LONDON, Uingereza
KIPA Jens Lehmann, ameonesha kuwa bado hajawa fiti baada ya juzi kurejea uwanjani katika kikosi cha Arsenal na kupokewa kwa kipigo.Kipa huyo mwenye
umri wa miaka 41, ambaye ametoka katika kustaafu ili kusaidia kutatua tatizo la makipa katika timu ya Gunners, alifanya makosa na kusababisha timu hiyo kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Wigan.
Goli la kwanza alirudishiwa mpira na Sead Hajrovic, ambao ulimpita juu ya miguu yake.
Kosa alilofanya lilifanana na la Paul Robinson, ambaye aliukosa mpira akiwa katika timu ya taifa ya England baada ya kurudishiwa pasi na Gary Neville katika mechi dhidi ya Croatia mwaka 2006.
Lakini safari hii, Lehmann alikuwa na bahati kwa kuwa mpira haukuingia katika nyavu.
Lehmann alikamatwa tena wakati mshambuliaji, Callum McManaman mwenye miaka 19 alipomzunguka na kufunga akiipatia Wigan bao dakika ya 53.
Kipa huyo Mjerumani alifanya makosa mengine, ambapo mlinzi Daniel alifuta makosa yake kwa kuokoa shuti la Daniel Redmond.
Lakini Lehmann alipata mkosi mwingine kwa kufungwa dakika ya 86 wakati mchezaji aliyetokea benchi, Joe Holt alipofunga na kufanya Wigan kuongoza kwa mabao 2-0.
Rhys Murphy aliifungia bao la kufutia machozi Gunners kwa penalti katika dakika za majeruhi.
Lakini Lehmann akizungumzia mechi hiyo, alisema amesisimka kwa kurejea uwanjani, alistaajabishwa kuitwa tena na Arsene."
No comments:
Post a Comment