Na Benedict Kaguo,Muheza
CHAMA cha Wananchi (CUF) kimemtaka Rais Jakaya Kikwete kuhakikisha kuwa suala la katiba mpya linafanikiwa wakati wa utawala wake ili kujiwekea historia ya
kukumbukwa na Watanzania.
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba ametoa kauli hiyo wakati akihutubia wananchi wa mji wa Muheza katika mwendeleza wa mikutano ya 'kuwazindua Watanzania kukiunga mkono chama hicho'.
Profesa Lipumba alisema pamoja na Serikali ya Rais Jakaya Kikwete kushindwa kuwaletea maendeleo wananchi katika kipindi cha miaka 50 ya uhuru, ni vema katiba mpya itakayozaa Tume Huru ya Uchaguzi ipatikane wakati wa utawala wake.
"Mtani wangu Kikwete pamoja na kushindwa kuwaletea maendeleo wananchi katika miaka 50 tangu uhuru, walau hili la katiba mpya lifanikiwe chini ya utawala wako ili Watanzania wakukumbuke kuwa ulileta mabadiliko makubwa ya demokrasia," alisema Profesa Lipumba.
Alisema CUF kina dhamira ya dhati ya kuwaletea ukombozi wa kweli Watanzania ndio maana kinafuata misingi ya kikatiba kutaka kuingia madarakani tofauti ya baadhi ya vyama vinavyotaka kuingia madarakani kwa njia ya maandamano.
"Katika ilani ya uchaguzi ya CCM, hakuna kipengele chochote kilichozungumzia mabadiliko ya katiba lakini sisi CUF tuliwasilisha rasimu ya katiba ili tuweze kupata tume huru ya uchaguzi na wananchi waweze kutoa ridhaa ya kuwachagua viongozi wanaowataka," alisema Prof. Lipumba
Alisema baada ya rasimu hiyo ya katiba, Rais Jakaya Kikwete alikubali na kuliambia bunge kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kuandikwa katiba mpya, sasa ni vema akahakikisha anasimamia mchakato mzima wa katiba ufanikiwe chini ya utawala wake ili kujiwekea historia kwa Watanzania.
"Vinginevyo Mheshimiwa Kikwete ukishindwa hili katika utawala wako, basi utakuwa ndio msanii wa kwanza kuwa rais katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania," alisema Profesa Lipumba.
Awali, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Bw. Julius Mtatiro alisema hali ya maisha ya Watanzania imezidi kuwa mbaya huku wanafunzi wakiishia kula mlo mmoja kwa siku.
Bw. Mtatiro alisema hayo baada ya mtoto wa darasa la tatu kuitwa jukwaani na kuulizwa alikula nini tangu alipoamka asubuhi, naye akajibu kuwa alikuwa hajala kitu.
"Watoto wa aina hii hawako Muheza peke yake ni Tanzania nzima wanakwenda shule na kula mlo mmoja jioni, watoto wa aina hii hawafundishiki darasani ndio maana matokeo ya mitihani yanakuwa mabovu, mtoto anamaliza darasa la saba hajui kusoma kitabu cha darasa la pili," alisema Bw. Mtatiro.
CUF hawana jipya kwa ni nini asiyejua ndoa yao na CCM na ndo maana wanaonekana hawana hoja inayoweza kuwashitua CCM kama CHADEMA wanavyofanya
ReplyDeleteHuyu Profesa au? kumbukumbu ya JK kwa vipi wakati CHADEMA Ndiyo walioanzisha wimbi la mamabadiliko ya katiba!
ReplyDeleteww malkiory usivamie mambo km mende kaona mavi bila kujua hivi unakumbuka watu walikufa pemba kwa sababu ya kudai katiba mpya km huna la kusema shut uppp cuf ndio walionza mchakato wa katiba kabla ya chadema naona wakati huo upo kenu huko unalima karanga km huji uliza na si kuropoka okay
ReplyDeleteInasikitisha sana, kuanza kuuliza nani alianza. ukweli CUF walianza kudai hicho Milkiory anachosema CHADEMA ndio waanzilishi. Kaka usishangae huyo jamaa alikuwa hajui walichodai CUF wakati huo sababu walikuwa wanasema chama cha waislamu, wameagiza makontena ya majambia. wengi wa wafuasi wake waislamu. Naha anachosema Lipumba bado hajakijua, kwa nini atakumbukwa? Hajui kuwa kwa miaka 23 ya baba wa Taifa tulitumia KATIBA YA MKOLONI. MIAKA 1O YA Mwinyi hivyo hivyo, miaka kumi ya Mkapa hivyo. Sasa Heshima na kukumbukwa Jakaya ni pale atakapo kubali kuharakisha kutungwa kwa Taifa la Tanzania na Kuachana na katiba ya wakoloni. Hiyo ndiyo heshima. Na ninaamini atafanya hivyo muheshimiwa rais atafanya mabadiliko haraka iwezekanavyo ili aje kukumbukwa kama Mzee Ali HAssan Mwinyi a.k.a RUKSA
ReplyDeleteHawa chadema wao wataka mambo ya kuigaiga tu.
ReplyDeleteKisa Libya na Tunisia wamefanya maandamano basi na Tanzania nao wafanye, sisi tuko tafauti na nchi hizo waangalie maraisi wao wako madarakani miaka mingapi?na Kikwete anamuda kaitika urais?
Kwahiyo katiba ikibadilishwa atatuwezesha kuondoa wasiwasi wa kuibiwa kura na tukaweza kuweka madarakini Raisi tumtakae bila maandamano ambayo yataleta mtafaruk mkubwa na usio na sababu.
chadema hawana maana.
ReplyDeleteNikweli kuwa sisi tuko Tafauti na hizi nchi zinazo andamana kwani sisi tuna uchaguzi kila baada ya miaka mitano,na kwakuwa tuna wasiwasi na tume basi mara baada ya kubata katiba mpya na tukapta tume huru basi tutaweka madarakani viongozi kwa ridhaa ya wananchi.
ReplyDeleteCHADEMA WACHENI FUJO WAELIMISHENI WANANCHI MAMBO YA KATIBA ILIWAJUE NIMAMBO GANI YA KUCHANGIA WATAKAPO KUJA KUULIZWA.