Na Mwali brahim
KLABU 10 za mchezo wa Judo, zimethibitisha kushiriki katika mchujo wa pili uliopangwa kufanyika Aprili 3, mwaka huu katika Uwanja wa ndani wa Taifa.Akizungumza
Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Chma cha Judo Tanzania (JATA), Kashinde Shabani alizitaja klabu hizo kuwa ni Flamingo, Magereza Ukonga, Imasco ya Temeke, Kisutu, Budocan ya Korogwe na ya Magomeni, Pentagon, Segerea na Shule ya Sekondari ya Loard Burden Poell na CCP Moshi.
Alisema, zipo Klabu nyingine zilizothibitisha, lakini si kwa maandishi ila klabu hizo 10 ndiyo zimethibitisha rasmi kushiriki.
Shabani alisema, nafasi zipo wazi kwa klabu nyingine kuthibitisha ambapo mwisho wa kuthibitisha ni leo kwa ajili ya kukamilisha mchakato mzima wa kupanga timu zitakazochuana.
Alisema baada ya kumalizika kwa mchujo huo wachezaji watakaofuzu watakwenda katika mchujo wa tatu utakaofanyika Zanzibar, ambao ndiyo utakuwa wa mwisho kwa ajili ya kupata wachezaji watakaounda timu ya taifa, itakayowakilisha kwenye mashindano ya Kanda Tano yakayofanyika nchini Julai mwaka huu.
Katibu huyo alisema, katika mchujo huo wa tatu watachagua wachezaji 20 watakaoonesha uwezo kwa ajili ya kuwaweka kambini, ili kujifua zaidi kwa kuhakikisha wanaacha ushindi nyumbani.
No comments:
Post a Comment