18 March 2011

JK apigwa changa la macho bandari

Na Mwandishi Wetu

MRADI wa ujenzi wa jengo la kisasa la kuhifadhia magari katika bandari ya Dar es Salaam umepigwa 'stop' kwa kile kilichoelezwa, Rais kupewa ushauri tofauti na
matumizi  halisi kwa lengo za kunufaisha kampuni fulani zinazobebwa na wanasiasa kushindwa kupata zabuni hiyo.

Gazeti hili limedokezwa kuwa badala ya Rais kuelezwa ukweli kuhusu aina na matumizi ya jengo hilo alielezwa kuwa kinachojengwa ni sehemu ya kuuzia magari ndani ya bandari(bounded warehouse) kinyume na ukweli kwamba jengo hilo ni port reception facility ambayo kazi yake ni kupokea magari kutoka kwenye meli na  kuyahifadhi kwa muda maalumu uliowekwa na bandari kabla ya kuchukuliwa na kupelekwa bandari kavu za kuhifadhi magari ((ICDS) au moja kwa moja kwa wateja wenyewe au wa nje kwa maana ya transit cargo.

Majira lilidokeza kwamba mradi huo ulikuwa unajengwa kwenye eneo ambalo  haliwezi kutumika kwa kuweka kontena, shaba , mbolea na mambo kama hayo.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba wakati mchakato wa mradi huu ukipamba moto baadhi ya wanasiasa wenye ushawishi mkubwa ndani ya chama tawala na serikali na kuuzunguka uongozi wa wizara husika na kufanikiwa kupotosha malengo ya mradi huo.

Mchakato wa mradi huu ulianza tangu mwaka 2008 kutokana na ongezeko la shehena ya magari iliyokuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka huku nafasi ya kuyapokelea  ikionekana kuwa finyu jambo lililoifanya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutoa leseni kwa ICDS  kupokea magari na kutahifadhi nje ya bandari ili kupunguza tatizo la nafasi.

"ICDS za nje zinaweza kubadilisha matumizi ya maeneo yao lakini jukumu la bandari lakupokea magari kutoka kwenye meli na kuyahifadhi kwa muda yakisubiri kuchukuliwa liko palepale" kilieleza chanzo kimoja kutokana ndani ya TPA na kuongeza;

"Meli zinazokuja kwa sasa hivi zinakuwa zimepakia magari kati ya 1,500 mpaka 2,000 kwa mara moja  na kwa mwezi bandari inapokea magari kati ya 5,000 hadi 8,000 wakati ICDS zilizopo zina uwezo wa kuhifadhi magari 4,000 tu.Demand inaongezeka  and we must be always ahead of demand. Interest za wanasiasa  zikiachwa pembeni  huu mradi ni muhimu."

Majira lilipowasiliana kwa njia ya simu na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mawakala wa Kutoa Mizigo Bandari Bw. Salifius Mligo kuhusu ujenzi wa jengo hilo alisema ni makosa kwa Bandari inayokua kwa kasi kama Dar es Salaam kukosa huduma hiyo kwani ingesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza msongamano wa magari bandarini.

Bw. Mligo alisema kazi ya bandari siku zote ni kupakua na kukabidhi mizigo lakini uwiano ulipo sasa katika hilo ni mdogo.

"Multstorage facility ni jengo la kisasa la kuhifadhi magari kwa kwenda ju hewani. bandari lazima iwe na uwezo wa kjitegemea kieneo. Bandari ikiwe na uwezo wa kuhifadhi magari hata wafanyabiashara hawawezi kuringa " alisema Bw. Mligo na kuongeza kuwa   ukweli wa mradi huo  

4 comments:

  1. We mwandishi ushapata mshiko! Mie nilikua najipitia tu!

    ReplyDelete
  2. kikwete ss unaaibsha. yaan hiik n mara ya 10 kudanganywa na kupelekeshwa ka mwenda wazimu. rais huyu n fek

    ReplyDelete
  3. Kwanza hakuna kiongozi duniani ambae hapati nusura ya kudanganywa na ujue kua kiongozi wa nchi hawezi kufanya kila jambo yeye lazima kuwe na watu wa kumsaidia na mambo kama haya ya kutaka kudanganywa sio mageni katika dunia ya sasa ya udhalimu kwa hiyo hapo kiongozi wa nchi hana kosa ila awe makini zaidi kila mara miradi inapotaka kufanyika lakini kumwita ni feki sio busara ila labda wewe una chuki binafsi je hamuyaoni mazuri mangapi anayoyafanya mnaona pale jambo baya ima limefanywa na viongozi wengine wa ngazi za chini na kusahau mazuri ambayo anayafanya hakuna mwenye mema matupu bila makosa na yeye ni binaadam na kumbuka kua wapo wa chini yake madhalimu na mafisadi itakua sio busara kumlaumu yeye kwa kila jambo kama ni hivyo basi hakuna rais hata mmoja duniani ambae anafaa

    ReplyDelete
  4. wewe pmb hapo juu naona huna hoja kabsa. yaan unahalalsha kudanganywa kwa rais tena kwa mara nyng kias hcho? kama kiongoz wa juu anaeza kuwa zuzu na pmb kiass hcho unatarajia nan atakayemwajbsha wa chn. nadhan hujui maana ya kuwa kiongoz na uongoz n nn. wewe huna tofaut na pmb mwenzako kikwete

    ReplyDelete