manyang'au hawawajali wananchi. Wananchi wengi wako vijijini na hawana wa kuwasemea. Wananchi wengi wanakula mlo mmoja, na wakati huo huo ccm wanafurahia ufisadi.

    Bila haki hakuna amani, amani ipo wapi kwa mtu anaekula mlo mmoja au kulala njaa?

    Amani ipo kwa viongozi wachache wa ccm maana wana hela nyingi kwenye akaunti zao ndo maana wanataka amani ili waendelee kula kiulaini.

    Tanzania hakuna amani, kuna utulivu. Na huu utulivu upo mwishoni, karibu unatoweka. CCM inatumia dola kupora haki na sasa wanatoa vitisho. Ole wenu mtaikimbia nchi no so long time to come!!

    ReplyDelete
  18. NAWAKUMBUSHA SANA WATANGANYIKA KWAMBA CCM INA AJENDA YA UDINI TOKA KUANZA KWA MFUMO WA VYAMA VINGI;CHAMA CHOCHOTE CHENYE NGUVU KWA KIPINDI HICHO WANA JENGA KWAMBA HICHO NI CHAMA CHA DINI FULANI;KUMBUKA CUF WALIPO KUA NA NGUVU WALOSEMA NI CHAMA CHA DINI FULANI;SASA HIVI CDM WANA SEMA KWAMBA NI CHAMA CHA DINI FULANI!

    ReplyDelete
  19. CCM acheni ubabe wasipofanya mikutano munawaita vyama vya musimu.Acheni wafanye siasa,CHADEMA mti wenye matunda mazuri lazima utupiwe mawe,shutumu zote hizi zinaonyesha mlivyo na mambo mema kwa watanzania.

    ReplyDelete
  20. Inasikitisha kuona mtu anamwita baba wa mtu mwingine "fala". Hivi kweli wazazi wetu ambao hata hawakufanikiwa kupata elimu ya juu kama wengi wetu ni mafala? Ewe msomi uliyemwita mzee huyo fala bila shaka una lako na maadili hata yale ya kisiasa ni mafupi mno kwako. Nashauri ya kwamba ni vema mtu achangie mawazo yake na wala si kwa lugha chafu. Tungoje CCM washindwe 2015 na watakaoshinda tuungane nao kuendeleza nchi yetu. Lowassa akisaidia anaitwa fisadi lakini Mbowe akisaidiwa na kisha naye akisaidia hawi fisadi ni kwa lipi?

