Na Dunstan Bahai
MGOGORO kati ya vigogo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Jumuiya yake ya Vijana (UV-CCM) umezidi kuumuka kuhusiana na utendajiwa sekretarieti ya
chama hicho, inayotakiwa kujiuzulu kwa kushindwa kumshauri mwenyekiti wa chama hicho, Rais Jakaya Kikwete.
Baadhi ya vijana wa chama hicho wakiongozwa na aliyejitambulisha kwa jina la Bw. David Gaudencia Msuya, walisema jana kuwa hakuna sababu za sekretarieti hiyo kuendelea kuwepo madarakani kutokana na kushindwa kumsaidia Rais Kikwete.
Bw. Msuya alisema anaungana na kauli ya Umoja wa Vijana iliyotolewa Mjini Bagamoyo na Makamu Mwenyekiti wa Umoja huo wa Mkoa wa Pwani, Bw. Abdallah Ulega wakati akifungua Baraza la Umoja huo mkoani Pwani.
âKauli iliyotolewa mjini Bagamoyo iko sahihi kabisa kwani ni kweli sekretarieti hiyo haina inachofanya. Kumekuwa na migogoro mingi kwenye taasisi mbalimbali hasa za elimu, kweli inafikia hata vijana wa sekondari wanaandamana, itafikia wa msingi na wale wa chekechea nao wataandamana, alisema Bw. Msuya.
Kauli ya umoja huo ilitolewa majibu jana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, Bw. John Chiligati na Katibu Mkuu wa CCM Bw. Yusuf Makamba ambao kwa nyakati tofauti walisema kuwa hayo ni maoni ya vijana hao ambayo kwa mujibu wa katiba ya chama, wametumia haki yao ya msingi.
Hata hivyo Bw. Makamba hakuamini kama kweli kauli hiyo ilitolewa na Umoja wa Vijana na badala yake akadai huenda ni kauli zinazotokana na uchochezi wa magazeti, huku Chiligati akisema kikatiba vijana hao hawana mamlaka ya kuing'oa sekretarieti.
Ukweli ni kwamba sioni kazi inayofanywa na huyu Makamba. Mimi ninadhani elimu nayo ni tatizo. Hii kauli ya Chiligati haina mantiki yoyote, tena ninasema hawa viongozi waache kabisa tabia yao ya kutishia vijana, tunao uwezo wa kuwaondoa madarakani,alisema Bw. Msuya.
Makada hao ambao walikutana na baadhi ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana na baadhi yao kukataa kutajwa majina, waliwataka viongozi hao kujiuzulu badala ya kusubiri wanachama waandamane.
Bw. Msuya alisema umoja huo kikatiba una uwezo wa kuwaondoa madarakani viongozi hao kwa kuwa wijana wenyewe nao wamo kwenye nyadhifa za juu za chama na serikali.
Kwa mujibu wa Bw. Msuya, chama chenyewe ni kizuri na kiko imara, lakini kinaharibiwa na baadhi ya viongozi.
Bw. Msuya ambaye kitaaluma ni mwanasheria, alisisitiza kuwa ipo haja ya Mwenyekiti wa Taifa wa CCM ambaye ni Rais Kikwete kuwawajibisha kwa madai kuwa wanamsaliti yeye na taifa kwa ujumla.
Alisema si kwa upande wa viongozi tu wa CCM wanaomuangusha Rais, lakini hata wateule wake kama makatibu wakuu wa wizara na watendaji wengine, wamekuwa wakimsaliti.
Alitoa mfano hivi karibuni Rais Kikwete na Waziri Mkuu Mizengo Pinda, walitoa kauli kwa nyakati tofauti za kuchukuliwa hatua wale wote wanaouza sukari kwa bei ya zaidi ya sh. 1,700, lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa kwani sukari hiyo imeendelea kuuzwa sh. 2,000 hata maeneo ambako kuna viwanda.
UVCCM wana malengo mazuri sana ili kukinusuru Chama lakini tatizo umoja huo hauko imara kutokana na makundi ambayo kila kukicha yanaleta mpasuko. Pia kuna hili tatizo la mitandao ndani ya CCM. Mimi binafsi ni mkereketwa mkubwa wa CCM lakini ninasema wazi kuwa hata huyu Ridhiwani Kikwete kijana huyu amechangia sana kuleta mtafaruku ndani ya UVCCM. Kijana huyu aangaliwe sana asiogopwe kwa vile ni mtoto wa mkubwa eti na yeye tayari ana mtandao wake. Hajengi chama kabisa anakibomoa bila yeye kujua mbwembwe zimemzidi anajiona yeye ni yeye. Ninachoona mimi kufanyike jitihada za nguvu kuunganisha wanachama. Na hii mitandao ifutiliwe mbali kama kuna uwezekano. CCM ni moja lakini matabaka mengi kwa nini?
ReplyDeleteMie naona nyie mnaojiita wakereketwa ndio mnao tuulia chama chetu. Sasa unataka Ridhwani aone fitina dhidi ya baba yake inafanyika anyamaze? Lazima atajiweka sawa ili kumlinda. Wakati wa kampeni nyie wakereketwa mlimuachia mama Salma na Ridhwani na usalama wa Taifa wakaifanya kazi yote, eti sasa mnalia kunamakundi CCM pelekeni unafiki wenu huko. CCM ina wenyewe na Ridhwani ni mmoja wao.
ReplyDelete