LONDON, Uingereza
FERNANDO Torres amesema kuwa anahofia kuwa Cesc Fabregas anaweza kupata shida ya kupata namba katika kikosi cha kwanza cha Barcelona kama
ataamua kuhamia klabu hiyo akitokea Arsenal.
Barcelona imekuwa ikitaka kumrejesha Nou Camp nahodha na kiungo wa Arsenal, Fabregas lakini Torres anahofia kwa kuwepo viungo wengine wakali waliokuwepo kwenye timu ya taifa ya Hispania iliyotwaa ubingwa wa Dunia Xavi, Sergio Busquets na Andres Iniesta itakuwa ngumu kwake kupata namba.
Mshambuliajiwa Chelsea, Torres ambaye naye bado hajaanza kung'ara katika timu yake mpya tangu alipotoka Liverpool alisema: "Barca ni timu ngumu. Kama Cesc atakwenda ni nani, ataondoka?"
Wakati huohuo Rais wa Barcelona, Sandro Rosell amedai kuwa klabu yake inajiandaa kutenga pauni milion 45 kwa ajili ya kumtwaa Fabregasna kwamba haitaongeza dau.
Mara ya mwisho Juni, mwaka jana miamba hiyo ya Hispania ilitoa ofa ya pauni milioni 30 kwa ajili ya kiungo huyo ambapo kocha wa Gunners, Arsene Wenger alikataa.
Kocha wa Barca, Pep Guardiola amekiri kuwa anamtaka
Fabregas (23) na kumekuwa na uvumi kuwa anataka kufanya tena harakati za kutaka kusaini katika majira ya joto.
Rosell alisema: "Kiwango cha mwisho tunachoweza kutumia katika kipindi cha soka la uhamisho ni pauni milioni 45.
"Kama hatutauza mchezaji yeyote, haitawezekana kumsaini mchezaji yeyote.
"Mwaka jana tulitoa ofa ya pauni milioni 30 na kila kipindi kinapopita bei ya wachezaji inashuka.
"Hatima ya baadaye ya Cesc iko mikononi mwake na tunaweza kufanya makubaliano na Arsenal kama Guardiola atataka hivyo."
No comments:
Post a Comment