    ReplyDelete
  21. Wazee wa Tanu kweli! Mawazo yao ni ya mwaka 47, hawa wazee akili zao zimechoka kufikiri na kuwaza. Nawahurumia kwani hawajui wanachokisema. Wao hawajui Tanzania ilipo hivi sasa! Hebu watuambie wakati wao walinunua sukari kwa bei ya 2200? Je wakati wao ufisadi watu kama Rostam Aziz ulikuwepo? Je serikali ya Nyerere ilikuwa imewekwa chini ya genge la wezi wachache? Mimi ningefurahi sana kama wazee hawa wangelimtaka Kikwete awachukulie hatua watu kama Rostam haraka sana. Wakina Rostam ndio wameifikisha nchi hii mahali ilipo. Sasa leo hii wazee wanataka Kikwete awashughulikie wakina Dr Slaa na Chadema na kuwaacha mafisadi wakina Rostam. SIsi tunasema hivi ufisadi ndio dhambi mbaya sana Tanzania kwani inafili nchi na kuiacha hata serikali kuwa chini ya watu wachache ambao wananeema na mfumo wa ufisadi ulioko hivi sasa Tanzania. Ufisadi ndio ajenda nyeti sana kwa sasa wazee wa CCM lazima waliseme hilo kwa nguvu zao zote kama kweli wanaipenda Tanzania. Hivi sasa watanzania hawadanganyiki na wimbo wa amani amani! Bila haki hakuna amani. Amani ni tunda la haki na usawa. Kwenye ufisadia hakuna haki wala usawa. Ukimya watanzania usichukuliwe kuwa ni kigezo cha amani. Hapana watanzania kwa sasa hawana amani kabisa wanasubiri mtu awaongoze kudai haki zao ikibidi hata kwa gharama yeyote. Ili serikali ilete amani Tanzania na kutuepusha na janga la vita ya wenyewe kwa wenyewe lazima Kikwete awashughulikie mafisadi bila kujali kwamba ni marafiki zao waliomuingiza madarakani. Wazee wa CCM mmeaibisha sana kwa kusema Kikwete awashughulikie Chadema na kuwaacha mafisadi. Naomba sana wazee wa CCM mwambieni Kikwete kwamba ili amani ya Tanzania idumu lazima ufisadi uondolewe ili sisi sote tufaidi matunda ya uhuru wetu kwa kununua sukaari bei halali, kupata umeme, barabara nzuri, watoto wetu wapate matibabu na elimu bora. Siyo hii ya shule za kata.Chakula na Maji ambayo ni mahitaji mhimu kwa binadamu yapatikane kwa wote na sio kwa kikundi kidogo cha watu. Bila hivyo hakuta kuwa na amani hata kidogo. Vinginevyo Tanzania hakutakalika. Rushwa imeingia kila eneo la nchi yetu hakuna kupata huduma yeyote mpaka uwe na chochote. Polisi wanabambikizia watu vyesi kwa kuwa hawana mishahara inayotosheleza mahitaji yao zaidi ya yote wameajiliwa vijana wa viongozi ambao hawana sifa za maadili. Wazee wa CCM mwambieni Kikwete aondoe uozo huu ndipo kutakuwepo na amani.

    ReplyDelete
  22. VIJANA; MISRI, TUNISIA, LYBYA NA INCHI ZOTE ZA KIARABU SINASHARE COMMON FEATURES. Watanzania wasikiliza muziki kuchakucha hamwezi, hamuelewi mambo yanakwendaje nawaona hapa mkiishia kutukana. itikieni wimbo wa slaa ufisadi ufisadi. miradi yote mikubwa kama ujenzi wa MANDELA UNV.KULE ARUSHA WAMEJAA WASIO WATANZANIA SISI UFISADI NA SLAA WETU.

    ReplyDelete
  23. Ninaamini Wazee wetu hawamwambii Kikwete awashughulikie CHADEMA bali wanaashiria hatari ya mafarakano kati ya Wanasiasa wetu; na bila shaka wazee hawa hawatazamii kumaliza maisha yao na wana wao kwa njia ya maafa bali kwa amani. Wakitutangulia mbele ya haki watuache na mema sisi na vitukuu wao. Sidhani kama yupo mzazi amtakiaye mwana au binti yake mabaya ila kila la heri. Naomba tusiwalaumu wazee wetu ila kwanza tujilaumu sisi wenyewe kwa kuifikisha nchi yetu hapa. Maana walioichagua CCM na kuwaacha wengine ni sisi wenyewe; nasema hivyo nikimaaanisha Vijana na watu wazima waleo ndio walioingia katika harakati za uchaguzi 2010 na kumchagua rais na wabunge kutoka vyama mbali mbali, Jamani tujipange kwa upya kama tunaona CCM hawafai basi harakati ziwe 2015 kuwaondoa, lakini sasa kwa ajili ya amani yetu tusichochee misalagambo, maana baadaye tutajajuta sisi na watoto wetu. Nawatakikia Watanzania wenzangu mema na kila heri.

    ReplyDelete
  24. Tatizo ni lile lile la CCM kuwa na viongozi wasio na upeo,angalia mtu kama Mgeja na kauli zake za mara kwa mara dhidi ya upinzani,mra namshtaki huyu,mara iki ambazo zote hazina tija,CCM iangalie viongozi wake hasa wale wasio na upeo na elimu kama Mgeja wapumzishwe mapema kabla hawajaleta madhara kwenye chama.

    ReplyDelete
  25. wewe mzee wa tanu watu wanakula mzigo nini?

    ReplyDelete