Na Tumaini Makene
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Mahesabu ya Shirika ya Umma (POAC), imedhamiria kuinusuru kampuni ya kutengeneza matairi ya General Tyre East African Ltd. kwa
kuchunguza mchezo mchafu unaohisiwa kuwepo katika 'kifo' chake.
Kamati hiyo imeunda kamati maalumu itakayojumuisha wabunge wanne, Ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), watakaochunguza namna gani kiwanda hicho kiliweza kujipatia mkopo wa dola za Marekani milioni 10 mwaka 2005, lakini ilipofika mwaka 2008 kikashindwa kuendelea na uzalishaji.
Kampuni hiyo ya General Tyre, iliwahi kusifika katika ukanda wa nchi za Afrika Mashariki na Kati, kwa uzalishaji na usambazaji wa matairi yenye ubora na kiwango cha hali ya juu, kabla ya kufunga shughuli zake mwaka 2009, miaka minne baada ya kuchukua mkopo wa sh. bilioni 10, kwa msaada wa serikali, kutoka Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Jana kamati hiyo ya POAC ilielezwa kuwa deni hilo sasa limefikia sh. bilioni 21.15 ambapo NSSF wanataka kiwanda hicho kiuzwe ili fedha hizo ziweze kurejeshwa, huku serikali nayo ikisema kuwa kifilisiwe, lakini kamati hiyo imekataa mapendekezo hayo, mpaka uchunguzi huo ufanyike, kwa maslahi ya nchi.
Kati ya sababu ambazo zimekuwa zikitajwa za 'kufa' kwa kampuni hiyo, licha ya kupata mkopo, ni uagizwaji na uingizwaji wa matairi yaliyotumika na kuuzwa rejareja kwa bei ya chini.
Ingawa sababu nyingine kubwa ambayo imekuwa ikidaiwa 'kuiua' General Tyre, ni mwekezaji aliyepewa kiwanda, akiendesha kiwanda hicho kwa ubia na serikali ya Tanzania, kutotaka kuendelea na shughuli hiyo, kuwa utengenezaji wa matairi hakikuwa kipaumbele chake.
Akizungumza na watendaji wa shirika lililochukua nafasi ya Shirila la Kurekebisha Mashirika ya Umma, Consolidated Holding Corporation (CHC), jana baada ya POAC kupitisha hesabu za shirika hilo, mwenyekiti wa kamati hiyo, Bw. Kabwe Zitto, alisema kuwa kamati hiyo ya kuchunguza 'kifo' cha General Tyre itafuatilia matumizi ya mkopo huo wa NSSF, iwapo ulitumika kama ilivyokusudiwa na taratibu zilizotumika kukopesha.
"Katika suala la General Tyre nashukuru mmetuletea taarifa yake, lakini it is not detailed as expected (si ya kina kama ilivyotarajiwa)...sasa deni limefikia sh. bilioni 21.15...NSSF walikuwa wanataka kiwanda hiki kiuzwe, serikali nao wanataka kifilisiwe. Hatuwezi kuuza kiwanda hiki halafu nchi ibaki kutegemea matairi ya nje.
"Tumeunda timu ya wabunge wanne, kufanya uchunguzi wa kampuni hiyo, itakayokuwa na wabunge wanne, watatu wa kamati hii, mmoja kamati ya viwanda na biashara na mtu wa ofisa ya CAG, watu wa CHC mnatakiwa kutoa ushirikiano wa kutosha utakapotakiwa na tumeipatia hadidu za rejea tayari," alisema Bw. Zitto.
Alitaja hadidu hizo kuwa ni pamoja na kufuatilia matumizi ya mkopo waliokopa kutoka NSSF, taratibu zilizotumika, mali zilizokuwa zikimilikiwa na kampuni hiyo, msimamo wa serikali kutaka kuifilisi kampuni hiyo, iwapo una maslahi ya umma na kuangalia namna ya kuifufua.
"Tunahisi kuna mchazo mchafu, maana waliomba mkopo lakini wanasema hawawezi kuendesha...tuangalie mkopo ulivyotumika, taratibu za kupata mkopo huo...tunataka nchi ishindane katika kuzalisha bidhaa, tunataka kiwanda hiki kizalishe ajira kwa Watanzania.
issue za General tyre ni Zao la ufisadi nasikitikia kamati ya Zito Hawatofika popote katika hilo, Ukufuatilia kwa undani kilkichotokea general tyre hakina tofauti na EPA haya TUONEMWISHO WAKE
ReplyDeleteA.M CHILENDU this is not the matter of asking who did what, waliofilisi General tyre wanajulikana kamati ya bunge ina ubavu wa kubadili kitu au yale yale ya EPA
ReplyDeleteWell done POAC, baada ya kusema hayo, mimi nimefuatilia kazi zinazofanywa na kamti hizi ndizo zile zilizzotkiw kufanywa na wizara, endepo wizara zingekuwa makini! Kama wizara ya viwanda inashindwa kufuatilia maswala kama haya badala yake mawaziri wanakua wafunguzi wa matamasha! Leo waziri anafungua tamasha ya bia hii, kesho bongo flava, siku ingine kongamano... sioni umuhmu wakuwa na mawaziri wanamna hii! Kamati za bunge zichukue majaukumu ya wizara na wizara ziwe na makatibu tu!
ReplyDeleteZitto yuko makini,jinsi anavyopigania maslahi ya mashirika ya umma inaonyesha alivyo mzalendo wa hali ya juu,na kitu kizuri ni kwamba he's so rational katika kazi zake,i mean no one within CHADEMA matches his sense of judgement,ndo uzuri wa shule,kijana kaelimika,wachaga mpo???
ReplyDeleteHongera Zitto kwa ujasiri ambao umekuwa ukiuonyesha siku zote. Hapa suala la kuuza kiwanda haraka haraka halipo.Uchunguzi ufanyike lakini waliokifisadi kiwanda wanajulikana kinachofuata ni hatua gani zichukuliwe dhidi yao.
ReplyDeleteNimekunwa sana na kamati ya Kudumu ya mahesebu ya mashirika ya umma ambayo kwa kweli sasa mnafanya kazi na nampongeza jamaa na kijana wetu Mhe.Zitto Kabwe kwa kazi nzuri. na hii sasa ndiyo kazi kubwa ya shadow Government ambayo inakuwa watch dog kwa serikali iliyoko madarakani. ukianza kufuatilia mashirika ya umma yalikufaje utaumia sana kwani makada wa CCM wakikosa hela walikimbilia kwa mameneja miradi wa mashirika hayo na kuwatishia ili wawape hela na walifanikiwa kuzikomba. angalia mashamba ya kapunga, basuto, mbozi maize farm pamoja na misaada kutoka kwa wafadhili mashamba yale yalikufa na serikali badala ya kubuni miradi kwa vijana wasio na Ajira wawachia infrastructure zilizomo wakafanya kazi na kuzalisha na nasema wataizidi mbali serikali kiutendaji. Mhe. zitto ukimaliza General Tyre angalia na mashirika mengine kama unapresha unaweza kufa. tunakutakia utendaji na ufanisi mwema Mungu akutangulie.
ReplyDelete