Na Omary Mngindo, Kibaha
OFISA Mtendaji wa Kata ya Soga Wilaya ya Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani, Betraham Mfaramagoha amemuomba Mkurugenzi wa Kampuni ya
Mohamed Enterprises Limited (METL), Mohamed Dewji kuukarabati Uwanja wa Alave uliopo ndani ya Kata hiyo.
Akizungumza mjini hapa juzi, Mfaramagoha alisema kuwa katika kata hiyo kuna uwanja wa kisasa ambao unamilikiwa na Dewji, ambao ulikuwa ukitumika kwa michezo mbalimbali ya ligi ngazi ya Wilaya ya Kibaha, kabla ya kutelekezwa baada ya kupoteza ubora
wake.
Alisema kutokana na Kata ya Soga kuwa na vipaji vya wacheza soka na timu imara, uongozi huo umeona ni vyema kumuomba Mkurugenzi huyo aelekeze nguvu zake katika ukarabati wu uwanja huo kwa ya kuchezewa mechi za Ligi ngazi za Wilaya, Mkoa na hata Daraja la Kwanza.
"Uwanja wa Alave una kila sababu ya kuwa kiwanja bora ndani ya Halmashauri ya Kibaha Vijijini na pengine na hata nje ya Halmashauri hii, kwani una vipimo vinavyokubalika kimataifa, hivyo tuna mpango wa kuwasiliana na Dewji kuangalia ni namna gani ataweza kutusaidia katika kuukarabati uwanja huo," alisema Mfaramagoha.
Alisema kwamba awali Kampuni hiyo ilivyokuwa ikiendeleza mashamba ya mkonge, uwanja huo ulikuwa katika mazingira mazuri na kuufanya uwe unatumika katika ligi mbalimbali ngazi za Wilaya na Mkoa.
"Imani ya uongozi wa Kata ya Soga na Halmashauri nzima ya Kibaha Vijijini kuwa Dewji atakaposoma taarifa yetu kupitia vyombo vya habari atakuwa tayari kutusaidia na kutuondoa kwenye kilio hiki, lakini wakati waandishi mkifanya kazi zenu nasi tunatarajia kumuandikia barua ya kumuomba," alisema Mfaramagoha.
Huku kuwalilia matajiri ndio kunawafanya wajione miungu watu!
ReplyDeleteViongozi wetu hawaamini kuwa nguvu ya wananchi inaweza kufanya mambo makubwa. wanawasubiri kina ME, RA, Abood, nk. Halafu hao jamaa wakitoa 1m wanaacha kukusanya bilioni za kodi.
Viongozi wetu mna nini? mtu mmoja achukue mzigo wa watu elfu kadhaa bure mliona wapi?
Kusanyeni kodi mjenge uwanja.